Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 22
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Kuheshimu wanyama wa jirani (1-4)

      • Kuvaa nguo za watu wa jinsia tofauti (5)

      • Kuwatendea wanyama kwa fadhili (6, 7)

      • Ukuta unaozunguka ukingo wa paa (8)

      • Michanganyiko isiyofaa (9-11)

      • Vishada vya nguo (12)

      • Sheria kuhusu kukiuka maadili ya ngono (13-30)

Kumbukumbu la Torati 22:1

Marejeo

  • +Kut 23:4

Kumbukumbu la Torati 22:2

Marejeo

  • +Mt 7:12

Kumbukumbu la Torati 22:4

Marejeo

  • +Kut 23:5; Law 19:18; Lu 10:27; Gal 6:10

Kumbukumbu la Torati 22:5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Furahia Maisha Milele!, somo la 52

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    9/2016, uku. 18

Kumbukumbu la Torati 22:6

Marejeo

  • +Law 22:28; Zb 145:9; Met 12:10; Mt 10:29

Kumbukumbu la Torati 22:8

Marejeo

  • +2Sa 11:2; Mdo 10:9

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 346

    Mnara wa Mlinzi,

    4/1/2013, uku. 10

    2/1/2001, kur. 4-5

  • Fahirishi ya Machapisho

    w01 2/1 4-5

Kumbukumbu la Torati 22:9

Marejeo

  • +Law 19:19

Kumbukumbu la Torati 22:10

Marejeo

  • +Met 12:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 649

    Mnara wa Mlinzi,

    10/15/2003, uku. 32

    11/15/1995, uku. 31

  • Fahirishi ya Machapisho

    w03 10/15 32

Kumbukumbu la Torati 22:11

Marejeo

  • +Law 19:19

Kumbukumbu la Torati 22:12

Marejeo

  • +Hes 15:38; Mt 23:2, 5

Kumbukumbu la Torati 22:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “amkatae.”

Kumbukumbu la Torati 22:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “anamkataa.”

Kumbukumbu la Torati 22:18

Marejeo

  • +Kut 18:21; Kum 1:13; 16:18
  • +Kum 25:2; Met 10:13; 19:29

Kumbukumbu la Torati 22:19

Marejeo

  • +Mal 2:16

Kumbukumbu la Torati 22:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “ukahaba.”

Marejeo

  • +Ebr 13:4
  • +Law 21:9
  • +Law 11:45; 1Ko 5:13

Kumbukumbu la Torati 22:22

Marejeo

  • +Mwa 20:3; Kut 20:14; Law 20:10; 1Ko 6:9, 10, 18

Kumbukumbu la Torati 22:24

Marejeo

  • +Law 20:10; Kum 5:18; 1Th 4:3, 6; Ebr 13:4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    12/2019, uku. 14

Kumbukumbu la Torati 22:25

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    12/2019, uku. 14

Kumbukumbu la Torati 22:26

Marejeo

  • +Mwa 4:8; Hes 35:20, 21; Yak 2:11

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    12/2019, uku. 14

Kumbukumbu la Torati 22:27

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    12/2019, uku. 14

Kumbukumbu la Torati 22:28

Marejeo

  • +Mwa 34:2, 5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/1989, uku. 31

Kumbukumbu la Torati 22:29

Marejeo

  • +Mwa 34:11, 12; Kut 22:16

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/1989, uku. 31

Kumbukumbu la Torati 22:30

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kumchukua.”

  • *

    Tnn., “asimfunue nguo baba yake.”

Marejeo

  • +Law 18:8; 20:11; Kum 27:20; 1Ko 5:1

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 22:1Kut 23:4
Kum. 22:2Mt 7:12
Kum. 22:4Kut 23:5; Law 19:18; Lu 10:27; Gal 6:10
Kum. 22:6Law 22:28; Zb 145:9; Met 12:10; Mt 10:29
Kum. 22:82Sa 11:2; Mdo 10:9
Kum. 22:9Law 19:19
Kum. 22:10Met 12:10
Kum. 22:11Law 19:19
Kum. 22:12Hes 15:38; Mt 23:2, 5
Kum. 22:18Kut 18:21; Kum 1:13; 16:18
Kum. 22:18Kum 25:2; Met 10:13; 19:29
Kum. 22:19Mal 2:16
Kum. 22:21Ebr 13:4
Kum. 22:21Law 21:9
Kum. 22:21Law 11:45; 1Ko 5:13
Kum. 22:22Mwa 20:3; Kut 20:14; Law 20:10; 1Ko 6:9, 10, 18
Kum. 22:24Law 20:10; Kum 5:18; 1Th 4:3, 6; Ebr 13:4
Kum. 22:26Mwa 4:8; Hes 35:20, 21; Yak 2:11
Kum. 22:28Mwa 34:2, 5
Kum. 22:29Mwa 34:11, 12; Kut 22:16
Kum. 22:30Law 18:8; 20:11; Kum 27:20; 1Ko 5:1
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 22:1-30

Kumbukumbu la Torati

22 “Ukimwona ng’ombe dume wa ndugu yako au kondoo wake akipotea njia, usimpuuze kimakusudi.+ Unapaswa kumrudisha kwa ndugu yako. 2 Lakini ikiwa huyo ndugu yako haishi karibu nawe au humjui, unapaswa kumpeleka mnyama huyo nyumbani kwako, naye atakaa nawe mpaka ndugu yako atakapokuja kumtafuta. Kisha utamrudishia mnyama huyo.+ 3 Unapaswa kufanya vivyo hivyo kuhusu punda wake, nguo zake, na kitu chochote utakachopata kilichopotezwa na ndugu yako. Hupaswi kukipuuza.

4 “Ukimwona punda wa ndugu yako au ng’ombe dume wake akianguka barabarani hupaswi kumpuuza kimakusudi. Unapaswa kumsaidia kumwinua mnyama huyo.+

5 “Mwanamke hapaswi kuvaa nguo za mwanamume, na mwanamume hapaswi kuvaa nguo za mwanamke. Kwa maana mtu yeyote anayefanya hivyo ni chukizo kwa Yehova Mungu wenu.

6 “Ukipata njiani kiota cha ndege chenye makinda au mayai, iwe mtini au kwenye ardhi, naye mama amefunika makinda au kuatamia mayai, usimchukue mama pamoja na makinda yake.+ 7 Hakikisha umemfukuza mama yao, lakini unaweza kuchukua makinda. Fanya hivyo ili mambo yakuendee vyema na uishi muda mrefu.

8 “Ukijenga nyumba mpya, ni lazima pia ujenge ukuta kuzunguka ukingo wa paa lako,+ ili mtu asianguke kutoka kwenye paa nawe uiletee familia yako hatia ya damu.

9 “Usipande aina mbili za mbegu katika shamba lako la mizabibu.+ La sivyo, mazao yote utakayopata kutokana na mbegu hizo na pia zabibu zitakuwa za mahali patakatifu.

10 “Usilime kwa ng’ombe dume na punda pamoja.+

11 “Usivae nguo zilizotengenezwa kwa kuchanganya sufu na kitani.+

12 “Unapaswa kutengeneza vishada kwenye pembe nne za nguo unazovaa.+

13 “Mwanamume akimchukua mke na kufanya ngono naye lakini baadaye amchukie* 14 na kudai kwamba ana mwenendo mbaya na kumharibia sifa kwa kusema, ‘Nilimchukua mwanamke huyu, lakini nilipofanya ngono naye sikupata uthibitisho wa kwamba yeye ni bikira,’ 15 baba na mama ya msichana huyo wanapaswa kuwapelekea wazee walio kwenye lango la jiji uthibitisho wa kwamba msichana huyo alikuwa bikira. 16 Baba ya msichana huyo atawaambia hivi wazee hao: ‘Nilimpa mwanamume huyu binti yangu awe mke wake, lakini anamchukia* 17 na anadai kwamba ana mwenendo mbaya kwa kusema, “Nimegundua kwamba binti yenu si bikira.” Sasa huu ndio uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.’ Kisha watatandaza nguo hiyo mbele ya wazee wa jiji. 18 Wazee wa jiji+ watamchukua mwanamume huyo na kumtia nidhamu.+ 19 Watamtoza shekeli 100 za fedha na kumpa baba ya msichana huyo, kwa sababu mtu huyo alimharibia sifa bikira wa Israeli,+ naye ataendelea kuwa mke wake. Maadamu mwanamume huyo anaishi, hataruhusiwa kumtaliki msichana huyo.

20 “Hata hivyo, ikiwa madai hayo ni ya kweli na hakuna uthibitisho kwamba msichana huyo alikuwa bikira, 21 wanapaswa kumpeleka msichana huyo kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na wanaume wa jiji watamuua kwa kumpiga mawe, kwa sababu ametenda jambo la aibu+ katika Israeli kwa kufanya uasherati* katika nyumba ya baba yake.+ Kwa hiyo ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.+

22 “Mwanamume akipatikana akifanya ngono na mke wa mwanamume mwingine, ni lazima wote wawili wauawe pamoja, mwanamume huyo pamoja na mwanamke aliyefanya naye ngono.+ Kwa hiyo ni lazima mwondoe uovu katika Israeli.

23 “Ikiwa bikira amechumbiwa na mwanamume, kisha mwanamume mwingine akutane naye jijini na kufanya naye ngono, 24 mnapaswa kuwaleta wote wawili kwenye lango la jiji na kuwaua kwa kuwapiga mawe, mtamuua msichana huyo kwa sababu hakupiga mayowe jijini na mwanamume huyo kwa sababu alimwaibisha mke wa mwanamume mwenzake.+ Kwa hiyo ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

25 “Hata hivyo, ikiwa mwanamume huyo alimkuta uwanjani msichana huyo aliyechumbiwa na kumkamata kwa nguvu na kufanya naye ngono, mwanamume huyo aliyelala naye atauawa peke yake, 26 lakini msimtendee lolote msichana huyo. Msichana huyo hajatenda dhambi inayostahili kifo. Kisa chake ni sawa na cha mtu anayemshambulia mwenzake na kumuua.+ 27 Kwa maana mwanamume huyo alimkuta uwanjani, na msichana huyo aliyechumbiwa akapiga mayowe, lakini hakukuwa na mtu wa kumwokoa.

28 “Mwanamume akikutana na bikira ambaye hajachumbiwa kisha amkamate kwa nguvu na kufanya naye ngono, nao wagunduliwe,+ 29 mwanamume aliyefanya ngono na msichana huyo anapaswa kumpa baba ya msichana huyo shekeli 50 za fedha, naye atakuwa mke wake.+ Kwa sababu mwanamume huyo alimwaibisha, hataruhusiwa kumtaliki msichana huyo maisha yake yote.

30 “Hakuna mwanamume anayepaswa kumwoa* mke wa baba yake, ili asimwaibishe baba yake.*+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki