1 Timotheo
5 Usichambue mwanamume mzee kwa ukali. Kinyume chake, msihi sana kama baba, wanaume vijana zaidi kama ndugu, 2 wanawake wazee zaidi kama mama, wanawake vijana zaidi kama dada kwa usafi wote wa kiadili.
3 Heshimu wajane ambao ni wajane kwelikweli. 4 Lakini ikiwa mjane yeyote ana watoto au wajukuu, acha hawa wajifunze kwanza kuzoea ujitoaji-kimungu kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe na kufuliza kulipa wazazi na babu na nyanya zao fidia ipasayo, kwa maana hili ni lenye kukubalika machoni pa Mungu. 5 Basi mwanamke ambaye kwa kweli ni mjane na mkiwa kabisa ametia tumaini lake katika Mungu na hudumu katika dua na sala usiku na mchana. 6 Lakini yule ajitiaye katika kufurahisha hisi za mwili ni mfu ingawa yuko hai. 7 Kwa hiyo wewe fuliza kutoa amri hizi, ili wao wapate kuwa wasiolaumika. 8 Hakika ikiwa yeyote hawaandalii kitu wale walio wake mwenyewe, na hasa kwa ajili ya wale walio washiriki wa nyumbani mwake, ameikana imani naye ni mbaya zaidi kuliko mtu asiye na imani.
9 Acha mjane ambaye amekuwa mwenye umri usiopungua miaka sitini, mke wa mume mmoja awekwe katika orodha, 10 mwenye kutolewa ushahidi kwa kazi zilizo bora, ikiwa alilea watoto, ikiwa alipokea wageni, ikiwa aliosha miguu ya watakatifu, ikiwa alisaidia wale wenye kuwa katika dhiki, ikiwa yeye alifuata kwa bidii yenye kuendelea kila kazi njema.
11 Kwa upande mwingine, kataa wajane walio vijana zaidi, kwa maana wakati misukumo yao ya kingono imekuja kati yao na Kristo, wao hutaka kuolewa, 12 wakiwa na hukumu kwa sababu wamekosa kujali wonyesho wa kwanza wa imani. 13 Wakati huohuo wao hujifunza pia kuwa wasio na shughuli, wakizurura huku na huku kwenye nyumba; ndiyo, si wakiwa wasio na shughuli tu, bali pia wapiga-porojo na wajiingizaji katika mambo ya watu wengine, wakiongea juu ya mambo yasiyowapasa. 14 Kwa hiyo nataka wajane walio vijana zaidi waolewe, wazae watoto, wasimamie watu wa nyumbani, wasimpe mpingaji kichocheo chochote cha kutukana. 15 Kwa kweli, tayari baadhi yao wamegeuzwa kando kumfuata Shetani. 16 Ikiwa mwanamke yeyote mwenye kuamini ana wajane, acha yeye awasaidie wao, na acha kutaniko lisiwe chini ya mzigo wenye kulemea. Ndipo laweza kusaidia wale ambao ni wajane kwelikweli.
17 Acha wanaume wazee wasimamiao katika njia bora wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa wale wafanyao kazi kwa bidii katika kusema na kufundisha. 18 Kwa maana andiko lasema: “Lazima usimfunge kinywa fahali apurapo nafaka”; pia: “Mtenda-kazi astahili mshahara wake.” 19 Usikubali shtaka dhidi ya mwanamume mzee, ila tu kwa uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu. 20 Karipia mbele ya watazamaji wote watu wazoeao dhambi, ili wale wengine pia wapate kuwa na hofu. 21 Nakuagiza wewe kwa uzito mbele ya Mungu na Kristo Yesu na malaika-wachaguliwa ushike mambo haya bila kuhukumu mapema, bila kufanya jambo lolote kulingana na mwelekeo wenye kuegemea upande.
22 Usiweke kamwe mikono yako haraka-haraka juu ya mtu yeyote; wala usiwe mshiriki katika dhambi za wengine; jihifadhi mwenyewe ukiwa safi kiadili.
23 Usinywe maji tena kamwe, bali tumia divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako na visa vyako vya ugonjwa vya mara nyingi.
24 Dhambi za watu wengine hudhihirika waziwazi kwa watu wote, zikiongoza moja kwa moja kwenye hukumu, lakini kwa habari ya watu wengine pia dhambi zao hudhihirika baadaye. 25 Katika njia ileile pia kazi zilizo bora hudhihirika waziwazi kwa watu wote na zile zilizo tofauti haziwezi kuwekwa zikiwa zimefichwa.