Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 28
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Sauli amtembelea mtu anayewasiliana na roho waovu kule En-dori (1-25)

1 Samweli 28:1

Marejeo

  • +1Sa 14:52
  • +1Sa 27:12; 29:3

1 Samweli 28:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kuwa mlinzi wa kichwa changu siku zote.”

Marejeo

  • +1Sa 29:2

1 Samweli 28:3

Marejeo

  • +1Sa 25:1
  • +Kut 22:18; Law 19:31; 20:6, 27; Kum 18:10, 11; Ufu 21:8

1 Samweli 28:4

Marejeo

  • +Yos 19:17, 18; 2Fa 4:8
  • +1Sa 31:1; 2Sa 1:21; 21:12

1 Samweli 28:5

Marejeo

  • +1Sa 28:20

1 Samweli 28:6

Marejeo

  • +1Sa 14:37
  • +Kut 28:30; Hes 27:21

1 Samweli 28:7

Marejeo

  • +Kut 22:18; Law 19:31; 20:6; 1Sa 15:23; 28:3
  • +Yos 17:11

1 Samweli 28:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nibashirie.”

Marejeo

  • +Kum 18:10, 11; 1Nya 10:13

1 Samweli 28:9

Marejeo

  • +1Sa 28:3
  • +Kut 22:18; Law 20:27

1 Samweli 28:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mtu aliyeonekana kama Samweli.”

Marejeo

  • +1Sa 28:3

1 Samweli 28:14

Marejeo

  • +1Sa 15:27

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (2010),

    1/1/2010, uku. 20

    1/15/1988, uku. 3

    Kutoa Sababu, kur. 140-141

  • Fahirishi ya Machapisho

    w10 1/1 20; rs 140-141

1 Samweli 28:15

Marejeo

  • +1Sa 28:6
  • +Law 19:31

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Kuishi Milele, kur. 91-92

1 Samweli 28:16

Marejeo

  • +1Sa 15:23; 16:14

1 Samweli 28:17

Marejeo

  • +1Sa 13:14; 15:28; 16:13; 24:20

1 Samweli 28:18

Marejeo

  • +1Sa 15:9; 1Nya 10:13

1 Samweli 28:19

Marejeo

  • +1Sa 28:1; 31:1
  • +1Sa 31:5
  • +1Sa 31:2; 2Sa 2:8
  • +1Sa 31:7

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/1988, uku. 3

1 Samweli 28:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nimetia nafsi yangu mikononi mwangu.”

Marejeo

  • +Law 20:27

1 Samweli 28:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “akamtoa dhabihu.”

1 Samweli 28:25

Marejeo

  • +1Sa 28:8

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 28:11Sa 14:52
1 Sam. 28:11Sa 27:12; 29:3
1 Sam. 28:21Sa 29:2
1 Sam. 28:31Sa 25:1
1 Sam. 28:3Kut 22:18; Law 19:31; 20:6, 27; Kum 18:10, 11; Ufu 21:8
1 Sam. 28:4Yos 19:17, 18; 2Fa 4:8
1 Sam. 28:41Sa 31:1; 2Sa 1:21; 21:12
1 Sam. 28:51Sa 28:20
1 Sam. 28:61Sa 14:37
1 Sam. 28:6Kut 28:30; Hes 27:21
1 Sam. 28:7Kut 22:18; Law 19:31; 20:6; 1Sa 15:23; 28:3
1 Sam. 28:7Yos 17:11
1 Sam. 28:8Kum 18:10, 11; 1Nya 10:13
1 Sam. 28:91Sa 28:3
1 Sam. 28:9Kut 22:18; Law 20:27
1 Sam. 28:121Sa 28:3
1 Sam. 28:141Sa 15:27
1 Sam. 28:151Sa 28:6
1 Sam. 28:15Law 19:31
1 Sam. 28:161Sa 15:23; 16:14
1 Sam. 28:171Sa 13:14; 15:28; 16:13; 24:20
1 Sam. 28:181Sa 15:9; 1Nya 10:13
1 Sam. 28:191Sa 28:1; 31:1
1 Sam. 28:191Sa 31:5
1 Sam. 28:191Sa 31:2; 2Sa 2:8
1 Sam. 28:191Sa 31:7
1 Sam. 28:21Law 20:27
1 Sam. 28:251Sa 28:8
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 28:1-25

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

28 Siku hizo Wafilisti walikusanya majeshi yao kwenda kupigana vita na Waisraeli.+ Basi Akishi akamwambia Daudi: “Bila shaka unajua kwamba wewe na wanaume wako mtaenda pamoja nami vitani.”+ 2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Akishi: “Kwa hakika unajua jambo ambalo mimi mtumishi wako nitafanya.” Akishi akamwambia Daudi: “Ndiyo sababu nitakuweka kuwa mlinzi wangu wa kudumu.”*+

3 Wakati huo Samweli alikuwa amekufa, na Waisraeli wote walikuwa wamemwombolezea na kumzika katika jiji lake mwenyewe la Rama.+ Naye Sauli alikuwa amewaondoa nchini watu wanaowasiliana na roho na pia wabashiri.+

4 Wafilisti wakakusanyika na kwenda kupiga kambi Shunemu.+ Basi Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga kambi Gilboa.+ 5 Sauli alipoona kambi ya Wafilisti, akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana.+ 6 Ingawa Sauli alikuwa akimwomba Yehova ushauri,+ Yehova hakumjibu kamwe, iwe ni katika ndoto au kwa Urimu+ au kupitia manabii. 7 Hatimaye Sauli akawaambia watumishi wake: “Nitafutieni mwanamke anayewasiliana na roho,+ nitaenda kwake kumwomba ushauri.” Watumishi wake wakamwambia: “Tazama! Kuna mwanamke anayewasiliana na roho kule En-dori.”+

8 Kwa hiyo Sauli akaficha sura yake, akavaa mavazi mengine na kwenda kwa mwanamke huyo usiku akiwa na wanaume wake wawili. Akasema: “Tafadhali, nifanyie uaguzi* kwa kuwasiliana na roho,+ nipandishie yule nitakayekutajia.” 9 Hata hivyo, mwanamke huyo akamwambia: “Unajua vizuri mambo ambayo Sauli alifanya, jinsi alivyowaondoa nchini watu wanaowasiliana na roho na pia wabashiri.+ Kwa nini basi unajaribu kunitega ili niuawe?”+ 10 Ndipo Sauli akamwapia kwa jina la Yehova, akisema: “Kwa hakika kama Yehova anavyoishi, hutakuwa na hatia yoyote kuhusu jambo hili!” 11 Basi mwanamke huyo akamuuliza: “Nikupandishie nani?” Akajibu: “Nipandishie Samweli.” 12 Mwanamke huyo alipomwona “Samweli,”*+ akapiga kelele kwa sauti yake yote na kumwambia Sauli: “Kwa nini ulinidanganya? Wewe ni Sauli!” 13 Mfalme akamwambia: “Usiogope, lakini unaona nini?” Mwanamke huyo akamjibu Sauli: “Ninaona mtu fulani kama mungu akipanda kutoka duniani.” 14 Mara moja Sauli akamuuliza mwanamke huyo: “Yukoje?” akamwambia: “Ni mwanamume mzee anayepanda, amevaa joho lisilo na mikono.”+ Ndipo Sauli akatambua kwamba ni “Samweli,” naye akainama chini kifudifudi na kusujudu.

15 Kisha “Samweli” akamuuliza Sauli: “Kwa nini umenisumbua kwa kufanya nipandishwe?” Sauli akamjibu: “Niko katika taabu kubwa. Wafilisti wanapigana nami, na Mungu ameniacha, hanijibu tena, iwe ni kupitia manabii au katika ndoto;+ ndiyo sababu nimekuita uniambie ninalopaswa kufanya.”+

16 “Samweli” akamuuliza: “Kwa nini unaniomba ushauri wakati ambapo Yehova amekuacha+ na kuwa adui yako? 17 Yehova atajifanyia mwenyewe yale aliyotabiri kupitia mimi: Yehova ataurarua ufalme kutoka mikononi mwako na kumpa mwenzako, Daudi.+ 18 Kwa sababu hukuitii sauti ya Yehova, nawe hukutekeleza hasira yake kali dhidi ya Waamaleki,+ ndiyo sababu Yehova anakutendea mambo haya leo. 19 Pia, Yehova atakutia wewe pamoja na Waisraeli mikononi mwa Wafilisti,+ na kesho wewe+ na wana wako+ mtakuwa pamoja nami. Yehova atalitia pia jeshi la Israeli mikononi mwa Wafilisti.”+

20 Papo hapo Sauli akaanguka chini akiwa amenyooka mwili mzima naye akaogopa sana kwa sababu ya maneno ya “Samweli.” Nguvu zikamwishia, kwa sababu hakuwa amekula chakula mchana wote na usiku kucha. 21 Mwanamke huyo alipomkaribia Sauli na kuona kwamba ana wasiwasi mwingi, akamwambia: “Mimi kijakazi wako nimetii jambo ulilosema, na nimehatarisha uhai wangu*+ kwa kufanya uliloniambia nifanye. 22 Sasa, tafadhali, sikiliza maneno ninayotaka kukwambia mimi mtumishi wako. Acha nikuandalie kipande cha mkate, ule ili upate nguvu za kuendelea na safari.” 23 Lakini akakataa na kusema: “Sitakula.” Hata hivyo, watumishi wake na pia mwanamke huyo wakaendelea kumsihi ale. Mwishowe akawasikiliza, akainuka kutoka ardhini na kuketi kitandani. 24 Mwanamke huyo alikuwa na ndama aliyenona nyumbani mwake, basi akamchinja* haraka, akachukua unga, akaukanda na kuoka mikate isiyo na chachu. 25 Akamwandalia Sauli na watumishi wake, nao wakala. Kisha wakaondoka na kwenda zao usiku huo.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki