Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 14
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Njia zisizofaa za kuomboleza (1, 2)

      • Vyakula safi na visivyo safi (3-21)

      • Sehemu ya kumi kwa ajili ya Yehova (22-29)

Kumbukumbu la Torati 14:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kutia (kunyoa) upara katikati ya macho yenu.”

Marejeo

  • +Law 19:28
  • +Law 21:1, 5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    9/15/2004, uku. 27

  • Fahirishi ya Machapisho

    w04 9/15 27

Kumbukumbu la Torati 14:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mali yake anayothamini sana.”

Marejeo

  • +Law 19:2; 20:26; Kum 28:9; 1Pe 1:15
  • +Kut 19:5, 6; Kum 7:6

Kumbukumbu la Torati 14:3

Marejeo

  • +Law 11:43; 20:25; Mdo 10:14

Kumbukumbu la Torati 14:4

Marejeo

  • +Law 11:2, 3

Kumbukumbu la Torati 14:7

Marejeo

  • +Law 11:4-8

Kumbukumbu la Torati 14:9

Marejeo

  • +Law 11:9, 10

Kumbukumbu la Torati 14:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “tai mla mizoga.”

Marejeo

  • +Law 11:13-20

Kumbukumbu la Torati 14:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mdudu.”

Kumbukumbu la Torati 14:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “malango.”

Marejeo

  • +Kut 22:31; Law 17:15
  • +Kut 23:19; 34:26

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    The Watchtower,

    7/1/2005, uku. 27

    9/15/2004, uku. 26

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 7/1 27; w04 9/15 26

Kumbukumbu la Torati 14:22

Marejeo

  • +Kum 12:11; 26:12

Kumbukumbu la Torati 14:23

Marejeo

  • +Kum 12:5, 17; 15:19, 20
  • +Zb 111:10

Kumbukumbu la Torati 14:24

Marejeo

  • +Kum 12:5, 6

Kumbukumbu la Torati 14:26

Marejeo

  • +Kum 12:7; 26:11; Zb 100:2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (2010),

    2/1/2010, uku. 23

  • Fahirishi ya Machapisho

    w10 2/1 23

Kumbukumbu la Torati 14:27

Marejeo

  • +Hes 18:21; 2Nya 31:4; 1Ko 9:13
  • +Hes 18:20; Kum 10:9

Kumbukumbu la Torati 14:28

Marejeo

  • +Kum 26:12

Kumbukumbu la Torati 14:29

Marejeo

  • +Kut 22:21; Kum 10:18; Yak 1:27
  • +Kum 15:10; Zb 41:1; Met 11:24; 19:17; Mal 3:10; Lu 6:35

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 14:1Law 19:28
Kum. 14:1Law 21:1, 5
Kum. 14:2Law 19:2; 20:26; Kum 28:9; 1Pe 1:15
Kum. 14:2Kut 19:5, 6; Kum 7:6
Kum. 14:3Law 11:43; 20:25; Mdo 10:14
Kum. 14:4Law 11:2, 3
Kum. 14:7Law 11:4-8
Kum. 14:9Law 11:9, 10
Kum. 14:12Law 11:13-20
Kum. 14:21Kut 22:31; Law 17:15
Kum. 14:21Kut 23:19; 34:26
Kum. 14:22Kum 12:11; 26:12
Kum. 14:23Kum 12:5, 17; 15:19, 20
Kum. 14:23Zb 111:10
Kum. 14:24Kum 12:5, 6
Kum. 14:26Kum 12:7; 26:11; Zb 100:2
Kum. 14:27Hes 18:21; 2Nya 31:4; 1Ko 9:13
Kum. 14:27Hes 18:20; Kum 10:9
Kum. 14:28Kum 26:12
Kum. 14:29Kut 22:21; Kum 10:18; Yak 1:27
Kum. 14:29Kum 15:10; Zb 41:1; Met 11:24; 19:17; Mal 3:10; Lu 6:35
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 14:1-29

Kumbukumbu la Torati

14 “Ninyi ni wana wa Yehova Mungu wenu. Msijikatekate+ wala kunyoa upara kwenye mapaji ya nyuso zenu* kwa ajili ya mtu aliyekufa.+ 2 Kwa maana ninyi ni watu watakatifu+ kwa Yehova Mungu wenu, na Yehova amewachagua ninyi muwe watu wake, mali yake ya pekee,* kutoka kati ya mataifa yote duniani.+

3 “Msile kitu chochote kinachochukiza.+ 4 Hawa ndio wanyama mnaoweza kula:+ ng’ombe, kondoo, mbuzi, 5 paa, swala, kulungu, mbuzi mwitu, mbawala, kondoo mwitu, na kondoo wa mlimani. 6 Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizopasuka na zilizogawanyika mara mbili na ambaye anacheua. 7 Lakini hampaswi kuwala wanyama wafuatao wanaocheua au wenye kwato zilizogawanyika: ngamia, sungura, na wibari, kwa sababu wanacheua lakini kwato zao hazijapasuka. Wao si safi kwenu.+ 8 Pia, msimle nguruwe kwa sababu ana kwato zilizopasuka lakini hacheui. Yeye si safi kwenu. Msile kamwe nyama yao wala kugusa mizoga yao.

9 “Kati ya viumbe wote wanaoishi ndani ya maji, mnaweza kula wafuatao: Mnaweza kumla kiumbe yeyote mwenye mapezi na magamba.+ 10 Lakini hampaswi kumla kiumbe yeyote ambaye hana mapezi na magamba. Yeye si safi kwenu.

11 “Mnaweza kumla ndege yeyote aliye safi. 12 Lakini hampaswi kuwala ndege wafuatao: tai, furukombe, tumbusi mweusi,*+ 13 mwewe mwekundu, mwewe mweusi, kila aina ya ndege mbua, 14 kila aina ya kunguru, 15 mbuni, bundi, shakwe, kila aina ya kipanga, 16 bundi mdogo, bundi mwenye masikio marefu, batamaji, 17 mwari, tumbusi, mnandi, 18 korongo, kila aina ya kulastara, hudihudi, na popo. 19 Pia, kila kiumbe* mwenye mabawa anayeishi katika makundi makubwa si safi kwenu. Hawapaswi kuliwa. 20 Mnaweza kumla kiumbe yeyote safi anayeruka.

21 “Msimle mnyama yeyote aliyepatikana amekufa.+ Mnaweza kumpa mkaaji mgeni aliye ndani ya majiji yenu,* naye anaweza kumla, au mnyama huyo anaweza kuuzwa kwa mgeni. Kwa maana ninyi ni watu watakatifu kwa Yehova Mungu wenu.

“Msimchemshe mwanambuzi katika maziwa ya mama yake.+

22 “Ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya mazao ya shambani yanayotokana na mbegu zenu mwaka baada ya mwaka.+ 23 Mtakula sehemu ya kumi ya nafaka yenu, divai yenu mpya, mafuta yenu, na wazaliwa wa kwanza wa ng’ombe wenu na kondoo wenu mbele za Yehova Mungu wenu mahali ambapo atachagua jina lake likae hapo,+ ili mjifunze kumwogopa Yehova Mungu wenu sikuzote.+

24 “Lakini ikiwa safari ni ndefu sana kwenu na hivyo hamwezi kupeleka vitu hivyo mahali ambapo Yehova Mungu wenu amechagua jina lake likae hapo,+ kwa sababu ni mbali sana (kwa sababu Yehova Mungu wenu atawabariki), 25 basi mnaweza kubadilisha vitu hivyo kwa pesa, na mbebe pesa hizo mikononi mwenu na kwenda mahali ambapo Yehova Mungu wenu atachagua. 26 Kisha mnaweza kutumia pesa hizo kununua chochote mnachotamani, iwe ni ng’ombe, kondoo, mbuzi, divai na vinywaji vingine vyenye kileo, na kitu chochote mpendacho; nanyi mtakula huko mbele za Yehova Mungu wenu na kushangilia, ninyi na familia zenu.+ 27 Na msimpuuze Mlawi yeyote aliye ndani ya majiji yenu,+ kwa sababu hana fungu wala urithi pamoja nanyi.+

28 “Mwishoni mwa kila miaka mitatu mnapaswa kuleta sehemu yote ya kumi ya mazao yenu ya mwaka huo na kuyahifadhi ndani ya majiji yenu.+ 29 Kisha Mlawi, ambaye hana fungu wala urithi kati yenu, mkaaji mgeni, yatima, na mjane aliye ndani ya majiji yenu atakuja kula na kushiba,+ ili Yehova Mungu wenu awabariki katika mambo yote mnayofanya.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki