Ufunuo
9 Na malaika wa tano akapuliza tarumbeta yake. Nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka kutoka mbinguni hadi kwenye dunia, naye akapewa ufunguo wa shimo la abiso. 2 Naye akalifungua shimo la abiso, na moshi ukapanda kutoka hilo shimo kama moshi wa tanuri kubwa, nalo jua likatiwa giza, pia hewa, kwa moshi wa shimo. 3 Na kutoka katika huo moshi nzige wakaja juu ya dunia; nao wakapewa mamlaka, mamlaka ileile kama waliyo nayo nge wa dunia. 4 Nao wakaambiwa wasidhuru mimea ya dunia wala kitu chochote cha kijani kibichi wala mti wowote, ila tu wanadamu wale wasio na muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.
5 Na hao nzige walipewa ruhusa, si wawaue, bali kwamba hawa wateswe-teswe miezi mitano, na mateso juu yao yalikuwa kama kuteswa-teswa na nge wakati ampigapo mwanadamu. 6 Na katika siku hizo wanadamu watatafuta kifo lakini hawatakipata kwa vyovyote, nao watatamani kufa lakini kifo chafuliza kuwakimbia.
7 Na mifanano ya hao nzige ilikuwa kama farasi waliotayarishwa kwa ajili ya pigano; na juu ya vichwa vyao kulikuwa na kilichoonekana kuwa mataji yaliyo kama dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanaume, 8 lakini walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama yale ya simba; 9 nao walikuwa na mabamba ya kifuani kama mabamba ya kifuani ya chuma. Na mvumo wa mabawa yao ulikuwa kama mvumo wa magari ya farasi wengi wakikimbia kuingia katika pigano. 10 Pia, wana mikia na vichomeo kama nge; na katika mikia yao mna mamlaka yao ya kuumiza wanadamu miezi mitano. 11 Wana mfalme juu yao, yule malaika wa abiso. Katika Kiebrania jina lake ni Abadoni, lakini katika Kigiriki ana jina Apolioni.
12 Ole mmoja umepita. Tazama! Ole mbili zaidi zinakuja baada ya mambo haya.
13 Na malaika wa sita akapuliza tarumbeta yake. Nami nikasikia sauti moja kutoka pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya Mungu 14 ikimwambia malaika wa sita, aliyekuwa na tarumbeta: “Wafungue malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.” 15 Na hao malaika wanne wakafunguliwa, ambao wametayarishwa kwa ajili ya saa na siku na mwezi na ule mwaka, kuua theluthi moja ya wanadamu.
16 Na idadi ya majeshi ya askari wapanda-farasi ilikuwa makumi mawili ya maelfu ya makumi ya maelfu: nikasikia idadi yao. 17 Na hivi ndivyo nilivyoona wale farasi katika ono, na wale waketio juu yao: walikuwa na mabamba ya kifuani mekundu-moto na hayasinthi-bluu na manjano-sulfa; na vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao moto na moshi na sulfa vikatoka. 18 Kwa hizo tauni tatu theluthi moja ya wanadamu waliuawa, kutokana na moto na moshi na sulfa vilivyotoka katika vinywa vyao. 19 Kwa maana mamlaka ya hao farasi imo katika vinywa vyao na katika mikia yao; kwa maana mikia yao ni kama nyoka na ina vichwa, nao wafanya dhara kwa hivyo.
20 Lakini wale wengine kati ya wanadamu ambao hawakuuawa kwa hizo tauni hawakutubu juu ya kazi za mikono yao, ili wasiabudu roho waovu na sanamu za dhahabu na fedha na shaba na mawe na miti, ambazo haziwezi kuona wala kusikia wala kutembea; 21 nao hawakutubu juu ya mauaji-kimakusudi yao wala juu ya mazoea yao ya kuwasiliana na roho wala juu ya uasherati wao wala juu ya wizi wao.