Matendo
17 Sasa wakasafiri kupitia Amfipolisi na Apolonia wakaja hadi Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. 2 Basi kulingana na desturi ya Paulo aliingia ndani walimo, na kwa sabato tatu akajadiliana nao kwa kutoa sababu kutokana na Maandiko, 3 akieleza na kuthibitisha kwa marejezo kwamba ilikuwa lazima Kristo kuteseka na kufufuliwa kutoka kwa wafu, akisema: “Huyu ndiye Kristo, Yesu huyu ninayewatangazia nyinyi.” 4 Tokeo ni kwamba baadhi yao wakawa waamini na kujishirikisha wenyewe na Paulo na Sila, na umati mkubwa kati ya Wagiriki waliomwabudu Mungu na si wachache kati ya wanawake walio wakubwa wakafanya hivyo.
5 Lakini Wayahudi, wakipata kuwa na wivu, wakashirikiana na wanaume fulani waovu kati ya wazururaji wa mahali pa soko na kufanyiza kikundi chenye ghasia ili kulitupa jiji katika ghasia. Nao wakaishambulia nyumba ya Yasoni na kuanza kujaribu sana kuwaleta mbele kwenye watu wenye kufanya ghasia. 6 Wakati hawakuwapata walikokota Yasoni na akina ndugu fulani kuwapeleka kwa watawala wa jiji, wakipaaza kilio hivi: “Watu hawa ambao wameipindua dunia inayokaliwa wapo hapa pia, 7 na Yasoni amewapokea kwa ukaribishaji-wageni. Na watu wote hawa watenda katika upinzani na maagizo ya Kaisari, wakisema kuna mfalme mwingine, Yesu.” 8 Kwa kweli walifadhaisha huo umati na watawala wa jiji waliposikia mambo haya; 9 na kwanza baada ya kuchukua dhamana ya kutosha kutoka kwa Yasoni na wale wengine wakawaacha waende.
10 Mara hiyo wakati wa usiku akina ndugu wakatuma Paulo na Sila pia hadi Berea, na hawa, walipowasili, wakaenda ndani ya sinagogi la Wayahudi. 11 Sasa hawa wa mwisho walikuwa wenye akili ya uelekevu bora zaidi kuliko wale katika Thesalonike, kwa maana walilipokea neno kwa hamu ya akili iliyo kubwa zaidi sana, wakiyachunguza Maandiko kwa uangalifu kila siku juu ya kama mambo hayo yalikuwa hivyo. 12 Kwa hiyo wengi kati yao wakawa waamini, na pia wakafanya hivyo si wachache kati ya wanawake Wagiriki na kati ya wanaume wenye kusifika. 13 Lakini Wayahudi kutoka Thesalonike walipopata habari kwamba neno la Mungu lilitangazwa na Paulo katika Berea pia, wakaja huko pia ili kuchochea na kufadhaisha yale matungamano ya watu. 14 Ndipo akina ndugu mara hiyo wakamsindikiza Paulo hadi baharini; lakini Sila na Timotheo pia wakabaki nyuma huko. 15 Hata hivyo, wale wenye kumwongoza Paulo wakamleta hadi Athene na, baada ya kupokea amri kwamba Sila na Timotheo wamjie upesi iwezekanavyo, wakaondoka.
16 Basi Paulo alipokuwa akiwangojea katika Athene, roho yake ikawa yenye kuudhika ndani yake kwa kuona kwamba hilo jiji lilijaa sanamu. 17 Kwa sababu hiyo akaanza kujadiliana kwa kutoa sababu katika sinagogi pamoja na Wayahudi na watu wengine waliomwabudu Mungu na kila siku mahali pa soko pamoja na wale waliotukia kuwa hapo. 18 Lakini watu fulani wa Waepikurea na wanafalsafa Wastoa pia wakawa wanaongea naye kwa mabishano, na baadhi yao walikuwa wakisema: “Ni nini ambalo mpiga-domo huyu angependa kusimulia?” Wengine: “Aonekana kuwa mtangazaji wa miungu migeni.” Hiyo ilikuwa kwa sababu alikuwa akitangaza habari njema ya Yesu na ufufuo. 19 Kwa hiyo wakamshika na kumwongoza kwenye Areopago, wakisema: “Je, twaweza kupata kujua fundisho hili jipya ni nini lisemwalo na wewe? 20 Kwa maana unaanzisha mambo fulani yaliyo mageni masikioni mwetu. Kwa hiyo twataka kupata kujua mambo haya yamaanisha nini.” 21 Kwa kweli, Waathene wote na watoka-ugenini wenye kukaa kwa muda hapo walikuwa wakitumia wasaa wao bila kufanya kitu chochote ila kuambiana kitu fulani au kusikiliza kitu fulani kipya. 22 Basi Paulo akasimama katikati ya Areopago na kusema:
“Wanaume wa Athene, naona kwamba katika mambo yote mwaonekana kuwa wenye mwelekeo zaidi wa kuhofu miungu kuliko wengine walivyo. 23 Kwa mfano, nilipokuwa nikipita njiani na kutazama kwa uangalifu vitu vyenu vya kupewa heshima inayozidi nilikuta pia madhabahu ambayo juu yayo ilikuwa imeandikwa ‘Kwa Mungu Asiyejulikana.’ Kwa hiyo kile mnachokipa ujitoaji-kimungu bila kujua, hicho ninawatangazia nyinyi. 24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyo katika huo, akiwa, kama Huyu alivyo, Bwana wa mbingu na dunia, hakai katika mahekalu yaliyofanywa kwa mikono, 25 wala yeye hahudumiwi kwa mikono ya kibinadamu kama kwamba yeye ahitaji kitu chochote, kwa sababu yeye mwenyewe huwapa watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. 26 Naye alifanya kutoka kwa mtu mmoja kila taifa la watu, ili wakae juu ya uso mzima wa dunia, naye aliagiza nyakati zilizowekwa na mipaka iliyowekwa ya makao ya watu, 27 ili wao wamtafute Mungu, ikiwa wangeweza kupapasa-papasa wakimtafuta na kwa kweli wampate, ijapokuwa, kweli, yeye hayuko mbali sana na kila mmoja wetu. 28 Kwa maana kwa njia yake tuna uhai na twaenda na kuwako, hata kama vile watu fulani kati ya washairi miongoni mwenu wamesema: ‘Kwa maana sisi pia ni uzao wake.’
29 “Kwa hiyo, kwa kuwa sisi ni uzao wa Mungu, hatupaswi kuwazia kwamba Mungu ni kama dhahabu au fedha au jiwe, kama kitu kilichochongwa kwa usanifu na mtungo wa binadamu. 30 Ni kweli, Mungu ameachilia nyakati za kutokuwa na ujuzi kwa namna hiyo, lakini sasa anaambia wanadamu kwamba wapaswa wote kila mahali kutubu. 31 Kwa sababu ameweka siku ambayo katika hiyo akusudia kuihukumu kwa uadilifu dunia inayokaliwa kwa njia ya mwanamume ambaye ameweka rasmi, naye ametoa uhakikisho kamili kwa watu wote kwa kuwa amemfufua kutoka kwa wafu.”
32 Basi, waliposikia juu ya ufufuo wa wafu, wengine wao wakaanza kudhihaki, huku wengine wakisema: “Hakika tutakusikiliza tena juu ya hili wakati mwingine.” 33 Hivyo Paulo akaenda kutoka katikati yao, 34 lakini wanaume fulani wakajiunga naye na kuwa waamini, miongoni mwao pia wakiwamo Dionisio, hakimu wa mahakama ya Areopago, na mwanamke mmoja aitwaye jina Damarisi, na wengine mbali na hao.