Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 21
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Samweli—Yaliyomo

      • Nyumba ya Sauli yalipizwa kisasi kwa ajili ya Wagibeoni (1-14)

      • Vita dhidi ya Wafilisti (15-22)

2 Samweli 21:1

Marejeo

  • +Law 26:18, 20
  • +Mwa 9:6; Kut 20:13; Hes 35:30, 33

2 Samweli 21:2

Marejeo

  • +Yos 9:3, 27
  • +Mwa 10:15, 16
  • +Yos 9:15

2 Samweli 21:4

Marejeo

  • +Hes 35:31

2 Samweli 21:5

Marejeo

  • +2Sa 21:1

2 Samweli 21:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “tutawaanika,” yaani, mikono na miguu yao ikiwa imevunjwa.

Marejeo

  • +Hes 25:4; Kum 21:22
  • +1Sa 10:26
  • +1Sa 9:17

2 Samweli 21:7

Marejeo

  • +2Sa 4:4; 9:10; 19:24
  • +1Sa 18:3; 20:42

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    3/2022, uku. 13

2 Samweli 21:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “Merabu.”

Marejeo

  • +2Sa 3:7
  • +1Sa 18:20; 25:44; 2Sa 3:14; 6:23
  • +1Sa 18:19

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    3/2022, uku. 13

    The Watchtower,

    5/15/2005, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 5/15 19

2 Samweli 21:9

Marejeo

  • +Hes 35:31; Kum 19:21

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    3/2022, uku. 13

2 Samweli 21:10

Marejeo

  • +2Sa 3:7

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    The Watchtower,

    5/15/2005, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 5/15 19

2 Samweli 21:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “wamiliki wa mashamba.”

Marejeo

  • +2Sa 2:5
  • +1Sa 28:4; 31:1, 11, 12; 2Sa 1:6; 1Nya 10:8

2 Samweli 21:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “wameanikwa.”

Marejeo

  • +2Sa 21:9

2 Samweli 21:14

Marejeo

  • +Yos 18:28
  • +1Sa 9:1; 10:11
  • +Yos 7:24-26; 2Sa 24:25

2 Samweli 21:15

Marejeo

  • +2Sa 5:17, 22

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2013, kur. 30-31

2 Samweli 21:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Karibu kilogramu 3.42. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +Kum 2:11
  • +1Sa 17:4, 7; 1Nya 11:23

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2013, kur. 30-31

2 Samweli 21:17

Marejeo

  • +2Sa 23:18, 19
  • +2Sa 22:19
  • +2Sa 18:3
  • +1Fa 11:36; 15:4; 2Fa 8:19

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2013, kur. 30-31

2 Samweli 21:18

Marejeo

  • +1Nya 20:4
  • +1Nya 11:26, 29; 27:1, 11
  • +Mwa 14:5

2 Samweli 21:19

Marejeo

  • +1Nya 20:5
  • +1Sa 17:4, 7

2 Samweli 21:20

Marejeo

  • +1Nya 20:6-8

2 Samweli 21:21

Marejeo

  • +1Sa 17:10, 45; 2Fa 19:22
  • +1Sa 16:9; 17:13; 1Nya 2:13

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/1989, uku. 28

2 Samweli 21:22

Marejeo

  • +Zb 60:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/1989, kur. 20, 28

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Sam. 21:1Law 26:18, 20
2 Sam. 21:1Mwa 9:6; Kut 20:13; Hes 35:30, 33
2 Sam. 21:2Yos 9:3, 27
2 Sam. 21:2Mwa 10:15, 16
2 Sam. 21:2Yos 9:15
2 Sam. 21:4Hes 35:31
2 Sam. 21:52Sa 21:1
2 Sam. 21:6Hes 25:4; Kum 21:22
2 Sam. 21:61Sa 10:26
2 Sam. 21:61Sa 9:17
2 Sam. 21:72Sa 4:4; 9:10; 19:24
2 Sam. 21:71Sa 18:3; 20:42
2 Sam. 21:82Sa 3:7
2 Sam. 21:81Sa 18:20; 25:44; 2Sa 3:14; 6:23
2 Sam. 21:81Sa 18:19
2 Sam. 21:9Hes 35:31; Kum 19:21
2 Sam. 21:102Sa 3:7
2 Sam. 21:122Sa 2:5
2 Sam. 21:121Sa 28:4; 31:1, 11, 12; 2Sa 1:6; 1Nya 10:8
2 Sam. 21:132Sa 21:9
2 Sam. 21:14Yos 18:28
2 Sam. 21:141Sa 9:1; 10:11
2 Sam. 21:14Yos 7:24-26; 2Sa 24:25
2 Sam. 21:152Sa 5:17, 22
2 Sam. 21:16Kum 2:11
2 Sam. 21:161Sa 17:4, 7; 1Nya 11:23
2 Sam. 21:172Sa 23:18, 19
2 Sam. 21:172Sa 22:19
2 Sam. 21:172Sa 18:3
2 Sam. 21:171Fa 11:36; 15:4; 2Fa 8:19
2 Sam. 21:181Nya 20:4
2 Sam. 21:181Nya 11:26, 29; 27:1, 11
2 Sam. 21:18Mwa 14:5
2 Sam. 21:191Nya 20:5
2 Sam. 21:191Sa 17:4, 7
2 Sam. 21:201Nya 20:6-8
2 Sam. 21:211Sa 17:10, 45; 2Fa 19:22
2 Sam. 21:211Sa 16:9; 17:13; 1Nya 2:13
2 Sam. 21:22Zb 60:12
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Samweli 21:1-22

Kitabu cha Pili cha Samweli

21 Basi katika siku za Daudi kulikuwa na njaa kali+ kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akamwomba Yehova ushauri, kisha Yehova akasema: “Sauli na nyumba yake wana hatia ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”+ 2 Basi mfalme akawaita Wagibeoni+ na kuongea nao. (Sasa, Wagibeoni hawakuwa Waisraeli bali walikuwa Waamori+ waliokuwa wamebaki, na Waisraeli walikuwa wameapa kwamba hawatawaua,+ lakini Sauli akichochewa na bidii yake kwa ajili ya watu wa Israeli na Yuda alitaka kuwaangamiza.) 3 Daudi akawauliza Wagibeoni: “Niwafanyie nini, nami nitawalipaje kwa ajili ya mliyotendewa, ili muubariki urithi wa Yehova?” 4 Wagibeoni wakamwambia: “Jambo ambalo Sauli na nyumba yake walitutendea si suala la fedha wala dhahabu;+ wala hatuwezi kumuua mtu yeyote katika Israeli.” Daudi akasema: “Nitawafanyia jambo lolote mtakalosema.” 5 Wakamwambia mfalme: “Mtu aliyetuua na kupanga njama ya kutuangamiza ili tusiishi katika eneo lolote la Israeli+— 6 tupatieni wanawe saba. Tutatundika maiti zao*+ mbele za Yehova katika jiji la Gibea+ la Sauli, aliyechaguliwa na Yehova.”+ Ndipo mfalme akasema: “Nitawapa.”

7 Hata hivyo, mfalme akamhurumia Mefiboshethi,+ mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa sababu ya kiapo ambacho Daudi na Yonathani mwana wa Sauli walikuwa wameapiana mbele za Yehova.+ 8 Basi mfalme akamchukua Armoni na Mefiboshethi, wana wawili ambao Rispa+ binti ya Aya alimzalia Sauli, na wana watano ambao Mikali*+ binti ya Sauli alimzalia Adrieli+ mwana wa Barzilai, Mmeholathi. 9 Daudi akawapa Wagibeoni wana hao, nao wakatundika maiti zao mlimani mbele za Yehova.+ Wana wote saba walikufa pamoja; waliuawa siku za kwanza za mavuno, mwanzoni mwa mavuno ya shayiri. 10 Kisha Rispa+ binti ya Aya akachukua gunia na kulitandika mwambani tangu mwanzo wa mavuno mpaka mvua kutoka mbinguni iliponyeshea maiti hizo; hakuruhusu ndege wa angani watue juu ya maiti hizo wakati wa mchana wala wanyama wa mwituni wazikaribie wakati wa usiku.

11 Daudi akaambiwa mambo ambayo Rispa binti ya Aya suria wa Sauli alikuwa amefanya. 12 Kwa hiyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwana wake kutoka kwa viongozi* wa Yabesh-gileadi,+ waliokuwa wameiba mifupa hiyo katika uwanja wa jiji la Beth-shani, ambako Wafilisti walikuwa wamewatundika siku ambayo walimuua Sauli juu ya Gilboa.+ 13 Akachukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwana wake kutoka mlimani, pia wakaikusanya mifupa ya wanaume waliokuwa wameuawa.*+ 14 Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwana wake katika nchi ya Benjamini kule Sela+ katika kaburi la Kishi+ baba yake. Baada ya kufanya kila jambo ambalo mfalme alikuwa ameamuru, Mungu akasikiliza maombi yao ya kumsihi kuhusu nchi.+

15 Vita vikatokea tena kati ya Wafilisti na Waisraeli.+ Kwa hiyo, Daudi na watumishi wake wakashuka kwenda kupigana na Wafilisti, lakini Daudi akachoka. 16 Mzao wa Warefaimu+ aliyeitwa Ishbi-benobu, aliyekuwa na mkuki wa shaba wenye uzito wa shekeli 300*+ na aliyejihami kwa upanga mpya, alikusudia kumuua Daudi. 17 Mara moja Abishai+ mwana wa Seruya akaja kumsaidia,+ akampiga Mfilisti huyo na kumuua. Wakati huo wanaume wa Daudi wakamwapia hivi: “Usiende tena vitani pamoja nasi!+ Usiizime taa ya Israeli!”+

18 Baada ya hayo, wakapigana tena na Wafilisti+ kule Gobu. Wakati huo Sibekai+ Mhusha alimuua Safu, aliyekuwa mzao wa Warefaimu.+

19 Wakapigana tena na Wafilisti+ huko Gobu, na Elhanani mwana wa Yaare-oregimu Mbethlehemu akamuua Goliathi Mgathi, aliyekuwa na mkuki wenye mpini kama mti wa wafumaji wa nguo.+

20 Vita vikatokea tena huko Gathi, ambako kulikuwa na mwanamume mkubwa isivyo kawaida, mwenye vidole 6 katika kila mkono na vidole 6 katika kila mguu, jumla ya vidole 24; naye pia alikuwa mzao wa Warefaimu.+ 21 Aliendelea kuwadhihaki Waisraeli.+ Basi Yonathani mwana wa Shimei,+ ndugu ya Daudi, akamuua.

22 Watu hao wanne walikuwa wazao wa Warefaimu huko Gathi, na Daudi na watumishi wake ndio waliowaua.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki