Luka
9 Ndipo akawaita pamoja wale kumi na wawili akawapa nguvu na mamlaka juu ya roho wote waovu na kuponya magonjwa. 2 Na kwa hiyo akawatuma kwenda kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya, 3 naye akawaambia: “Msichukue kitu chochote kwa ajili ya safari, wala fimbo wala mfuko wa chakula, wala mkate wala sarafu ya fedha; wala msiwe na mavazi mawili ya ndani. 4 Lakini popote pale mwingiapo katika nyumba, kaeni hapo na mwondoke kutoka hapo. 5 Na popote pale watu wasipowapokea nyinyi, mnapoondoka katika jiji hilo yakung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushahidi dhidi yao.” 6 Ndipo walipoanza kuondoka wakapita katika hilo eneo kutoka kijiji hadi kijiji, wakitangaza habari njema na kufanya maponyo kila mahali.
7 Sasa Herode mtawala wa wilaya akasikia juu ya mambo yote yaliyokuwa yakitukia, naye alikuwa katika fadhaa kubwa kwa sababu ya kusemwa na baadhi ya watu kwamba Yohana alikuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu, 8 lakini na wengine kwamba Eliya alikuwa ameonekana, lakini bado na wengine kwamba mtu fulani mmoja wa manabii wa kale alikuwa amefufuliwa. 9 Herode akasema: “Yohana nilimkata kichwa. Basi, ni nani huyu ambaye juu yake ninasikia mambo ya namna hiyo?” Kwa hiyo alikuwa akitafuta sana kumwona.
10 Na mitume waliporudi wakamsimulia mambo waliyokuwa wameyafanya. Ndipo akawachukua waambatane naye na kujiondoa kwenda faraghani kuingia katika jiji liitwalo Bethsaida. 11 Lakini umati ulipopata kujua hilo, ukamfuata. Naye akawapokea kwa fadhili na kuanza kuwaambia juu ya ufalme wa Mungu, naye akawaponya wale wenye kuhitaji ponyo. 12 Ndipo mchana ukaanza kushuka. Wale kumi na wawili sasa wakaja na kumwambia: “Ambia umati uende, ili upate kuingia katika vijiji na upande wa mashambani wenye kuzunguka na kujipatia makao na upate chakula, kwa sababu huku nje sisi tuko katika mahali pa upweke.” 13 Lakini akawaambia: “Nyinyi wapeni kitu cha kula.” Wakasema: “Sisi hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, isipokuwa labda sisi wenyewe twende na kununua vyakula kwa ajili ya watu wote hawa.” 14 Kwa kweli, walikuwa karibu wanaume elfu tano. Lakini akawaambia wanafunzi wake: “Waagizeni waegame kama kwenye milo, vikundi vikundi vya karibu hamsini kila kimoja.” 15 Nao wakafanya hivyo na kuwaegamisha wote. 16 Ndipo akichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki na kuvimega akaanza kuwapa wanafunzi waviweke mbele ya umati. 17 Kwa hiyo wote wakala wakashiba, na ziada waliyokuwa nayo ikaokotwa, vikapu kumi na viwili vya vipande vidogo.
18 Baadaye, alipokuwa akisali peke yake, wanafunzi walimjia pamoja, naye akawauliza swali, akisema: “Umati unasema kwamba mimi ni nani?” 19 Kwa kujibu wakasema: “Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya, na wengine bado, kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuliwa.” 20 Ndipo akawaambia: “Ingawa hivyo, nyinyi mwasema mimi ni nani?” Petro akasema kwa kujibu: “Kristo wa Mungu.” 21 Ndipo kwa maongezi ya kuwasisitizia akawaagiza wasiwe wakiambia yeyote hilo, 22 lakini akasema: “Mwana wa binadamu lazima apatwe na mateso mengi na kukataliwa na wanaume wazee na makuhani wakuu na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu afufuliwe.”
23 Ndipo akaendelea kuwaambia wote: “Ikiwa yeyote ataka kunifuata, na ajikane mwenyewe na kuchukua mti wake wa mateso siku baada ya siku na kunifuata kwa kuendelea. 24 Kwa maana yeyote yule atakaye kuokoa nafsi yake ataipoteza; lakini yeyote yule aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeiokoa. 25 Kwa kweli, mtu ajinufaisha mwenyewe nini ikiwa atapata faida ya kuwa na ulimwengu wote lakini aipoteze nafsi yake mwenyewe au apate hasara? 26 Kwa maana awaye yote yule mwenye kuaibika juu yangu na juu ya maneno yangu, Mwana wa binadamu ataaibika juu ya huyo awasilipo katika utukufu wake na ule wa Baba na wa malaika watakatifu. 27 Lakini nawaambia nyinyi kwa kweli, Kuna baadhi ya wale ambao wamesimama hapa ambao hawataonja kifo hata kidogo mpaka kwanza wauone ufalme wa Mungu.”
28 Kwa kweli kabisa, karibu siku nane baada ya maneno hayo, alichukua pamoja naye Petro na Yohana na Yakobo wakapanda kuingia katika mlima ili kusali. 29 Naye alipokuwa akisali kuonekana kwa uso wake kukawa tofauti na vao lake likawa jeupe kwa kumeremeta. 30 Pia, tazama! wanaume wawili walikuwa wakiongea naye, waliokuwa ni Musa na Eliya. 31 Hawa walionekana wakiwa na utukufu nao wakaanza kuongea juu ya kuondoka kwake alikokusudiwa kutimiza Yerusalemu. 32 Sasa Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipopata kuamka kabisa waliona utukufu wake na wale wanaume wawili waliosimama pamoja naye. 33 Nao walipokuwa wakitengwa kutoka kwake, Petro akamwambia Yesu: “Mfunzi, ni vizuri kwetu kuwa hapa, kwa hiyo na tusimamishe mahema matatu, moja lako na moja la Musa na moja la Eliya,” yeye akiwa hang’amui alilokuwa akisema. 34 Lakini alipokuwa akisema mambo haya wingu lilifanyika na kuanza kuwafunika kivuli. Walipokuwa wakiingia katika wingu, wakawa wenye hofu. 35 Na sauti ikaja kutoka katika lile wingu, ikisema: “Huyu ni Mwana wangu, yule ambaye amechaguliwa. Msikilizeni yeye.” 36 Na ile sauti ilipokuwa ikitukia Yesu alionekana akiwa peke yake. Lakini wao wakafuliza kukaa wanyamavu na hawakuripoti kwa yeyote siku hizo lolote la mambo waliyoona.
37 Siku iliyofuata, waliposhuka kutoka mlimani, umati mkubwa ulikutana naye. 38 Na, tazama! mwanamume mmoja akapaaza kilio kutoka katika umati, akisema: “Mwalimu, nakuomba umtazame kidogo mwana wangu, kwa sababu yeye ni mzaliwa-pekee wangu, 39 na, tazama! roho humchukua, na kwa ghafula yeye hupaaza kilio, na huyo roho humtupa katika mifurukuto pamoja na povu, naye hamwachi kabisa baada ya kumchubua. 40 Nami niliomba wanafunzi wako wamfukuze huyo roho, lakini hawakuweza.” 41 Kwa kujibu Yesu akasema: “Ewe kizazi kisicho na imani na kilichopotoka, ni kwa muda gani lazima niendelee kuwa pamoja nanyi na kuchukuliana nanyi? Ongoza mwana wako upande huu.” 42 Lakini hata alipokuwa akikaribia, yule roho mwovu akambwaga kwenye ardhi na kumfurukutisha kwa nguvu nyingi. Hata hivyo, Yesu akamkemea yule roho asiye safi na kumponya mvulana naye akamkabidhi kwa baba yake. 43 Basi, wote wakaanza kustaajabishwa na nguvu yenye ukuu ya Mungu.
Sasa walipokuwa wote wakistaajabia mambo yote aliyokuwa akifanya, aliwaambia wanafunzi wake: 44 “Yapeni maneno hayo makao katika masikio yenu, kwa maana Mwana wa binadamu amekusudiwa kukabidhiwa mikononi mwa watu.” 45 Lakini wao wakaendelea kuwa hawaelewi usemi huo. Kwa kweli, ulisitiriwa kutoka kwao ili wasipate kuufahamu, nao waliogopa kumuuliza swali juu ya usemi huo.
46 Ndipo kuwazawaza kukaingia miongoni mwao kuhusu nani angekuwa ndiye mkubwa zaidi sana kati yao. 47 Yesu, akijua kuwazawaza kwa mioyo yao, akachukua mtoto mchanga, akamweka kando yake 48 na kuwaambia: “Yeyote yule apokeaye mtoto mchanga huyu juu ya msingi wa jina langu anipokea mimi pia, na yeyote yule anipokeaye mimi ampokea pia aliyenituma mimi. Kwa maana yeye ajiendeshaye mwenyewe kama aliye mdogo zaidi miongoni mwenu nyote ndiye aliye mkubwa.”
49 Kwa kujibu Yohana akasema: “Mfunzi, tuliona mtu fulani akitoa roho waovu kwa utumizi wa jina lako nasi tukajaribu kumzuia, kwa sababu yeye hafuatani na sisi.” 50 Lakini Yesu akamwambia: “Nyinyi watu msijaribu kumzuia, kwa maana asiye dhidi yenu yuko upande wenu.”
51 Siku zilipokuwa sasa zikija kwenye ukamili ili yeye achukuliwe juu, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu. 52 Kwa hiyo akatuma wajumbe kumtangulia. Nao wakashika njia yao kwenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, kumfanyia tayarisho; 53 lakini hawakumpokea, kwa sababu uso wake ulikuwa umekazwa kwenda Yerusalemu. 54 Wanafunzi Yakobo na Yohana walipoona hilo wakasema: “Bwana, je, wataka tuambie moto uteremke kutoka mbinguni na kuwaangamiza?” 55 Lakini yeye akageuka akawakemea. 56 Basi wakaenda kwenye kijiji tofauti.
57 Sasa walipokuwa wakienda barabarani, mtu fulani akamwambia: “Hakika mimi nitakufuata wewe kokote ambako huenda ukaenda.” 58 Naye Yesu akamwambia: “Mbweha wana mapango na ndege wa mbinguni wana viota, lakini Mwana wa binadamu hana mahali popote pa kulaza kichwa chake.” 59 Ndipo akaambia mwingine: “Uwe mfuasi wangu.” Mtu huyo akasema: “Niruhusu kwanza niondoke nikazike baba yangu.” 60 Lakini yeye akamwambia: “Acha wafu wazike wafu wao, lakini wewe enda zako na kuutangaza kotekote ufalme wa Mungu.” 61 Na mwingine bado akasema: “Hakika nitakufuata wewe, Bwana; lakini kwanza niruhusu mimi niwaambie kwaheri wale walio katika watu wa nyumbani mwangu.” 62 Yesu akamwambia: “Hakuna mtu ambaye ameweka mkono wake kwenye plau naye atazama kwenye mambo yaliyo nyuma aufaaye sana ufalme wa Mungu.”