1 Wakorintho
10 Sasa sitaki nyinyi mwe wasio na ujuzi, akina ndugu, kwamba baba zetu wa zamani walikuwa wote chini ya wingu na wote walipita katika bahari 2 na wote walibatizwa katika Musa kupitia wingu na bahari; 3 na wote walikula chakula cha kiroho kilekile 4 na wote walikunywa kinywaji cha kiroho kilekile. Kwa maana walikuwa na kawaida ya kunywa kutoka katika tungamo-mwamba la kiroho lililowafuata, na tungamo-mwamba hilo lilimaanisha Kristo. 5 Hata hivyo, juu ya walio wengi zaidi kati yao Mungu hakuonyesha kibali chake, kwa maana waliangamizwa nyikani.
6 Basi mambo hayo yalipata kuwa vielelezo vyetu sisi, ili tusiwe watu wanaotamani mambo mabaya, kama vile wao walivyoyatamani. 7 Wala tusiwe waabudu-sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa; kama vile imeandikwa: “Watu waliketi kula na kunywa, nao wakainuka wapate kujitumbuiza.” 8 Wala tusiwe tukifanya uasherati, kama vile baadhi yao walivyofanya uasherati, ila kuanguka, ishirini na tatu elfu kati yao katika siku moja. 9 Wala tusimtie Yehova kwenye jaribu, kama vile baadhi yao walivyomtia yeye kwenye jaribu, ila kuangamia kutokana na wale nyoka. 10 Wala tusiwe wanung’unikaji, kama vile baadhi yao walivyonung’unika, ila kuangamia kutokana na mwangamizi. 11 Basi mambo hayo yaliendelea kuwapata kuwa vielelezo, nayo yaliandikwa kuwa onyo kwetu sisi ambao juu yetu miisho ya mifumo ya mambo imewasili.
12 Kwa sababu hiyo acheni yeye ambaye afikiri kuwa amesimama ajihadhari kwamba asianguke. 13 Hakuna kishawishi ambacho kimewapata nyinyi ila kilicho kawaida kwa watu. Lakini Mungu ni mwaminifu, naye hatawaacha nyinyi mshawishwe kupita vile mwezavyo kuhimili, bali pamoja na hicho kishawishi ataifanya pia njia ya kutokea kusudi mweze kuvumilia hilo.
14 Kwa hiyo, wapendwa wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama kwamba ni kwa watu wenye ufahamu; hukumuni nyinyi wenyewe lile nisemalo. 16 Kikombe cha baraka ambacho sisi twabariki, je, hicho si ushirika katika damu ya Kristo? Ule mkate ambao sisi twamega, je, huo si ushirika katika mwili wa Kristo? 17 Kwa sababu kuna mkate mmoja, sisi, tujapokuwa wengi, tuko mwili mmoja, kwa maana sisi sote tunashiriki mkate mmoja huo.
18 Tazameni kile ambacho ni Israeli kwa njia ya kimwili: Je, wale wazilao dhabihu si washiriki pamoja na madhabahu? 19 Basi, niseme nini? Kwamba kile ambacho kimefanywa dhabihu kwa sanamu ni kitu, au kwamba sanamu ni kitu? 20 La; bali nasema kwamba vitu ambavyo mataifa huvidhabihu huwa wavidhabihu kwa roho waovu, na si kwa Mungu; nami sitaki nyinyi mwe washiriki pamoja na roho waovu. 21 Hamwezi kuwa mkinywa kikombe cha Yehova na kikombe cha roho waovu; hamwezi kuwa mkishiriki “meza ya Yehova” na meza ya roho waovu. 22 Au je, “tunamchochea Yehova kwenye wivu”? Sisi hatuna nguvu zaidi kuliko yeye, ndivyo?
23 Mambo yote yaruhusika kisheria; lakini si mambo yote yenye faida. Mambo yote yaruhusika kisheria; lakini si mambo yote yajengayo. 24 Acheni kila mmoja afulize kutafuta sana, si faida yake mwenyewe, bali ya mtu yule mwingine.
25 Kila kitu kiuzwacho katika soko la nyama fulizeni kukila, bila kuulizia habari kwa sababu ya dhamiri yenu; 26 kwa maana “ni ya Yehova dunia na kile chenye kuijaa.” 27 Ikiwa yeyote wa wasio waamini awaalika nanyi mwataka kwenda, endeleeni kula kila kitu kiwekwacho mbele yenu, bila kuulizia habari kwa sababu ya dhamiri yenu. 28 Lakini yeyote akiwaambia nyinyi: “Hiki ni kitu kilichotolewa dhabihu,” msile kwa sababu ya yule aliyefunua hilo na kwa sababu ya dhamiri. 29 “Dhamiri,” nasema, si yako mwenyewe, bali ile ya mtu yule mwingine. Kwa maana kwa nini iwe kwamba uhuru wangu wahukumiwa na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Ikiwa nashiriki nikiwa na shukrani, kwa nini nisemwe kwa maneno yenye kuudhi juu ya kile nitoleacho shukrani?
31 Kwa hiyo, kama mnakula au mnakunywa au mnafanya jambo jingine lolote, fanyeni mambo yote kwa utukufu wa Mungu. 32 Epukeni kuwa sababu za kukwaza Wayahudi vilevile Wagiriki na kutaniko la Mungu, 33 kama vile mimi ninavyopendeza watu wote katika mambo yote, bila kutafuta sana faida yangu mwenyewe bali ile ya walio wengi, ili wapate kuokolewa.