Luka
14 Na pindi fulani yeye alipoenda ndani ya nyumba ya mtu fulani mmoja wa watawala wa Mafarisayo siku ya sabato ili kula mlo, wao walikuwa wakimchunguza sana. 2 Na, tazama! alikuwapo mbele yake mtu fulani aliyekuwa na ugonjwa wa chovya. 3 Kwa hiyo kwa kujibu Yesu aliwaambia wale wenye ujuzi mwingi katika Sheria na Mafarisayo, akisema: “Je, yaruhusika kisheria kuponya siku ya sabato au sivyo?” 4 Lakini wao wakafuliza kukaa kimya. Ndipo akashika huyo mtu, akamponya na kumwacha aende zake. 5 Naye akawaambia: “Ni nani kati yenu, ikiwa mwana wake au fahali aanguka ndani ya kisima, hatamtoa nje mara hiyo siku ya sabato?” 6 Nao hawakuweza kurudisha jibu juu ya mambo hayo.
7 Ndipo akaendelea kuwaambia kielezi watu walioalikwa, kwa kuwa aliangalia jinsi walivyokuwa wakijichagulia wenyewe mahali pa kutokeza zaidi sana kwa ajili yao wenyewe, akiwaambia: 8 “Wakati ualikwapo na mtu fulani kwenye karamu ya ndoa, usijilaze mahali pa kutokeza zaidi sana. Labda mtu fulani mashuhuri zaidi kuliko wewe huenda akawa wakati huo amekwisha kualikwa naye, 9 naye aliyekualika wewe na yeye, atakuja na kukuambia, ‘Acha mtu huyu apate mahali hapo.’ Na ndipo wewe utakapoanza kuondoka kwa aibu kukalia mahali pa chini zaidi sana. 10 Lakini ualikwapo, nenda uegame katika mahali pa chini zaidi sana, ili wakati mtu ambaye amekualika ajapo akuambie, ‘Rafiki, nenda juu zaidi.’ Ndipo wewe utakapokuwa na heshima mbele ya wageni-waalikwa wenzako wote. 11 Kwa maana kila mtu ajikwezaye mwenyewe atanyenyekezwa na yeye ajinyenyekezaye mwenyewe atakwezwa.”
12 Halafu akaendelea pia kumwambia mtu aliyemwalika: “Uandaapo mlo-mkuu au mlo wa jioni, usiite marafiki wako au ndugu zako au jamaa zako au majirani walio matajiri. Labda wakati fulani huenda nao pia wakakualika na hilo lingekuwa kukurudishia malipo. 13 Lakini wakati uandaapo karamu, alika maskini, viwete, vilema, vipofu; 14 nawe utakuwa mwenye furaha, kwa sababu wao hawana kitu cha kukulipa nacho. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa walio waadilifu.”
15 Aliposikia mambo hayo mtu fulani kati ya wageni-waalikwa-wenzi alimwambia: “Mwenye furaha ni yeye alaye mkate katika ufalme wa Mungu.”
16 Yesu akamwambia: “Mtu fulani alikuwa akiandaa mlo wa jioni mkubwa, naye akaalika wengi. 17 Naye alimtuma nje mtumwa wake kwenye saa ya huo mlo wa jioni ili awaambie walioalikwa, ‘Njoni, kwa sababu mambo sasa yako tayari.’ 18 Lakini wote kwa namna moja wakaanza kutoa udhuru. Yule wa kwanza akamwambia, ‘Nilinunua shamba nami nahitaji kutoka niende kuliona; nakuomba, Niwie radhi.’ 19 Na mwingine akasema, ‘Nilinunua jozi tano za ng’ombe nami ninaenda kuwachunguza; nakuomba, Niwie radhi.’ 20 Na bado mwingine akasema, ‘Nimetoka kuoa mke sasa hivi na kwa sababu hii siwezi kuja.’ 21 Kwa hiyo yule mtumwa akaja akaripoti mambo haya kwa bwana-mkubwa wake. Ndipo mwenye nyumba akawa na hasira ya kisasi na kumwambia mtumwa wake, ‘Toka uende upesi uingie katika zile njia pana na barabara ndogo za jiji, uwaingize humu maskini na viwete na vipofu na vilema.’ 22 Baada ya muda yule mtumwa akasema, ‘Bwana-mkubwa, uliloagiza limefanywa, na bado mna nafasi.’ 23 Naye bwana-mkubwa akamwambia yule mtumwa, ‘Toka uende uingie barabarani na mahali palipozungushiwa ua, na uwashurutishe waingie, ili nyumba yangu ipate kujazwa. 24 Kwa maana nawaambia nyinyi watu, Hakuna hata mmoja wa watu wale walioalikwa ambaye atapata mwonjo wa mlo wangu wa jioni.’”
25 Sasa umati mkubwa ulikuwa ukisafiri pamoja naye, naye akageuka na kuwaambia: 26 “Yeyote akinijia naye hachukii baba yake na mama na mke na watoto na akina ndugu na akina dada, ndiyo, na hata nafsi yake mwenyewe, yeye hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 Yeyote yule asiyechukua mti wake wa mateso na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28 Kwa kielelezo, ni nani kati yenu atakaye kujenga mnara asiyeketi kwanza na kupiga hesabu ya gharama, ili aone kama ana kiasi cha kutosha kuukamilisha? 29 Kama sivyo, yeye angeweza kuuwekea msingi lakini asiweze kuumaliza, na watazamaji wote wangeweza kuanza kumdhihaki, 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kumaliza.’ 31 Au ni mfalme gani, anayeenda kukutana na mfalme mwingine vitani, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kama yeye aweza akiwa na askari elfu kumi kukabiliana na yule mtu ajaye dhidi yake pamoja na elfu ishirini? 32 Ikiwa, kwa kweli, hawezi kufanya hivyo, basi yule awapo bado yuko mbali sana yeye hutuma nje baraza la mabalozi na kuomba amani. 33 Hivyo, nyinyi mwaweza kuwa na hakika, hakuna hata mmoja kati yenu asiyesema kwaheri kwa mali zake zote awezaye kuwa mwanafunzi wangu.
34 “Chumvi, kwa hakika, ni bora. Lakini ikiwa hata hiyo chumvi yapoteza nguvu yayo, itakolezwa kwa kitu gani? 35 Hiyo haifai kwa ajili ya udongo wala kwa ajili ya mbolea. Watu huitupa nje. Acheni yeye aliye na masikio ya kusikiliza, asikilize.”