1 Yohana
4 Wapendwa, msiamini kila usemi uliopuliziwa, lakini jaribuni semi zilizopuliziwa ili kuona kama hizo zatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wasio wa kweli wameenda kuingia katika ulimwengu.
2 Mwapata ujuzi juu ya usemi uliopuliziwa kutoka kwa Mungu kwa hili: Kila usemi uliopuliziwa ambao huungama Yesu Kristo kuwa alikuja akiwa mwili hutokana na Mungu, 3 lakini kila usemi uliopuliziwa ambao hauungami Yesu hautokani na Mungu. Zaidi ya hilo, huu ndio usemi uliopuliziwa wa mpinga-Kristo ambao mmesikia ulikuwa ukija, na sasa tayari umo katika ulimwengu.
4 Nyinyi mwatokana na Mungu, watoto wadogo, nanyi mmeshinda watu hao, kwa sababu yeye aliye katika muungano nanyi ni mkubwa zaidi kuliko yeye ambaye yumo katika muungano na ulimwengu. 5 Wao watokana na ulimwengu; hiyo ndiyo sababu wasema kile kitokacho kwa ulimwengu na ulimwengu huwasikiliza wao. 6 Sisi twatokana na Mungu. Yeye ambaye hupata ujuzi juu ya Mungu hutusikiliza; yeye ambaye hatokani na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo sisi tunavyojua usemi uliopuliziwa wa kweli na usemi uliopuliziwa wa kosa.
7 Wapendwa, acheni tuendelee kupendana, kwa sababu upendo ni wa kutoka kwa Mungu, na kila mtu ambaye hupenda amezaliwa kutokana na Mungu na hupata ujuzi juu ya Mungu. 8 Yeye ambaye hapendi hajaja kujua Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo. 9 Kwa hili upendo wa Mungu ulifanywa dhahiri katika kisa chetu, kwa sababu Mungu alituma Mwana wake mzaliwa-pekee kuingia katika ulimwengu ili tuweze kupata uhai kupitia kwake. 10 Upendo uko hivi, si kwamba sisi tumempenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda akamtuma Mwana wake kuwa dhabihu yenye kufunika kwa ajili ya dhambi zetu.
11 Wapendwa, ikiwa hivi ndivyo Mungu alivyotupenda, basi sisi wenyewe tuko chini ya wajibu kupendana. 12 Hakuna yeyote ambaye amemwona Mungu wakati wowote. Ikiwa twaendelea kupendana, Mungu hukaa katika sisi na upendo wake unafanywa mkamilifu katika sisi. 13 Kwa hili sisi twapata ujuzi kwamba tunakaa katika muungano na yeye na yeye katika muungano na sisi, kwa sababu ametupa roho yake. 14 Kwa kuongezea, sisi wenyewe tumemwona na tunatoa ushahidi kwamba Baba amemtuma Mwana wake kuwa Mwokozi wa ulimwengu. 15 Yeyote yule afanyaye ungamo kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu, Mungu hukaa katika muungano na mtu kama huyo na yeye katika muungano na Mungu. 16 Na sisi wenyewe tumekuja kujua na tumeamini upendo ambao Mungu anao katika kisa chetu.
Mungu ni upendo, na yeye ambaye hukaa katika upendo hukaa katika muungano na Mungu na Mungu hukaa katika muungano na yeye. 17 Hivi ndivyo upendo umefanywa mkamilifu pamoja na sisi, kwamba tupate kuwa na uhuru wa usemi siku ya hukumu, kwa sababu, kama vile huyo alivyo, ndivyo tulivyo sisi wenyewe katika ulimwengu huu. 18 Hakuna hofu katika upendo, lakini upendo mkamilifu hutupa hofu nje, kwa sababu hofu hufanyiza kizuizi. Kwa kweli, yeye ambaye yuko chini ya hofu hajafanywa mkamilifu katika upendo. 19 Kwa habari yetu, twapenda, kwa sababu yeye alitupenda sisi kwanza.
20 Ikiwa yeyote atoa taarifa: “Mimi nampenda Mungu,” na bado anachukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana yeye ambaye hapendi ndugu yake, ambaye ameona, hawezi kuwa anapenda Mungu, ambaye hajaona. 21 Na amri hii tunayo kutoka kwake, kwamba yeye ambaye hupenda Mungu apaswa kuwa anapenda ndugu yake pia.