Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 15
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Samweli—Yaliyomo

      • Njama na uasi wa Absalomu (1-12)

      • Daudi akimbia kutoka Yerusalemu (13-30)

      • Ahithofeli ajiunga na Absalomu (31)

      • Hushai atumwa kuvuruga ushauri wa Ahithofeli (32-37)

2 Samweli 15:1

Marejeo

  • +1Sa 8:11; 1Fa 1:5; Met 11:2

2 Samweli 15:2

Marejeo

  • +Kum 25:7; Ru 4:1
  • +1Sa 8:20; 2Sa 8:15

2 Samweli 15:5

Marejeo

  • +Zb 10:9; 55:21; Met 26:25

2 Samweli 15:6

Marejeo

  • +Met 11:9

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    7/15/2012, uku. 13

  • Fahirishi ya Machapisho

    w12 7/15 13

2 Samweli 15:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “miaka 40.”

Marejeo

  • +2Sa 3:2

2 Samweli 15:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nitamwabudu; nitamtumikia.”

Marejeo

  • +2Sa 13:38; 14:23
  • +Law 22:21

2 Samweli 15:10

Marejeo

  • +2Sa 2:1; 5:1, 5; 1Nya 3:4

2 Samweli 15:12

Marejeo

  • +2Sa 16:23; 17:14; 23:8, 34
  • +Zb 41:9; 55:12, 13; Yoh 13:18
  • +Yos 15:20, 51
  • +Zb 3:1; Met 24:21

2 Samweli 15:14

Marejeo

  • +2Sa 19:9; Zb 3:utangulizi
  • +2Sa 12:11

2 Samweli 15:15

Marejeo

  • +Met 18:24

2 Samweli 15:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “jumba la mfalme.”

Marejeo

  • +2Sa 12:11; 16:21; 20:3

2 Samweli 15:17

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2009, uku. 27

  • Fahirishi ya Machapisho

    w09 5/15 27

2 Samweli 15:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “waliovuka upande wake.”

  • *

    Au “wakavuka mbele ya uso wa mfalme.”

Marejeo

  • +2Sa 8:18; 20:7; 1Fa 1:38; 1Nya 18:17
  • +Yos 13:2, 3
  • +1Sa 27:4; 1Nya 18:1

2 Samweli 15:19

Marejeo

  • +2Sa 18:2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2009, uku. 27

  • Fahirishi ya Machapisho

    w09 5/15 27

2 Samweli 15:20

Marejeo

  • +2Sa 2:5, 6; Zb 25:10; 57:3; 61:7; 89:14

2 Samweli 15:21

Marejeo

  • +Met 17:17; 18:24

2 Samweli 15:22

Marejeo

  • +2Sa 18:2

2 Samweli 15:23

Marejeo

  • +1Fa 2:36, 37; 2Nya 30:14; Yoh 18:1

2 Samweli 15:24

Marejeo

  • +2Sa 8:17; 20:25; 1Fa 1:8; 2:35; 1Nya 6:8
  • +Hes 8:19
  • +Kut 37:1; Law 16:2
  • +Hes 4:15; 7:9; 1Nya 15:2
  • +1Sa 22:20; 30:7

2 Samweli 15:25

Marejeo

  • +2Sa 6:17
  • +2Sa 7:2; Zb 26:8; 27:4

2 Samweli 15:27

Marejeo

  • +1Sa 9:9
  • +2Sa 17:17

2 Samweli 15:28

Marejeo

  • +2Sa 15:36; 17:16, 21

2 Samweli 15:30

Marejeo

  • +Mt 21:1; 24:3; Mdo 1:12

2 Samweli 15:31

Marejeo

  • +Zb 41:9; 55:12, 13; Yoh 13:18
  • +Zb 3:utangulizi
  • +Zb 3:7
  • +2Sa 16:23; 17:14

2 Samweli 15:32

Marejeo

  • +2Sa 16:16
  • +Yos 16:1, 2

2 Samweli 15:34

Marejeo

  • +2Sa 16:18, 19
  • +2Sa 17:7, 14

2 Samweli 15:35

Marejeo

  • +2Sa 17:15, 16

2 Samweli 15:36

Marejeo

  • +2Sa 18:19
  • +2Sa 17:17; 1Fa 1:42

2 Samweli 15:37

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “msiri wa.”

Marejeo

  • +2Sa 16:16; 1Nya 27:33

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Sam. 15:11Sa 8:11; 1Fa 1:5; Met 11:2
2 Sam. 15:2Kum 25:7; Ru 4:1
2 Sam. 15:21Sa 8:20; 2Sa 8:15
2 Sam. 15:5Zb 10:9; 55:21; Met 26:25
2 Sam. 15:6Met 11:9
2 Sam. 15:72Sa 3:2
2 Sam. 15:82Sa 13:38; 14:23
2 Sam. 15:8Law 22:21
2 Sam. 15:102Sa 2:1; 5:1, 5; 1Nya 3:4
2 Sam. 15:122Sa 16:23; 17:14; 23:8, 34
2 Sam. 15:12Zb 41:9; 55:12, 13; Yoh 13:18
2 Sam. 15:12Yos 15:20, 51
2 Sam. 15:12Zb 3:1; Met 24:21
2 Sam. 15:142Sa 19:9; Zb 3:utangulizi
2 Sam. 15:142Sa 12:11
2 Sam. 15:15Met 18:24
2 Sam. 15:162Sa 12:11; 16:21; 20:3
2 Sam. 15:182Sa 8:18; 20:7; 1Fa 1:38; 1Nya 18:17
2 Sam. 15:18Yos 13:2, 3
2 Sam. 15:181Sa 27:4; 1Nya 18:1
2 Sam. 15:192Sa 18:2
2 Sam. 15:202Sa 2:5, 6; Zb 25:10; 57:3; 61:7; 89:14
2 Sam. 15:21Met 17:17; 18:24
2 Sam. 15:222Sa 18:2
2 Sam. 15:231Fa 2:36, 37; 2Nya 30:14; Yoh 18:1
2 Sam. 15:242Sa 8:17; 20:25; 1Fa 1:8; 2:35; 1Nya 6:8
2 Sam. 15:24Hes 8:19
2 Sam. 15:24Kut 37:1; Law 16:2
2 Sam. 15:24Hes 4:15; 7:9; 1Nya 15:2
2 Sam. 15:241Sa 22:20; 30:7
2 Sam. 15:252Sa 6:17
2 Sam. 15:252Sa 7:2; Zb 26:8; 27:4
2 Sam. 15:271Sa 9:9
2 Sam. 15:272Sa 17:17
2 Sam. 15:282Sa 15:36; 17:16, 21
2 Sam. 15:30Mt 21:1; 24:3; Mdo 1:12
2 Sam. 15:31Zb 41:9; 55:12, 13; Yoh 13:18
2 Sam. 15:31Zb 3:utangulizi
2 Sam. 15:31Zb 3:7
2 Sam. 15:312Sa 16:23; 17:14
2 Sam. 15:322Sa 16:16
2 Sam. 15:32Yos 16:1, 2
2 Sam. 15:342Sa 16:18, 19
2 Sam. 15:342Sa 17:7, 14
2 Sam. 15:352Sa 17:15, 16
2 Sam. 15:362Sa 18:19
2 Sam. 15:362Sa 17:17; 1Fa 1:42
2 Sam. 15:372Sa 16:16; 1Nya 27:33
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
  • 31
  • 32
  • 33
  • 34
  • 35
  • 36
  • 37
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Samweli 15:1-37

Kitabu cha Pili cha Samweli

15 Baada ya mambo hayo yote, Absalomu akajipatia gari na farasi na watu 50 wa kukimbia mbele yake.+ 2 Absalomu alikuwa akiamka mapema na kusimama kando ya barabara iliyoelekea kwenye lango la jiji.+ Absalomu alikuwa akimwita na kumuuliza hivi mtu yeyote aliyekuwa na kesi ambayo ilipaswa kuamuliwa na mfalme:+ “Unatoka jiji gani?” naye alijibu: “Mimi mtumishi wako ninatoka katika mojawapo ya makabila ya Waisraeli.” 3 Kisha Absalomu alimwambia: “Madai yako ni ya kweli na ya haki, lakini hakuna yeyote kutoka kwa mfalme wa kusikiliza kesi yako.” 4 Absalomu alimwambia: “Laiti ningewekwa kuwa mwamuzi nchini! Kila mtu aliye na kesi au mashtaka angekuja kwangu, nami ningehakikisha kwamba anatendewa haki.”

5 Mtu alipomkaribia ili amwinamie, Absalomu alikuwa akinyoosha mkono wake na kumshika na kumbusu.+ 6 Absalomu alikuwa akiwafanyia hivyo Waisraeli wote waliokuwa wakienda kwa mfalme kuwasilisha mashtaka yao; basi Absalomu akaendelea kuiba mioyo ya Waisraeli.+

7 Mwishoni mwa miaka minne,* Absalomu akamwambia mfalme: “Tafadhali, acha niende Hebroni+ nikatimize nadhiri yangu niliyomwekea Yehova. 8 Kwa maana mimi mtumishi wako nilipokuwa nikiishi Geshuri+ huko Siria niliweka nadhiri hii takatifu:+ ‘Ikiwa Yehova atanirudisha Yerusalemu, nitamtolea Yehova dhabihu.’”* 9 Basi mfalme akamwambia: “Nenda kwa amani.” Absalomu akaondoka na kwenda Hebroni.

10 Sasa Absalomu akawatuma wapelelezi katika makabila yote ya Israeli, akawaambia: “Mara tu mtakaposikia sauti ya pembe, tangazeni hivi: ‘Absalomu amekuwa mfalme katika Hebroni!’”+ 11 Absalomu alikuwa ameenda huko na wanaume 200 kutoka Yerusalemu; alikuwa amewakaribisha, nao hawakushuku wala kujua kilichokuwa kikiendelea. 12 Isitoshe, Absalomu alipotoa dhabihu, aliwatuma watu wamwite Ahithofeli+ Mgiloni, mshauri wa Daudi,+ kutoka jiji la Gilo.+ Njama iliendelea kupamba moto, na idadi ya watu waliomuunga mkono Absalomu ikaendelea kuongezeka.+

13 Baada ya muda mpelelezi fulani akaja kwa Daudi na kumwambia: “Mioyo ya watu wa Israeli imegeuka kumfuata Absalomu.” 14 Mara moja Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu: “Tuondoke, tukimbie,+ kwa maana hakuna yeyote kati yetu atakayemkwepa Absalomu! Fanyeni haraka, asije akatufikia na kutuletea msiba na kuwaua watu wote jijini kwa upanga!”+ 15 Watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme: “Lolote ambalo wewe bwana wetu mfalme utaamua, sisi watumishi wako tuko tayari kulifanya.”+ 16 Basi mfalme akatoka pamoja na watu wote wa nyumbani mwake, lakini mfalme akawaacha masuria kumi+ ili watunze nyumba.* 17 Mfalme akaondoka pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakasimama Beth-merhaki.

18 Watumishi wake wote walioondoka pamoja naye* na Wakerethi wote na Wapelethi+ wote na Wagathi+ wote, watu 600 waliokuwa wamemfuata kutoka Gathi,+ wakapita mbele yake akiwachunguza.* 19 Ndipo mfalme akamwambia Itai+ Mgathi: “Kwa nini wewe pia uende pamoja nasi? Rudi ukaishi na mfalme mpya, kwa sababu wewe ni mgeni, na pia ulifukuzwa kutoka katika nchi yako. 20 Ulikuja jana tu, kwa nini leo nikufanye utange-tange pamoja nasi, uende wakati ninapohitaji kwenda na mahali popote ninapoenda? Rudi pamoja na ndugu zako, na Yehova akutendee kwa upendo mshikamanifu na kwa uaminifu!”+ 21 Lakini Itai akamwambia mfalme: “Kwa hakika kama Yehova anavyoishi na kwa hakika kama bwana wangu mfalme anavyoishi, mahali popote utakapokuwa wewe bwana wangu mfalme, ukiwa hai au ukiwa umekufa, mimi mtumishi wako nitakuwa mahali hapo!”+ 22 Ndipo Daudi akamwambia Itai:+ “Pita uvuke.” Basi Itai Mgathi akavuka, pamoja na watu wake wote na watoto wake.

23 Watu wote nchini walikuwa wakilia kwa sauti kubwa watu hao wote walipokuwa wakivuka ng’ambo ile nyingine, naye mfalme alikuwa amesimama kando ya Bonde la Kidroni;+ watu wote walivuka na kufuata barabara inayoelekea nyikani. 24 Sadoki+ pia alikuwa mahali hapo pamoja na Walawi wote+ waliobeba sanduku+ la agano la Mungu wa kweli;+ nao wakaliweka chini Sanduku la Mungu wa kweli; Abiathari+ pia alikuwepo watu wote walipovuka kutoka jijini. 25 Lakini mfalme akamwambia Sadoki: “Lirudishe jijini Sanduku la Mungu wa kweli.+ Nikipata kibali machoni pa Yehova, atanirudisha na kuniruhusu kuliona na kuona mahali linapokaa.+ 26 Lakini akisema, ‘Sipendezwi nawe,’ basi na anitendee jambo lolote analoona ni jema.” 27 Mfalme akamwambia kuhani Sadoki: “Je, wewe si mwonaji?+ Rudi jijini kwa amani, na pia wachukue wana wenu wawili, Ahimaazi mwana wako na Yonathani+ mwana wa Abiathari. 28 Nitangojea kando ya vivuko vya nyikani mpaka nitakapopata habari kutoka kwenu.”+ 29 Basi Sadoki na Abiathari wakalirudisha Sanduku la Mungu wa kweli Yerusalemu, nao wakabaki huko.

30 Daudi alipanda Mlima wa Mizeituni+ huku akilia; alikuwa amefunika kichwa chake, na alikuwa miguu mitupu. Pia watu wote waliokuwa pamoja naye walifunika vichwa vyao, nao walikuwa wakilia huku wakipanda. 31 Kisha Daudi akaambiwa hivi: “Ahithofeli ni miongoni mwa watu wanaopanga njama+ pamoja na Absalomu.”+ Daudi akasema: “Ee Yehova,+ tafadhali badili ushauri wa Ahithofeli uwe upumbavu!”+

32 Daudi alipofika kwenye kilele, mahali ambapo watu walizoea kumwinamia Mungu, Hushai+ Mwarki+ alikuwa mahali hapo ili kumpokea, joho lake lilikuwa limeraruka na alikuwa na mavumbi kichwani. 33 Hata hivyo, Daudi akamwambia: “Ukivuka kwenda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu. 34 Lakini ukirudi jijini nawe umwambie Absalomu, ‘Mimi ni mtumishi wako, Ee mfalme. Nilikuwa mtumishi wa baba yako zamani, lakini sasa mimi ni mtumishi wako,’+ ndipo utakaponisaidia kuvuruga ushauri wa Ahithofeli.+ 35 Kuhani Sadoki na Abiathari wako huko pamoja nawe. Utamwambia kuhani Sadoki na Abiathari mambo yote utakayosikia katika nyumba ya mfalme.+ 36 Wana wao wawili, Ahimaazi+ mwana wa Sadoki na Yonathani+ mwana wa Abiathari wako huko pamoja nao, nanyi mtawatumia wana hao kuniletea habari zote mtakazosikia.” 37 Basi Hushai rafiki ya*+ Daudi akaingia jijini Absalomu alipokuwa akiingia Yerusalemu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki