Ayubu
39 “Je, umepata kujua wakati uliowekwa wa mbuzi wa milimani kuzaa?+
Je, unaangalia wakati ule paa wanapozaa+ kwa uchungu?
2 Je, wewe huhesabu miezi ambayo wao hutimiza,
Au, je, umepata kujua wakati uliowekwa ambapo wao huzaa?
3 Wao huinama wanapotoa watoto wao,
Wanapoondoa uchungu wao.
4 Wana wao huwa wenye nguvu, huwa wakubwa porini;
Kwa kweli wao huenda zao wala hawarudi kwao.
5 Ni nani aliyemwachilia punda-milia+ awe huru,
Na ni nani aliyevifungua vifungo vya punda-mwitu,
6 Ambao nimeweka nchi tambarare ya jangwa kuwa nyumba yao
Na ambao makao yao ni nchi ya chumvi?+
10 Je, utamfunga imara ng’ombe-mwitu kwa kamba zake katika mtaro,
Au, je, yeye atalima+ nchi tambarare za chini nyuma yako?
11 Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingi,
Na, je, utamwachia yeye kazi yako ngumu?
12 Je, utamtegemea kwamba atarudisha mbegu zako
Na kwamba atakusanya kwenye uwanja wako wa kupuria?
14 Kwa maana yeye huyaacha mayai yake katika nchi
Naye huyatia joto katika mavumbi,
15 Naye husahau kwamba mguu fulani unaweza kuyavunja
Au hata mnyama wa mwituni anaweza kuyakanyaga.
16 Yeye huwatendea wanawe kwa ukali, kana kwamba si wake+—
Kazi yake ngumu ni ya ubatili kwa sababu yeye hana hofu.
18 Wakati anapopiga-piga mabawa yake juu,
Yeye humcheka farasi na mpandaji wake.
21 Yeye huparapara+ katika nchi tambarare ya chini na kufurahia nguvu;
Husonga mbele kukutana na silaha.+
23 Podo hupiga kelele juu yake,
Kichwa cha mkuki na pia fumo.
24 Yeye huimeza nchi kwa mwendo wa kishindo na msisimuko,
Wala haamini kwamba ni sauti ya baragumu.
25 Mara tu baragumu inapopiga yeye husema Aha!
Naye hunusa harufu ya pigano kutoka mbali sana,
Mshindo wa wakuu na kelele za vita.+
26 Je, ni kwa sababu ya uelewaji wako kwamba kipanga hupaa juu,
Kwamba yeye hunyoosha mabawa yake kuuelekea upepo wa kusini?
27 Au, je, ni kwa agizo lako kwamba tai+ huruka kuelekea juu
Na kwamba hujenga kiota chake huko juu,+
28 Kwamba yeye hukaa kwenye mwamba na wakati wa usiku hukaa
Juu ya ncha ya mwamba na mahali pasipoweza kufikiwa?