Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 25
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Sheria kuhusu kumpiga mtu viboko (1-3)

      • Usimfunge kinywa ng’ombe dume anapopura (4)

      • Ndoa ya ndugu mkwe (5-10)

      • Kumkamata mtu sehemu zisizofaa anapopigana (11, 12)

      • Mizani na vipimo sahihi (13-16)

      • Waamaleki wataangamizwa (17-19)

Kumbukumbu la Torati 25:1

Marejeo

  • +Kum 16:18; 17:8, 9; 19:16, 17
  • +Kut 23:6; 2Nya 19:6; Met 17:15; 31:9

Kumbukumbu la Torati 25:2

Marejeo

  • +Met 10:13; 20:30; 26:3; Lu 12:48; Ebr 2:2

Kumbukumbu la Torati 25:3

Marejeo

  • +2Ko 11:24

Kumbukumbu la Torati 25:4

Marejeo

  • +Met 12:10; 1Ko 9:9; 1Ti 5:18

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/1/2012, uku. 30

    5/1/1989, uku. 17

  • Fahirishi ya Machapisho

    w12 5/1 30

Kumbukumbu la Torati 25:5

Marejeo

  • +Mwa 38:7, 8; Ru 4:5; Mk 12:19

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 371

    Tafsiri ya Ulimwengu Mpya, uku. 2027

Kumbukumbu la Torati 25:6

Marejeo

  • +Mwa 38:9; Ru 4:10, 17
  • +Hes 27:1, 4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 371

Kumbukumbu la Torati 25:9

Marejeo

  • +Ru 4:7

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 371

    Mnara wa Mlinzi,

    9/15/2004, uku. 26

  • Fahirishi ya Machapisho

    w04 9/15 26

Kumbukumbu la Torati 25:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “jina la nyumba.” Tnn., “jina lake.”

  • *

    Tnn., “Nyumba.”

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 371

Kumbukumbu la Torati 25:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Jicho lenu halipaswi.”

Kumbukumbu la Torati 25:13

Marejeo

  • +Met 11:1; 20:10; Mik 6:11

Kumbukumbu la Torati 25:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “efa na efa.” Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +Law 19:36

Kumbukumbu la Torati 25:15

Marejeo

  • +Kum 4:40

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    8/2022, uku. 27

Kumbukumbu la Torati 25:16

Marejeo

  • +Law 19:35

Kumbukumbu la Torati 25:17

Marejeo

  • +Kut 17:8; Hes 24:20

Kumbukumbu la Torati 25:19

Marejeo

  • +Yos 22:4
  • +Kut 17:14; 1Sa 14:47, 48; 15:1-3; 1Nya 4:42, 43

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Igeni, uku. 144

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/2012, uku. 29

  • Fahirishi ya Machapisho

    w12 1/1 29

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 25:1Kum 16:18; 17:8, 9; 19:16, 17
Kum. 25:1Kut 23:6; 2Nya 19:6; Met 17:15; 31:9
Kum. 25:2Met 10:13; 20:30; 26:3; Lu 12:48; Ebr 2:2
Kum. 25:32Ko 11:24
Kum. 25:4Met 12:10; 1Ko 9:9; 1Ti 5:18
Kum. 25:5Mwa 38:7, 8; Ru 4:5; Mk 12:19
Kum. 25:6Mwa 38:9; Ru 4:10, 17
Kum. 25:6Hes 27:1, 4
Kum. 25:9Ru 4:7
Kum. 25:13Met 11:1; 20:10; Mik 6:11
Kum. 25:14Law 19:36
Kum. 25:15Kum 4:40
Kum. 25:16Law 19:35
Kum. 25:17Kut 17:8; Hes 24:20
Kum. 25:19Yos 22:4
Kum. 25:19Kut 17:14; 1Sa 14:47, 48; 15:1-3; 1Nya 4:42, 43
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 25:1-19

Kumbukumbu la Torati

25 “Watu wakizozana, wanaweza kwenda kuwaona waamuzi,+ nao wataamua kesi yao na kumtangaza mtu asiye na hatia kuwa mwadilifu na aliye na hatia kuwa mwovu.+ 2 Ikiwa mtu mwovu anastahili kupigwa viboko,+ mwamuzi atamwagiza alale chini kifudifudi, na mtu huyo atapigwa viboko mbele yake. Idadi ya viboko inapaswa kulingana na uovu aliotenda. 3 Anaweza kumpiga kufikia viboko 40,+ lakini asizidishe. Akiendelea kumpiga viboko zaidi, ndugu yenu ataaibika machoni penu.

4 “Hupaswi kumfunga kinywa ng’ombe dume anapopura nafaka.+

5 “Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao afe bila mwana, mke wa yule aliyekufa hapaswi kuolewa na mwanamume mwingine nje ya ukoo huo. Ndugu ya mume wake anapaswa kwenda kwake, amchukue awe mke wake, na kufunga naye ndoa ya ndugu mkwe.+ 6 Mtoto wa kwanza atakayemzaa ataendeleza jina la ndugu yake aliyekufa,+ ili jina lake lisifutiliwe mbali kutoka Israeli.+

7 “Sasa ikiwa mwanamume huyo hataki kumwoa mjane wa ndugu yake, mjane huyo anapaswa kwenda kwa wazee kwenye lango la jiji na kuwaambia, ‘Ndugu ya mume wangu amekataa kuhifadhi jina la ndugu yake katika Israeli. Amekataa kufunga nami ndoa ya ndugu mkwe.’ 8 Ni lazima wazee wa jiji lake wamwite na kuzungumza naye. Ikiwa atasisitiza hivi: ‘Sitaki kumwoa,’ 9 basi mjane wa ndugu yake atamkaribia mbele ya wazee, atamvua mwanamume huyo kiatu,+ kisha amtemee mate usoni na kusema, ‘Hivyo ndivyo anavyopaswa kutendewa mwanamume ambaye hatajenga familia ya ndugu yake.’ 10 Kisha, jina la familia* yake katika Israeli litakuwa ‘Familia* ya mtu aliyevuliwa kiatu.’

11 “Wanaume wawili wakipigana na mke wa mmoja wao aingilie kati ili kumlinda mume wake asipigwe, naye aunyooshe mkono wake na kumkamata sehemu za siri mwanamume anayepigana na mume wake, 12 ni lazima mumkate mkono mwanamke huyo. Hampaswi* kumhurumia.

13 “Hupaswi kuwa na aina mbili za mawe ya mizani katika mfuko wako,+ jiwe kubwa na dogo. 14 Hupaswi kuwa na aina mbili za vyombo vya kupimia*+ nyumbani mwako, kikubwa na kidogo. 15 Unapaswa kuwa na mawe ya kupimia yaliyo sahihi na ya haki na kipimo kilicho sahihi na cha haki, ili uendelee kuishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa.+ 16 Kwa maana kila mtu asiyetenda haki ambaye anafanya mambo hayo ni chukizo kwa Yehova Mungu wenu.+

17 “Kumbukeni yale ambayo Waamaleki waliwatendea mlipokuwa njiani kutoka Misri,+ 18 jinsi walivyokutana nanyi njiani na kuwashambulia wale wote waliokuwa wakijikokota nyuma mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu. Hawakumwogopa Mungu. 19 Yehova Mungu wenu atakapokuwa amewapumzisha kutokana na maadui wenu wote wanaowazunguka katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa kuwa urithi ili mwimiliki,+ mnapaswa kuwaangamiza kabisa Waamaleki ili wasikumbukwe tena chini ya mbingu.+ Msisahau jambo hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki