Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 3
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Wamshinda Mfalme Ogu wa Bashani (1-7)

      • Kugawanywa kwa nchi upande wa mashariki wa Yordani (8-20)

      • Yoshua aambiwa asiogope (21, 22)

      • Musa hataingia katika nchi hiyo (23-29)

Kumbukumbu la Torati 3:1

Marejeo

  • +Hes 21:33-35

Kumbukumbu la Torati 3:4

Marejeo

  • +Hes 32:33; Kum 29:7, 8; Yos 13:29, 30

Kumbukumbu la Torati 3:6

Marejeo

  • +Law 27:29
  • +Law 18:25

Kumbukumbu la Torati 3:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Korongo.”

Marejeo

  • +Hes 32:33
  • +Yos 12:1, 2

Kumbukumbu la Torati 3:10

Marejeo

  • +Hes 21:33

Kumbukumbu la Torati 3:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “jiwe jeusi la volkano.”

  • *

    Mkono mmoja ulilingana na sentimita 44.5 (inchi 17.5). Angalia Nyongeza B14.

Kumbukumbu la Torati 3:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Korongo.”

Marejeo

  • +Hes 32:34
  • +Hes 32:33

Kumbukumbu la Torati 3:13

Marejeo

  • +Hes 32:39; Yos 13:29-31; 1Nya 5:23

Kumbukumbu la Torati 3:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Maana yake “Vijiji vya Mahema vya Yairi.”

Marejeo

  • +1Nya 2:22
  • +Kum 3:4
  • +Yos 13:13
  • +Hes 32:40, 41

Kumbukumbu la Torati 3:15

Marejeo

  • +Hes 32:39; Yos 17:1

Kumbukumbu la Torati 3:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Korongo.”

Marejeo

  • +Hes 32:33; Yos 22:9

Kumbukumbu la Torati 3:17

Marejeo

  • +Hes 34:11, 12

Kumbukumbu la Torati 3:18

Marejeo

  • +Hes 32:20-22

Kumbukumbu la Torati 3:20

Marejeo

  • +Yos 1:14, 15; 22:4, 8

Kumbukumbu la Torati 3:21

Marejeo

  • +Hes 11:28; 14:30; 27:18
  • +Yos 10:25

Kumbukumbu la Torati 3:22

Marejeo

  • +Kut 14:14; 15:3; Kum 1:30; 20:4; Yos 10:42

Kumbukumbu la Torati 3:24

Marejeo

  • +Kut 15:16; Kum 11:2
  • +Kut 15:11; 2Sa 7:22; 1Fa 8:23; Zb 86:8; Yer 10:6, 7

Kumbukumbu la Torati 3:25

Marejeo

  • +Kut 3:8; Kum 1:7; 11:11, 12

Kumbukumbu la Torati 3:26

Marejeo

  • +Hes 20:12; 27:13, 14; Kum 4:21; Zb 106:32

Kumbukumbu la Torati 3:27

Marejeo

  • +Hes 27:12
  • +Kum 34:1, 4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha, 2/2020, uku. 1

Kumbukumbu la Torati 3:28

Marejeo

  • +Hes 27:18-20; Kum 1:38; 31:7
  • +Yos 1:1, 2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha, 2/2020, uku. 1

Kumbukumbu la Torati 3:29

Marejeo

  • +Kum 4:45, 46; 34:5, 6

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 3:1Hes 21:33-35
Kum. 3:4Hes 32:33; Kum 29:7, 8; Yos 13:29, 30
Kum. 3:6Law 27:29
Kum. 3:6Law 18:25
Kum. 3:8Hes 32:33
Kum. 3:8Yos 12:1, 2
Kum. 3:10Hes 21:33
Kum. 3:12Hes 32:34
Kum. 3:12Hes 32:33
Kum. 3:13Hes 32:39; Yos 13:29-31; 1Nya 5:23
Kum. 3:141Nya 2:22
Kum. 3:14Kum 3:4
Kum. 3:14Yos 13:13
Kum. 3:14Hes 32:40, 41
Kum. 3:15Hes 32:39; Yos 17:1
Kum. 3:16Hes 32:33; Yos 22:9
Kum. 3:17Hes 34:11, 12
Kum. 3:18Hes 32:20-22
Kum. 3:20Yos 1:14, 15; 22:4, 8
Kum. 3:21Hes 11:28; 14:30; 27:18
Kum. 3:21Yos 10:25
Kum. 3:22Kut 14:14; 15:3; Kum 1:30; 20:4; Yos 10:42
Kum. 3:24Kut 15:16; Kum 11:2
Kum. 3:24Kut 15:11; 2Sa 7:22; 1Fa 8:23; Zb 86:8; Yer 10:6, 7
Kum. 3:25Kut 3:8; Kum 1:7; 11:11, 12
Kum. 3:26Hes 20:12; 27:13, 14; Kum 4:21; Zb 106:32
Kum. 3:27Hes 27:12
Kum. 3:27Kum 34:1, 4
Kum. 3:28Hes 27:18-20; Kum 1:38; 31:7
Kum. 3:28Yos 1:1, 2
Kum. 3:29Kum 4:45, 46; 34:5, 6
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 3:1-29

Kumbukumbu la Torati

3 “Kisha tuligeuka na kupanda kupitia njia ya Bashani. Ndipo Ogu, mfalme wa Bashani, akatoka pamoja na watu wake wote ili kupigana vita nasi kule Edrei.+ 2 Basi Yehova akaniambia, ‘Usimwogope, kwa maana nitamtia mikononi mwako pamoja na watu wake wote na nchi yake, nawe utamtendea kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeishi Heshboni.’ 3 Basi Yehova Mungu wetu akamtia pia mikononi mwetu Mfalme Ogu wa Bashani pamoja na watu wake wote, nasi tukaendelea kumshambulia hivi kwamba hakuna mtu yeyote kati ya watu wake aliyeokoka. 4 Kisha tukateka majiji yake yote. Hakuna mji wao hata mmoja ambao hatukuuteka, tuliteka majiji 60 katika eneo lote la Argobu, yaani, ufalme wa Ogu kule Bashani.+ 5 Majiji hayo yote yalikuwa na kuta ndefu zenye ngome, malango, na makomeo, tuliteka pia miji mingi sana ya mashambani. 6 Hata hivyo, tuliwaangamiza,+ kama tulivyomwangamiza Mfalme Sihoni wa Heshboni, tuliangamiza kila jiji, kutia ndani wanaume, wanawake, na watoto.+ 7 Nasi tukajichukulia mifugo yote na nyara za majiji hayo.

8 “Wakati huo tulichukua nchi ya wafalme wawili wa Waamori+ waliokuwa katika eneo la Yordani, kuanzia Bonde* la Arnoni mpaka Mlima Hermoni+ 9 (Wasidoni walikuwa wakiuita mlima huo Sirioni, nao Waamori walikuwa wakiuita Seniri), 10 majiji yote yaliyokuwa katika nchi tambarare, nchi yote ya Gileadi, nchi yote ya Bashani mpaka Saleka na Edrei,+ majiji ya ufalme wa Ogu kule Bashani. 11 Kwa maana Mfalme Ogu wa Bashani ndiye Mrefaimu pekee aliyekuwa amebaki. Jeneza lake lilitengenezwa kwa chuma,* na bado liko katika jiji la Waamoni la Raba. Lina urefu wa mikono tisa* na upana wa mikono minne, kulingana na kipimo cha kawaida cha mkono. 12 Wakati huo tulimiliki nchi hii: kuanzia Aroeri,+ karibu na Bonde* la Arnoni, na nusu ya eneo lenye milima la Gileadi, na majiji yake nimewapa watu wa kabila la Rubeni na kabila la Gadi.+ 13 Kisha nusu ya kabila la Manase+ nimewapa sehemu inayobaki ya Gileadi na eneo lote la Bashani la ufalme wa Ogu. Eneo lote la Argobu, la Bashani, lilijulikana kuwa nchi ya Warefaimu.

14 “Yairi+ mwana wa Manase alichukua eneo lote la Argobu+ hadi kwenye mpaka wa Wageshuri na Wamaakathi,+ akaviita vijiji hivyo vya Bashani kwa jina lake mwenyewe, Hawoth-yairi,*+ mpaka leo. 15 Naye Makiri nimempa Gileadi.+ 16 Na watu wa kabila la Rubeni na kabila la Gadi+ nimewapa kuanzia Gileadi mpaka kwenye Bonde* la Arnoni, katikati ya bonde ulikuwa ndio mpaka, hadi Bonde la Yaboki, ambalo ni mpaka wa Waamoni, 17 na Araba na Yordani na ule mpaka, kuanzia Kinerethi hadi Bahari ya Araba, Bahari ya Chumvi, chini ya mteremko wa Pisga kuelekea upande wa mashariki.+

18 “Kisha nikawaamuru hivi: ‘Yehova Mungu wenu amewapa nchi hii mwimiliki. Wanaume wenu wote mashujaa watachukua silaha na kuvuka mbele ya ndugu zenu, Waisraeli.+ 19 Lakini wake zenu, watoto wenu, na wanyama wenu tu (najua vizuri kwamba mna wanyama wengi sana) ndio watakaoendelea kukaa katika majiji ambayo nimewapa, 20 mpaka Yehova atakapowapumzisha ndugu zenu, kama anavyowapumzisha ninyi, nao pia waimiliki nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa ng’ambo ya Yordani. Ndipo mtakaporudi, kila mmoja atarudi kwenye miliki yake ambayo nimempa.’+

21 “Wakati huo nilimwamuru hivi Yoshua:+ ‘Umeona kwa macho yako mwenyewe mambo ambayo Yehova Mungu wako amewatendea wafalme hao wawili. Hivyo ndivyo Yehova atakavyozitendea falme zote huko mnakovuka kwenda.+ 22 Msiwaogope, kwa maana Yehova Mungu wenu ndiye anayewapigania ninyi.’+

23 “Wakati huo nilimsihi hivi Yehova: 24 ‘Ee Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova, umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye nguvu,+ kwa maana ni mungu gani mbinguni au duniani anayetenda mambo makuu kama wewe?+ 25 Tafadhali niruhusu nivuke na kuona nchi nzuri iliyo ng’ambo ya Yordani, eneo hili zuri lenye milima na Lebanoni.’+ 26 Lakini bado Yehova alikuwa amenikasirikia vikali kwa sababu yenu,+ naye hakutaka kunisikiliza. Badala yake Yehova aliniambia, ‘Imetosha! Usizungumze nami tena kamwe kuhusu jambo hili. 27 Panda juu ya kilele cha Pisga,+ utazame magharibi na kaskazini na kusini na mashariki, uone nchi hiyo kwa macho yako, kwa maana hutavuka mto huu wa Yordani.+ 28 Nawe umweke Yoshua+ kuwa kiongozi, umtie moyo na kumwimarisha, kwa sababu yeye ndiye atakayewaongoza watu hawa kuvuka+ na kuwawezesha kuirithi nchi utakayoiona.’ 29 Mambo hayo yote yalitendeka tulipokuwa tukikaa katika bonde lililo mbele ya Beth-peori.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki