34 Mwishowe akaenda juu, akajilaza juu ya yule mtoto,+ akakitia kinywa chake juu ya kinywa chake, na macho yake juu ya macho yake, na mikono yake juu ya mikono yake, akaendelea kuinama juu yake, na hatua kwa hatua mwili wa mtoto ukawa na joto.
21 Na ikawa kwamba walipokuwa wakimzika mtu, tazama, wakaona kikundi cha waporaji. Wakamtupa mara moja yule mtu ndani ya kaburi la Elisha, wakaenda zao. Mtu yule alipoigusa mifupa ya Elisha, akawa hai+ mara moja na kusimama kwa miguu+ yake.
44 Huyo mtu aliyekuwa mfu akatoka miguu na mikono yake ikiwa imefungwa vitambaa,+ na uso wake ulikuwa umefungwa-fungwa kwa kitambaa. Yesu akawaambia: “Mfungueni, mmwache aende.”