-
Isaya 11:6-9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Mbwamwitu atakaa pamoja na mwanakondoo kwa muda fulani,+
Na chui atalala pamoja na mwanambuzi,
Na ndama na simba* na mnyama aliyenoneshwa wote watakuwa pamoja;*+
Na mvulana mdogo atawaongoza.
7 Ng’ombe na dubu watakula pamoja,
Na watoto wao watalala pamoja.
Simba atakula majani kama ng’ombe dume.+
8 Na mtoto anayenyonya atacheza juu ya shimo la swila,
Na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake juu ya shimo la nyoka mwenye sumu.
-
-
Isaya 35:9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Hakuna simba atakayekuwa huko,
Na hakuna wanyama hatari wa mwituni watakaokuja kwenye njia hiyo.
-