Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1993
MAAGIZO
Wakati wa 1993, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango ya kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Kiongozi cha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi [sg-SW], Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi [gt-SW], Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW], na “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation [*td] au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW] vitakuwa msingi wa migawo.
Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha, kisha itaendelea hivi:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma mwenye kustahili. Hotuba hii itategemea habari katika kitabu “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” au Kiongozi cha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi. Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika sehemu hiyo. Lengo lapasa kuwa si kufanya mwenezo wa habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kundi yakikaziwa. Mahali inapohitajiwa, kichwa kimepasa kichaguliwe. Wote wanatiwa moyo wafanye matayarisho ya kimbele kwa uangalifu ili wanufaike kikamili na habari hiyo.
Ndugu waliogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa iwapo lazima.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Hii yapasa ishughulikiwe na mwangalizi wa shule au mzee mwingine anayestahili au na mtumishi wa huduma aliyepewa mgawo na mwangalizi wa shule. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliotolewa kuwa mgawo usomwe. Baada ya kutoa mwono wa ujumla wa sekunde 30 hadi 60 wa sura zilizotolewa kuwa mgawo, saidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Chunguza matoleo ya Mnara wa Mlinzi upate habari zaidi za kukaziwa. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Hii ni kusoma Biblia juu ya habari iliyotolewa kuwa mgawo itakayotolewa na ndugu. Hii itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia, na hata katika mambo makuu ya katikati. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na jinsi kanuni zinavyohusu, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo yapasa hasa isomwe bila kukatizwa.
HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa dada. Vichwa vya hotuba hii vitategemea kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Mwanafunzi aliyegawiwa apaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hii, mwanafunzi aweza kuwa ameketi au amesimama. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi wa ziada wanaweza kutumiwa. Ni afadhali vikao vihusishe utumishi wa shambani au utoaji wa ushahidi wa vivi hivi. Anayetoa hotuba aweza ama kuanzisha mazungumzo ili kuweka kikao au kuacha msaidizi (wasaidizi) wake afanye hivyo. Habari wala si kikao ndiyo ya kufikiriwa kwanza. Mwanafunzi apaswa kutumia kichwa kilichoonyeshwa.
HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Inapogawiwa ndugu, yapaswa iwe hotuba inayotolewa kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi ndugu huyo atayarishe hotuba yake akiwa anafikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Hata hivyo, endapo habari hiyo yataka kikao cha aina nyingine ya wasikilizaji chenye kutumika na kinachofaa, ndugu huyo aweza kuchagua kusitawisha hotuba yake kwa njia hiyo. Mwanafunzi apaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
Inapogawiwa dada, habari hii yapasa itolewe kama ambavyo Hotuba Na. 3 imetolewa muhtasari.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, si lazima afuate mpango wa shauri lenye kufuliza kama ilivyoandikwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala yake, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri amepaswa atie duara kuzunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atafanyia kazi safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V” “M” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati, na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa ule utoaji wa mambo makuu ya Biblia haukuridhisha, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA HOTUBA: Ndugu wanaotoa Mgawo Na. 1 wapaswa wachague kichwa inapohitajiwa. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya pili wapaswa kuchagua kichwa kitakachowezesha mwenezo unaofaa zaidi wa habari hiyo. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya tatu na ya nne wapaswa watumie kichwa kilichoonyeshwa. Kabla ya kutoa hotuba, ingefaa wanafunzi warudie kusoma habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulika na sifa ya usemi inayofanyiwa kazi.
KUFUATA WAKATI: Hotuba, wala shauri na maelezo ya mshauri hazipasi kupita wakati uliowekwa. Hotuba Na. 2 hadi 4 zapasa zikatizwe kwa busara ikiwa wakati unakwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa “ishara ya kuacha” amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 wanapopitisha wakati wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wapaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Programu kwa jumla: Dakika 45, bila wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi, pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari na kukamilisha ratiba ya kusoma Biblia. Biblia pekee ndiyo ya kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atapitia majibu ya maswali ya pitio pamoja na wasikilizaji na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kutumiwa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.
MAKUNDI MAKUBWA NA MADOGO: Makundi yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasiobatizwa wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kundi wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa dhati. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule anaweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
*td – “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation
Jan. 4 Kusoma Biblia: 1 Samweli 25 hadi 27
Na. 1: sg-SW kur. 84-8 maf. 1-9
Na. 2: 1 Samweli 26:7-25
Na. 3: Somo la Rehema (gt-SW sura 40)
Na. 4: Ni Nini Kuchukuliwa Kimwili Kutoka Duniani, na ‘Kudakwa’ Ili Kuwa Pamoja na Bwana Kunamaanisha Nini Hasa? (rs-SW uku. 113 fu. 1)
Jan. 11 Kusoma Biblia: 1 Samweli 28 hadi 31
Na. 1: 1 Samweli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 57-8 maf. 27-35)
Na. 2: 1 Samweli 30:7-25
Na. 3: Yesu Kibishanio (gt-SW sura 41)
Na. 4: *td 1A au td-SW 12A Kwa Nini Mtu Asiwaabudu Wazazi Waliokufa?
Jan. 18 Kusoma Biblia: 2 Samweli 1 hadi 4
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Samweli (si-SW uku. 59 maf. 1-5)
Na. 2: 2 Samweli 1:1-4, 17-27
Na. 3: Yesu Akemea Mafarisayo (gt-SW sura 42)
Na. 4: Ni Akina Nani ‘Wanaodakwa Katika Mawingu’ Wakawe Pamoja na Bwana? (rs-SW uku. 113 fu. 2)
Jan. 25 Kusoma Biblia: 2 Samweli 5 hadi 8
Na. 1: sg-SW kur. 88-90 maf. 10-15
Na. 2: 2 Samweli 6:1-19
Na. 3: Vielezi Vitano Akiwa Kwenye Mashua (gt-SW sura 43 maf. 1-8)
Na. 4: *td 1B au td-SW 12B Sababu Wanadamu Wanaweza Kuheshimiwa Lakini Mungu Peke Yake Aabudiwe
Feb. 1 Kusoma Biblia: 2 Samweli 9 hadi 12
Na. 1: sg-SW kur. 90-2 maf. 1-7
Na. 2: 2 Samweli 10:1-14
Na. 3: Jinsi Wanafunzi Wanavyofaidika Kutokana na Mafundisho ya Yesu (gt-SW sura 43 maf. 9-19)
Na. 4: Bwana ‘Ashukapo Kutoka Mbinguni,’ Hataonekana na Macho (rs-SW uku. 114 maf. 1, 2)
Feb. 8 Kusoma Biblia: 2 Samweli 13 hadi 15
Na. 1: sg-SW kur. 92-5 maf. 8-18
Na. 2: 2 Samweli 15:1-17
Na. 3: Yesu Awabariki Wanafunzi Wake kwa Mafundisho Zaidi (gt-SW sura 43 maf. 20-31)
Na. 4: *td 2A au td-SW 7A Uovu Utamalizwaje?
Feb. 15 Kusoma Biblia: 2 Samweli 16 hadi 18
Na. 1: sg-SW kur. 96-9 maf. 1-10
Na. 2: 2 Samweli 18:1-17
Na. 3: Yesu Anyamazisha Dhoruba Inayotisha (gt-SW sura 44)
Na. 4: Ni Katika Maana Gani Wanadamu ‘Watamwona’ Bwana “Akija Katika Wingu”? (rs-SW uku. 114 fu. 3)
Feb. 22 Kusoma Biblia: 2 Samweli 19 hadi 21
Na. 1: sg-SW kur. 100-102 maf. 1-12
Na. 2: 2 Samweli 19:1-14
Na. 3: Mtu Mwenye Kupagawa na Roho Waovu Awa Mwanafunzi (gt-SW sura 45)
Na. 4: *td 2B au td-SW 7C Kwa Nini Har–Magedoni Itakuwa Tendo Lenye Upendo kwa Upande wa Mungu?
Mac. 1 Kusoma Biblia: 2 Samweli 22 hadi 24
Na. 1: 2 Samweli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 63 maf. 28-31)
Na. 2: 2 Samweli 22:1-4, 24-36
Na. 3: Aligusa Vazi Lake (gt-SW sura 46)
Na. 4: Sababu Wakristo Hawawezi Kuchukuliwa Mbinguni Wakiwa na Miili Yao ya Asili (rs-SW uku. 115 maf. 1, 2)
Mac. 8 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 1 na 2
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Wafalme (si-SW kur. 64-5 maf. 1-5)
Na. 2: 1 Wafalme 1:32-48
Na. 3: Machozi Yalibadilika Yakawa Pindi Yenye Furaha Kubwa (gt-SW sura 47)
Na. 4: *td 3A au td-SW 41A Ubatizo Ni Takwa la Kikristo
Mac. 15 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 3 hadi 6
Na. 1: sg-SW kur. 103-8 maf. 13-21
Na. 2: 1 Wafalme 3:10-28
Na. 3: Ijapokuwa Miujiza Yake, Yesu Akataliwa Mbali (gt-SW sura 48)
Na. 4: Je! Wakristo Waaminifu Watakwenda Mbinguni kwa Siri, kwa Kutoweka Kutoka Duniani Bila Kufa? (rs-SW uku. 115 fu. 3 hadi uku. 116 fu. 1)
Mac. 22 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 7 na 8
Na. 1: sg-SW kur. 108-12 maf. 1-20
Na. 2: 1 Wafalme 8:54-66
Na. 3: Safari ya Tatu ya Kuhubiri Galilaya (gt-SW sura 49)
Na. 4: *td 3B au td-SW 41B Ubatizo Hausafishi Dhambi
Mac. 29 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 9 hadi 11
Na. 1: sg-SW kur. 113-16 maf. 1-16
Na. 2: 1 Wafalme 10:1-13
Na. 3: Kuwatayarisha Wanafunzi Wake Ili Wakabiliane na Upinzani (gt-SW sura 50)
Na. 4: Je! Wakristo Waaminifu Wote Watachukuliwa Kimuujiza Kutoka Duniani Kabla ya Dhiki Kubwa? (rs-SW uku. 116 maf. 2, 3)
Apr. 5 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 12 hadi 14
Na. 1: sg-SW kur. 116-18 maf. 1-12
Na. 2: 1 Wafalme 12:1-15
Na. 3: Uuaji Kimakusudi Wakati wa Karamu ya Siku ya Kuzaliwa (gt-SW sura 51)
Na. 4: *td 4A au td-SW 1A Biblia kwa Kweli Imepuliziwa Roho?
Apr. 12 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 15 hadi 17
Na. 1: sg-SW kur. 119-21 maf. 13-28
Na. 2: 1 Wafalme 17:1-16
Na. 3: Yesu Alisha Maelfu kwa Muujiza (gt-SW sura 52)
Na. 4: Wakristo Watalindwaje Wakati wa Dhiki Kubwa? (rs-SW uku. 116 maf. 4, 5)
Apr. 19 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 18 hadi 20
Na. 1: sg-SW kur. 122-5 maf. 1-21
Na. 2: 1 Wafalme 18:25-40
Na. 3: Yesu Anapotembea Juu ya Maji (gt-SW sura 53)
Na. 4: *td 4B au td-SW 1C Sababu Biblia Ni Uongozi Unaofaa Siku Zetu
Apr. 26 Pitio la Kuandika. Kamilisha 1 Samweli 25 hadi 1 Wafalme 20
Mei 3 Kusoma Biblia: 1 Wafalme 21 na 22
Na. 1: 1 Wafalme—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 68-9 maf. 23-26)
Na. 2: 1 Wafalme 21:15-29
Na. 3: Mkate Kutoka Mbinguni—Zawadi Itokayo kwa Nani? (gt-SW sura 54)
Na. 4: Kwa Nini Wakristo Fulani Wanachukuliwa Kwenda Mbinguni, na Je, Watarudi Kuishi Milele Duniani? (rs-SW uku. 117 maf. 5-8)
Mei 10 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wafalme (si-SW uku. 69 maf. 1-4)
Na. 2: 2 Wafalme 2:1-14
Na. 3: Sababu ya Wengi Kuacha Kumfuata Yesu (gt-SW sura 55)
Na. 4: *td 4C au td-SW 1F Biblia Iliandikwa kwa Faida ya Nani?
Mei 17 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 4 hadi 6
Na. 1: sg-SW kur. 126-9 maf. 1-22
Na. 2: 2 Wafalme 5:1-14
Na. 3: Ni Nini Kinachochafua Mtu? (gt-SW sura 56)
Na. 4: Fundisho la Kuzaliwa Upya Katika Mwili Mwingine Haliungwi Mkono na Biblia (rs-SW uku. 154 fu. 2 hadi uku. 156 fu. 4)
Mei 24 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 7 hadi 9
Na. 1: sg-SW kur. 130-3 maf. 1-20
Na. 2: 2 Wafalme 9:1-14
Na. 3: Huruma ya Yesu kwa Waliosumbuka (gt-SW sura 57)
Na. 4: *td 5A au td-SW 2A Kutiwa Damu Mishipani Kunaharibu Utakatifu wa Damu
Mei 31 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 10 hadi 12
Na. 1: sg-SW kur. 133-5 maf. 1-8
Na. 2: 2 Wafalme 10:15-30
Na. 3: Yesu Asahihisha Kutokuelewa Fulani (gt-SW sura 58)
Na. 4: Fundisho la Biblia Juu ya Nafsi na Kifo Haliruhusu Kuzaliwa Upya Katika Mwili Mwingine (rs-SW uku. 157 fu. 1-3)
Juni 7 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 13 hadi 15
Na. 1: sg-SW kur. 135-8 maf. 9-21
Na. 2: 2 Wafalme 13:14-25
Na. 3: Kwa Kweli Yesu Ni Nani? (gt-SW sura 59)
Na. 4: *td 5B au td-SW 2B Je! Uhai wa Mtu Uokolewe kwa Vyovyote?
Juni 14 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 16 hadi 18
Na. 1: sg-SW kur. 138-41 maf. 1-19
Na. 2: 2 Wafalme 17:1-15
Na. 3: Mtazamo-Kimbele wa Utukufu wa Ufalme wa Kristo (gt-SW sura 60)
Na. 4: Kuna Tofauti Kadiri Gani Kati ya Kuzaliwa Upya Katika Mwili Mwingine na Tumaini Linalotolewa Katika Biblia? (rs-SW uku. 157 fu. 4 hadi uku. 158 fu. 1)
Juni 21 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 19 hadi 22
Na. 1: sg-SW kur. 142-5 maf. 1-15
Na. 2: 2 Wafalme 19:14-28, 35
Na. 3: Uwezo wa Imani (gt-SW sura 61)
Na. 4: *td 6A au td-SW 40D Tunajuaje Kwamba Nyakati za Wasio Wayahudi Ziliisha Katika 1914?
Juni 28 Kusoma Biblia: 2 Wafalme 23 hadi 25
Na. 1: 2 Wafalme—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 74 maf. 33-36)
Na. 2: 2 Wafalme 23:1-15
Na. 3: Somo Juu ya Unyenyekevu (gt-SW sura 62)
Na. 4: Kwa Nini Kuna Dini Nyingi Sana, na Ni Nani Aliye Mwanzilishi Wazo? (rs-SW uku. 67 maf. 1-3)
Julai 5 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Mambo ya Nyakati (si-SW kur. 75-6 maf. 1-7)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 3:1-16
Na. 3: Epukana na Kuwakwaza Wengine (gt-SW sura 63)
Na. 4: *td 7A au td-SW 10A Kanisa la Kweli Ni Gani na Msingi Wayo Ni Nini?
Julai 12 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 4 hadi 6
Na. 1: sg-SW kur. 145-8 maf. 16-34
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 5:1-17
Na. 3: Somo Juu ya Kusamehe (gt-SW sura 64)
Na. 4: Sababu Si Dini Zote Zinazokubalika kwa Mungu (rs-SW uku. 67 fu. 4 hadi uku. 68 fu. 5)
Julai 19 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 7 hadi 10
Na. 1: sg-SW kur. 149-50 maf. 1-8
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 7:1-12
Na. 3: Kisafari cha Siri Kwenda Yerusalemu (gt-SW sura 65)
Na. 4: *td 7B au td-SW 10D Je! Petro ndiye “Mwamba”?
Julai 26 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 11 hadi 14
Na. 1: sg-SW kur. 151-3 maf. 9-21
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 13:1-14
Na. 3: Hatari Kwenye Sikukuu ya Mahema (gt-SW sura 66)
Na. 4: Wakati Inapofaa Kuacha Dini ya Wazazi (rs-SW uku. 69 maf. 1-3)
Ago. 2 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 15 hadi 18
Na. 1: sg-SW kur. 153-6 maf. 1-14
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 17:1-15
Na. 3: Sababu ya Maofisa Kushindwa Kumkamata Yesu (gt-SW sura 67)
Na. 4: *td 8A au td-SW 50A Je! Sayansi ya Kweli Hukubaliana na Biblia?
Ago. 9 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 19 hadi 22
Na. 1: sg-SW kur. 156-8 maf. 15-24
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 22:6-19
Na. 3: Asili ya Yesu ya Kimungu na Wakati Ujao Wake Mbinguni (gt-SW sura 68 maf. 1-11)
Na. 4: Maoni ya Biblia Juu ya Kuchangamana na Dini Nyingine (rs-SW uku. 70 fu. 1 hadi uku. 71 fu. 2)
Ago. 16 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 23 hadi 26
Na. 1: sg-SW kur. 158-60 maf. 1-9
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 23:1-5, 24-32
Na. 3: Kweli Inayoweka Watu Huru (gt-SW sura 68 maf. 12-16)
Na. 4: *td 8B au td-SW 50B Je! Siku Moja ya Kuumba Ilikuwa ya Muda wa Saa 24?
Ago. 23 Kusoma Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 27 hadi 29
Na. 1: 1 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 78-9 maf. 22-25)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 27:23-34
Na. 3: Lile Swali la Ubaba (gt-SW sura 69)
Na. 4: Sababu Dini ya Kweli Lazima Iwe Imefanywa Tengenezo (rs-SW uku. 71 fu. 3 hadi uku. 72 fu. 2)
Ago. 30 Pitio la Kuandika. Kamilisha 1 Wafalme 21 hadi 1 Mambo ya Nyakati 29
Sept. 6 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 1 hadi 5
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Mambo ya Nyakati (si-SW kur. 79-80 maf. 1-6)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 5:1-14
Na. 3: Kuponya Mwanamume Aliyezaliwa Akiwa Kipofu (gt-SW sura 70)
Na. 4: *td 9A au td-SW 28A Kwa Nini Yesu Alitundikwa Kwenye Mti?
Sept. 13 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 6 hadi 8
Na. 1: sg-SW kur. 160-3 maf. 10-24
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 7:1-16
Na. 3: Mwombaji Awafadhaisha Mafarisayo (gt-SW sura 71)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Zaidi Yanahitajiwa Kuliko Kupenda Jirani (rs-SW uku. 72 fu. 4)
Sept. 20 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 9 hadi 12
Na. 1: sg-SW kur. 163-5 maf. 1-9
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 9:1-14
Na. 3: Yesu Awatuma Nje Wale 70 (gt-SW sura 72)
Na. 4: *td 9B au td-SW 28B Je! Wakristo Wauabudu Msalaba?
Sept. 27 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 13 hadi 17
Na. 1: sg-SW kur. 165-7 maf. 10-21
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 13:8-22
Na. 3: Ni Nani kwa Kweli Aliye Jirani Yetu? (gt-SW sura 73)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Zaidi Yanahitajiwa Kuliko Kuwa na Uhusiano wa Kibinafsi Pamoja na Mungu (rs-SW uku. 72 fu. 5 hadi uku. 73 fu. 1)
Okt. 4 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 18 hadi 21
Na. 1: sg-SW kur. 168-70 maf. 1-14
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 19:1-11
Na. 3: Shauri la Yesu kwa Martha (gt-SW sura 74 maf. 1-5)
Na. 4: *td 10A au td-SW 24A Kwa Nini Mwanadamu Hufa?
Okt. 11 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 22 hadi 25
Na. 1: sg-SW kur. 170-1 maf. 15-22
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 23:1-15
Na. 3: Uhitaji wa Kudumu Katika Sala (gt-SW sura 74 maf. 6-9)
Na. 4: Sababu Kuisoma Biblia tu Hakutoshi (rs-SW uku. 73 maf. 2, 3)
Okt. 18 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 26 hadi 28
Na. 1: sg-SW kur. 172-5 maf. 1-13
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 26:11-23
Na. 3: Itikio Lifaalo kwa Miujiza ya Yesu (gt-SW sura 75)
Na. 4: *td 10B au td-SW 24B Ni Nini Hali ya Wafu?
Okt. 25 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 29 na 30
Na. 1: sg-SW kur. 175-7 maf. 1-14
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 30:1-12
Na. 3: Yesu Awafunua Mafarisayo na Mawakili (gt-SW sura 76)
Na. 4: Dini ya Kweli Inategemea Biblia na Inajulisha Jina la Mungu (rs-SW uku. 73 maf. 4, 5)
Nov. 1 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 31 hadi 33
Na. 1: sg-SW kur. 177-80 maf. 15-29
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 32:10-22
Na. 3: Yesu Ashughulikia Suala la Urithi (gt-SW sura 77)
Na. 4: *td 10C au td-SW 24C Je! Inawezekana Kusema na Wafu?
Nov. 8 Kusoma Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 34 hadi 36
Na. 1: 2 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 84 maf. 34-36)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 34:22-33
Na. 3: Yesu Awasihi Wanafunzi Wake Waendelee Kuwa Tayari Kwa Ajili ya Kurudi Kwake (gt-SW sura 78)
Na. 4: Dini ya Kweli inaonyesha Imani ya Kweli Katika Yesu Kristo (rs-SW uku. 74 fu. 1)
Nov. 15 Kusoma Biblia: Ezra 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Ezra (si-SW uku. 85 maf. 1-7)
Na. 2: Ezra 3:1-13
Na. 3: Taifa Lapotea, Lakini Si Lote (gt-SW sura 79 maf. 1-5)
Na. 4: *td 11A au td-SW 9A Ibilisi Ni Nani?
Nov. 22 Kusoma Biblia: Ezra 4 hadi 7
Na. 1: sg-SW kur. 181-3 maf. 1-14
Na. 2: Ezra 6:1-13
Na. 3: Kuwakanusha Wale Wanaopinga Kuponya Katika Siku ya Sabato (gt-SW sura 79 maf. 6-9)
Na. 4: Dini ya Kweli Si ya Kisherehe Bali Ni Njia ya Maisha (rs-SW uku. 74 fu. 2)
Nov. 29 Kusoma Biblia: Ezra 8 hadi 10
Na. 1: Ezra—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 87 maf. 14-18)
Na. 2: Ezra 9:1-9, 15
Na. 3: Mazizi ya Kondoo na Mchungaji Mwema (gt-SW sura 80)
Na. 4: *td 11B au td-SW 9B Ni Nani Mtawala wa Ulimwengu?
Des. 6 Kusoma Biblia: Nehemia 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Nehemia (si-SW uku. 88 maf. 1-5)
Na. 2: Nehemia 3:1-14
Na. 3: Sababu Wanajaribu Kumuua Yesu (gt-SW sura 81)
Na. 4: Washiriki wa Dini ya Kweli Wanapendana na Wanajitenga na Ulimwengu (rs-SW uku. 74 maf. 3, 4)
Des. 13 Kusoma Biblia: Nehemia 4 hadi 6
Na. 1: sg-SW kur. 183-7 maf. 15-34
Na. 2: Nehemia 6:1-13
Na. 3: Ni Nani Ambao Hawataokolewa? (gt-SW sura 82 maf. 1-6)
Na. 4: *td 11C au td-SW 9D Mashetani Walitoka Wapi?
Des. 20 Kusoma Biblia: Nehemia 7 na 8
Na. 1: sg-SW kur. 187-91 maf. 1-13
Na. 2: Nehemia 8:1-12
Na. 3: Utendaji Mbalimbali Njiani Kwenda Yerusalemu (gt-SW sura 82 maf. 7-11)
Na. 4: Washiriki Wote wa Dini ya Kweli Ni Mashahidi Watendaji (rs-SW uku. 75 fu. 1)
Des. 27 Pitio la Kuandika. Kamilisha 2 Mambo ya Nyakati 1 hadi Nehemia 8