1 Samweli
27 Hata hivyo, Daudi akasema moyoni mwake: “Sasa mkono wa Sauli utanifagilia mbali siku moja. Hakuna jambo bora kwangu kuliko kuponyoka+ bila shaka, niende katika nchi ya Wafilisti;+ na Sauli atakata tamaa ya kunitafuta tena katika eneo lote la Israeli,+ nami nitaponyoka kutoka mkononi mwake.” 2 Basi Daudi akaondoka, yeye pamoja na watu mia sita+ waliokuwa pamoja naye, akavuka kwenda kwa Akishi+ mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi. 3 Na Daudi akaendelea kukaa na Akishi katika Gathi, yeye pamoja na watu wake, kila mmoja na nyumba yake,+ Daudi na wake zake wawili, Ahinoamu+ Myezreeli na Abigaili,+ mke wa Nabali Mkarmeli. 4 Baada ya muda Sauli akapelekewa habari kwamba Daudi alikuwa amekimbia kwenda Gathi, kwa hiyo hakwenda kumtafuta tena.+
5 Ndipo Daudi akamwambia Akishi: “Ikiwa sasa nimepata kibali machoni pako, na wanipe mahali katika moja la majiji ya mashambani, ili nikae huko; kwa nini mtumishi wako akae katika jiji la kifalme pamoja nawe?” 6 Basi Akishi akampa Siklagi+ siku hiyo. Ndiyo sababu Siklagi limekuwa la wafalme wa Yuda mpaka leo hii.
7 Na hesabu ya siku ambazo Daudi alikaa katika nchi ya mashambani ya Wafilisti ikawa mwaka mmoja na miezi minne.+ 8 Na Daudi akapanda pamoja na watu wake ili wavamie Wageshuri+ na Wagirzi na Waamaleki;+ kwa maana walikuwa wakikaa katika nchi iliyoanzia Telamu+ mpaka Shuri+ na kushuka mpaka nchi ya Misri. 9 Naye Daudi akaipiga nchi, lakini hakuhifadhi hai mwanamume wala mwanamke;+ naye akachukua makundi na mifugo na punda na ngamia na mavazi, kisha akarudi, akaja kwa Akishi. 10 Ndipo Akishi akasema: “Mlivamia wapi leo?” Naye Daudi akasema:+ “Upande wa kusini wa Yuda+ na upande wa kusini wa Wayerahmeeli+ na upande wa kusini wa Wakeni.”+ 11 Na kuhusu mwanamume na mwanamke, Daudi hakuhifadhi hai yeyote ili kuwaleta Gathi, akisema: “Wasije wakatusema kwa maneno haya, ‘Hivi ndivyo Daudi alivyofanya.’”+ (Na hii imekuwa kawaida yake siku zote ambazo aliishi katika nchi ya mashambani ya Wafilisti.) 12 Kwa hiyo Akishi akamwamini+ Daudi, akisema moyoni mwake: “Bila shaka amenuka katikati ya watu wake Israeli;+ naye atakuwa mtumishi wangu mpaka wakati usio na kipimo.”