4 Hivyo Ahabu akaenda nyumbani kwake, akiwa mwenye kinyongo na mwenye huzuni kwa sababu ya lile neno ambalo Nabothi Myezreeli alikuwa amemwambia, aliposema: “Sitakupa fungu la urithi la mababu zangu.” Kisha akalala kitandani pake, akakaa akiwa amegeuza uso wake,+ naye hakula mkate.