Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 19
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Hatia ya damu na majiji ya makimbilio (1-13)

      • Alama za mipaka zisisogezwe (14)

      • Mashahidi mahakamani (15-21)

        • Mashahidi wawili au watatu wahitajika (15)

Kumbukumbu la Torati 19:1

Marejeo

  • +Kum 7:1; 9:1

Kumbukumbu la Torati 19:2

Marejeo

  • +Hes 35:14; Yos 20:7, 9

Kumbukumbu la Torati 19:3

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    11/2017, uku. 14

Kumbukumbu la Torati 19:4

Marejeo

  • +Hes 35:15; Kum 4:42

Kumbukumbu la Torati 19:5

Marejeo

  • +Hes 35:25

Kumbukumbu la Torati 19:6

Marejeo

  • +Hes 35:12, 19
  • +Yos 20:4, 5

Kumbukumbu la Torati 19:8

Marejeo

  • +Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 11:24
  • +Mwa 28:14

Kumbukumbu la Torati 19:9

Marejeo

  • +Kum 11:22, 23
  • +Yos 20:7, 8

Kumbukumbu la Torati 19:10

Marejeo

  • +Met 6:16, 17
  • +Kum 21:6-9

Kumbukumbu la Torati 19:11

Marejeo

  • +1Yo 3:15

Kumbukumbu la Torati 19:12

Marejeo

  • +Mwa 9:6; Kut 21:12; Hes 35:16; Kum 27:24

Kumbukumbu la Torati 19:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Jicho lenu lisimhurumie.”

Marejeo

  • +Law 24:17, 21; Hes 35:33; 2Sa 21:1

Kumbukumbu la Torati 19:14

Marejeo

  • +Kum 27:17

Kumbukumbu la Torati 19:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kinywa cha.”

Marejeo

  • +Hes 35:30; Kum 17:6
  • +Mt 18:16; Yoh 8:17; 2Ko 13:1; 1Ti 5:19

Kumbukumbu la Torati 19:16

Marejeo

  • +Kut 23:1; 1Fa 21:13; Mk 14:56

Kumbukumbu la Torati 19:17

Marejeo

  • +Kum 17:8, 9

Kumbukumbu la Torati 19:18

Marejeo

  • +Kum 13:14; 17:4; 2Nya 19:6

Kumbukumbu la Torati 19:19

Marejeo

  • +Met 19:5
  • +Kum 21:20, 21; 24:7; 1Ko 5:13

Kumbukumbu la Torati 19:20

Marejeo

  • +Kum 13:11; 17:13; 1Ti 5:20

Kumbukumbu la Torati 19:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Jicho lenu halipaswi.”

  • *

    Tnn., “Nafsi itatolewa kwa nafsi.”

Marejeo

  • +Kum 19:13
  • +Kut 21:23-25; Law 24:20; Mt 5:38

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Maswali ya Biblia Yajibiwa, makala 149

    Mkaribie Yehova, kur. 131-133

    Ulimwengu Usio na Vita, uku. 14

  • Fahirishi ya Machapisho

    cl 131, 133

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 19:1Kum 7:1; 9:1
Kum. 19:2Hes 35:14; Yos 20:7, 9
Kum. 19:4Hes 35:15; Kum 4:42
Kum. 19:5Hes 35:25
Kum. 19:6Hes 35:12, 19
Kum. 19:6Yos 20:4, 5
Kum. 19:8Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 11:24
Kum. 19:8Mwa 28:14
Kum. 19:9Kum 11:22, 23
Kum. 19:9Yos 20:7, 8
Kum. 19:10Met 6:16, 17
Kum. 19:10Kum 21:6-9
Kum. 19:111Yo 3:15
Kum. 19:12Mwa 9:6; Kut 21:12; Hes 35:16; Kum 27:24
Kum. 19:13Law 24:17, 21; Hes 35:33; 2Sa 21:1
Kum. 19:14Kum 27:17
Kum. 19:15Hes 35:30; Kum 17:6
Kum. 19:15Mt 18:16; Yoh 8:17; 2Ko 13:1; 1Ti 5:19
Kum. 19:16Kut 23:1; 1Fa 21:13; Mk 14:56
Kum. 19:17Kum 17:8, 9
Kum. 19:18Kum 13:14; 17:4; 2Nya 19:6
Kum. 19:19Met 19:5
Kum. 19:19Kum 21:20, 21; 24:7; 1Ko 5:13
Kum. 19:20Kum 13:11; 17:13; 1Ti 5:20
Kum. 19:21Kum 19:13
Kum. 19:21Kut 21:23-25; Law 24:20; Mt 5:38
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 19:1-21

Kumbukumbu la Torati

19 “Yehova Mungu wenu atakapoyaangamiza mataifa ambayo Yehova Mungu wenu anawapa nchi yao na mtakapokuwa mmemiliki nchi yao na kuishi katika majiji yao na nyumba zao,+ 2 mnapaswa kutenga majiji matatu katikati ya nchi yenu ambayo Yehova Mungu wenu anawapa mwimiliki.+ 3 Mnapaswa kugawanya mara tatu eneo la nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa mwimiliki, nanyi mtengeneze barabara ili muuaji yeyote aweze kukimbilia katika mojawapo ya majiji hayo.

4 “Sasa hivi ndivyo itakavyokuwa kuhusu muuaji ambaye huenda akakimbilia humo ili kuokoa uhai wake: Akimuua jirani yake bila kukusudia naye hakuwa akimchukia;+ 5 kwa mfano, anapoenda na jirani yake msituni kukusanya kuni, kisha anainua mkono wake ili akate mti kwa shoka, lakini shoka lichomoke kwenye mpini na kumgonga jirani yake na kumuua, muuaji huyo anapaswa kukimbilia katika mojawapo ya majiji hayo.+ 6 Asipofanya hivyo, mtu anayelipiza kisasi cha damu+ anaweza kwa hasira kali kumkimbiza, kumkamata, na kumuua, kwa sababu jiji hilo lilikuwa mbali sana. Hata hivyo, hakustahili kufa kwa sababu hakuwa akimchukia jirani yake.+ 7 Ndiyo sababu ninawaamuru hivi: ‘Tengeni majiji matatu.’

8 “Yehova Mungu wenu akipanua eneo lenu kama alivyowaapia mababu zenu+ na kuwapa nchi yote aliyoahidi kuwapa mababu zenu+ 9 —maadamu mnashika kwa uaminifu amri hii yote ninayowapa leo, kwa kumpenda Yehova Mungu wenu na kutembea daima katika njia zake+—basi mtaongeza majiji mengine matatu zaidi ya hayo matatu.+ 10 Hivyo hakuna damu isiyo na hatia itakayomwagwa+ katika nchi yenu ambayo Yehova Mungu wenu anawapa kuwa urithi, nanyi hamtakuwa na hatia yoyote ya damu.+

11 “Lakini ikiwa mtu alikuwa akimchukia jirani yake,+ akamvizia, akamjeruhi vibaya sana na kumuua, na mtu huyo amekimbilia katika mojawapo ya majiji hayo, 12 basi wazee wa jiji lake wanapaswa kumwita kutoka humo na kumtia mikononi mwa yule anayelipiza kisasi cha damu, naye lazima afe.+ 13 Hampaswi kumhurumia,* nanyi lazima mwondoe hatia ya damu isiyo na hatia kutoka katika Israeli,+ ili mambo yawaendee vyema.

14 “Mtakapopokea urithi wenu katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa mwimiliki, hampaswi kusogeza alama ya mpaka+ wa jirani yenu kutoka mahali ambapo uliwekwa na mababu zenu.

15 “Shahidi mmoja hawezi kufanya mtu mwingine ahukumiwe kwa kosa lolote au dhambi yoyote ambayo huenda ametenda.+ Jambo hilo linapaswa kuthibitishwa kwa ushahidi wa* mashahidi wawili au mashahidi watatu.+ 16 Shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akitoa ushahidi dhidi ya mtu na kumshtaki kwa kosa fulani,+ 17 watu hao wawili wanaozozana watasimama mbele za Yehova, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwa wakihudumu wakati huo.+ 18 Waamuzi watachunguza jambo hilo kikamili,+ na ikiwa mtu huyo ni shahidi wa uwongo na ameleta shtaka la uwongo dhidi ya ndugu yake, 19 mnapaswa kumtendea kama alivyopanga kumtendea ndugu yake kwa hila,+ nanyi lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.+ 20 Wale wanaobaki watasikia na kuogopa, nao hawatatenda tena kamwe uovu kama huo miongoni mwenu.+ 21 Hampaswi* kuwahurumia:+ Uhai utatolewa kwa uhai,* jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki