5 Ndipo wakakusanyika pamoja na kupanda, wafalme watano wa Waamori,+ mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi, mfalme wa Egloni, hao na kambi zao zote, nao wakaanza kupiga kambi juu ya Gibeoni na kupiga vita juu yake.