2 Petro
3 Wapendwa, sasa hii ndiyo barua ya pili ninayowaandikia nyinyi, ambayo katika hiyo, kama katika ile yangu ya kwanza, ninaamsha uwezo wenu mwangavu wa kufikiri kwa njia ya kikumbusha, 2 kwamba mwapaswa kukumbuka semi zilizosemwa hapo awali na manabii watakatifu na amri ya Bwana na Mwokozi kupitia mitume wenu. 3 Kwa maana mwajua hili kwanza, kwamba katika siku za mwisho watakuja wadhihaki pamoja na dhihaka zao, wakiendelea kulingana na tamaa zao wenyewe 4 na kusema: “Kuko wapi kuwapo kwake huku kulikoahidiwa? Kwani, kutoka siku baba zetu wa zamani walipolala katika kifo, mambo yote yanaendelea sawasawa kabisa kama kutoka mwanzo wa kuumba.”
5 Kwa maana, kulingana na kutaka kwao, jambo hili huponyoka kujali kwao, kwamba mbingu zilikuwako tangu zamani za kale na dunia ikisimama kwa kutungamana kutoka katika maji na katikati ya maji kwa neno la Mungu; 6 na kwa njia hizo ulimwengu wa wakati huo ulipatwa na uangamizo ulipogharikishwa kwa maji. 7 Lakini kwa neno hilohilo mbingu na dunia zilizopo sasa zimewekwa akiba kwa ajili ya moto na zinawekwa akiba hadi siku ya hukumu na ya uangamizo wa watu wasiomwogopa Mungu.
8 Hata hivyo, wapendwa, acheni jambo hili moja lisiwe likiponyoka kujali kwenu, kwamba siku moja kwa Yehova ni kama miaka elfu na miaka elfu kama siku moja. 9 Yehova si wa polepole kwa habari ya ahadi yake, kama watu fulani waonavyo kuwa ni upolepole, bali yeye ni mwenye subira kwenu kwa sababu hataki yeyote aangamizwe bali hutaka wote wafikie toba. 10 Lakini siku ya Yehova itakuja kama mwizi, ambayo katika hiyo mbingu zitapitilia mbali kwa kelele ya kuchatachata, lakini elementi zikiwa moto sana zitafumuliwa, na dunia na kazi zilizo ndani yayo zitagunduliwa.
11 Kwa kuwa vitu vyote hivi vitafumuliwa hivyo, nyinyi mwapaswa kuwa watu wa namna gani katika matendo matakatifu ya mwenendo na vitendo vya ujitoaji-kimungu, 12 mkingojea na kuweka karibu akilini kuwapo kwa siku ya Yehova, ambayo kupitia kwayo mbingu zikiwa zimewaka moto zitafumuliwa na elementi zikiwa moto sana zitayeyuka! 13 Lakini ziko mbingu mpya na dunia mpya ambazo tunangojea kulingana na ahadi yake, na katika hizo uadilifu utakaa.
14 Kwa sababu hiyo, wapendwa, kwa kuwa mnangojea mambo haya, fanyeni kabisa yote mwezayo ili mwishowe mpatikane naye mkiwa bila doa na bila waa na katika amani. 15 Zaidi ya hilo, ioneni subira ya Bwana wetu kuwa wokovu, kama vile ndugu yetu mpendwa Paulo, kulingana na hekima aliyopewa alivyowaandikia nyinyi pia, 16 akisema juu ya mambo haya kama afanyavyo pia katika barua zake zote. Katika hizo, hata hivyo, mna mambo fulani magumu kuelewa, ambayo wale wasiofundishwa na wasio imara wanayapotoa, kama wafanyavyo na Maandiko mengine pia, kwa uangamizo wao wenyewe.
17 Kwa hiyo, nyinyi, wapendwa, mkiwa mnakuwa na ujuzi huu wa kimbele, iweni wenye kulinda ili msipate kuongozwa kando pamoja nao kwa kosa la watu wanaokaidi sheria na kuanguka kutoka kwenye uimara wenu wenyewe. 18 La, bali endeleeni kukua katika fadhili isiyostahiliwa na ujuzi juu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kwake uwe utukufu sasa na pia hadi siku ya umilele.