Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 15
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Madeni yafutwa kila mwaka wa saba (1-6)

      • Kuwasaidia maskini (7-11)

      • Kuwaachilia huru watumwa kila mwaka wa saba (12-18)

        • Kutoboa sikio la mtumwa kwa msumari (16, 17)

      • Wazaliwa wa kwanza wa wanyama watakaswa (19-23)

Kumbukumbu la Torati 15:1

Marejeo

  • +Law 25:2

Kumbukumbu la Torati 15:2

Marejeo

  • +Kum 31:10

Kumbukumbu la Torati 15:3

Marejeo

  • +Kut 12:43; Kum 14:21; 23:20

Kumbukumbu la Torati 15:4

Marejeo

  • +Kum 28:8

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 122

Kumbukumbu la Torati 15:5

Marejeo

  • +Yos 1:7, 8; Isa 1:19

Kumbukumbu la Torati 15:6

Marejeo

  • +Kum 28:12
  • +Kum 28:13; 1Fa 4:24, 25

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, kur. 122-123

Kumbukumbu la Torati 15:7

Marejeo

  • +Met 21:13; Yak 2:15, 16; 1Yo 3:17

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (2010),

    9/15/2010, uku. 8

  • Fahirishi ya Machapisho

    w10 9/15 8

Kumbukumbu la Torati 15:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kumkopesha kwa rehani.”

Marejeo

  • +Law 25:35; Met 19:17; Mt 5:42; Lu 6:34, 35; Gal 2:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (2010),

    9/15/2010, uku. 8

  • Fahirishi ya Machapisho

    w10 9/15 8

Kumbukumbu la Torati 15:9

Marejeo

  • +Kum 15:1
  • +Kut 22:22, 23; Kum 24:14, 15; Met 21:13

Kumbukumbu la Torati 15:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “moyo wenu haupaswi.”

Marejeo

  • +Mdo 20:35; 2Ko 9:7; 1Ti 6:18; Ebr 13:16
  • +Kum 24:19; Zb 41:1

Kumbukumbu la Torati 15:11

Marejeo

  • +Mt 26:11
  • +Met 3:27; Mt 5:42; Lu 12:33

Kumbukumbu la Torati 15:12

Marejeo

  • +Kut 21:2; Law 25:39

Kumbukumbu la Torati 15:15

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/2014, uku. 19

Kumbukumbu la Torati 15:16

Marejeo

  • +Kut 21:5, 6

Kumbukumbu la Torati 15:19

Marejeo

  • +Kut 13:2; 22:30; Hes 3:13; 18:15, 17

Kumbukumbu la Torati 15:20

Marejeo

  • +Kum 12:5, 6; 14:23; 16:11

Kumbukumbu la Torati 15:21

Marejeo

  • +Law 22:20; Kum 17:1; Mal 1:8; Ebr 9:14

Kumbukumbu la Torati 15:22

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “malango.”

Marejeo

  • +Kum 12:15; 14:4, 5

Kumbukumbu la Torati 15:23

Marejeo

  • +Mwa 9:4; Law 7:26; Mdo 15:20, 29
  • +Law 17:10, 13; Kum 12:16

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    10/15/2000, kur. 30-31

  • Fahirishi ya Machapisho

    w00 10/15 30-31

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 15:1Law 25:2
Kum. 15:2Kum 31:10
Kum. 15:3Kut 12:43; Kum 14:21; 23:20
Kum. 15:4Kum 28:8
Kum. 15:5Yos 1:7, 8; Isa 1:19
Kum. 15:6Kum 28:12
Kum. 15:6Kum 28:13; 1Fa 4:24, 25
Kum. 15:7Met 21:13; Yak 2:15, 16; 1Yo 3:17
Kum. 15:8Law 25:35; Met 19:17; Mt 5:42; Lu 6:34, 35; Gal 2:10
Kum. 15:9Kum 15:1
Kum. 15:9Kut 22:22, 23; Kum 24:14, 15; Met 21:13
Kum. 15:10Mdo 20:35; 2Ko 9:7; 1Ti 6:18; Ebr 13:16
Kum. 15:10Kum 24:19; Zb 41:1
Kum. 15:11Mt 26:11
Kum. 15:11Met 3:27; Mt 5:42; Lu 12:33
Kum. 15:12Kut 21:2; Law 25:39
Kum. 15:16Kut 21:5, 6
Kum. 15:19Kut 13:2; 22:30; Hes 3:13; 18:15, 17
Kum. 15:20Kum 12:5, 6; 14:23; 16:11
Kum. 15:21Law 22:20; Kum 17:1; Mal 1:8; Ebr 9:14
Kum. 15:22Kum 12:15; 14:4, 5
Kum. 15:23Mwa 9:4; Law 7:26; Mdo 15:20, 29
Kum. 15:23Law 17:10, 13; Kum 12:16
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 15:1-23

Kumbukumbu la Torati

15 “Mwishoni mwa kila miaka saba mnapaswa kufuta madeni.+ 2 Hivi ndivyo mtakavyoyafuta: Kila mtu aliyemkopesha jirani yake atafuta deni hilo. Hapaswi kudai malipo kutoka kwa jirani au ndugu yake, kwa maana yatatangazwa yamefutwa kwa agizo la Yehova.+ 3 Mnaweza kudai malipo kutoka kwa mgeni,+ lakini mnapaswa kufuta deni lolote la ndugu yenu. 4 Hata hivyo, hakuna yeyote kati yenu anayepaswa kuwa maskini, kwa sababu hakika Yehova atawabariki+ katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa mwimiliki kama urithi, 5 lakini ikiwa tu mtatii kabisa sauti ya Yehova Mungu wenu na kushika kwa uangalifu amri yote hii ninayowapa leo.+ 6 Kwa maana Yehova Mungu wenu atawabariki kama alivyowaahidi, nanyi mtayakopesha mataifa mengi, lakini ninyi hamtahitaji kukopa;+ nanyi mtatawala mataifa mengi, lakini hayatawatawala.+

7 “Ikiwa mmoja wa ndugu zenu atakuwa maskini miongoni mwenu katika mojawapo ya majiji yaliyo katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa, msiifanye mioyo yenu iwe migumu au kumfumbia mkono ndugu yenu maskini.+ 8 Kwa maana mnapaswa kumfumbulia mkono wenu kwa ukarimu+ na kufanya yote mwezayo kumkopesha* chochote anachohitaji au alichopungukiwa. 9 Jihadharini wazo hili ovu lisiingie mioyoni mwenu: ‘Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni, umekaribia,’+ na hivyo mkatae kumtendea kwa ukarimu ndugu yenu aliye maskini na kukosa kumpa chochote. Akimlilia Yehova kuwahusu ninyi, mtakuwa mmetenda dhambi.+ 10 Mnapaswa kumpa kwa ukarimu,+ nanyi hampaswi* kumpa huku mkinung’unika, kwa sababu hiyo Yehova Mungu wenu atabariki kila kazi na kila jambo mnalofanya.+ 11 Kwa maana sikuzote kutakuwa na maskini nchini.+ Ndiyo sababu ninawaamuru hivi: ‘Mnapaswa kumfumbulia mkono wenu kwa ukarimu ndugu yenu anayeteseka na maskini katika nchi yenu.’+

12 “Ikiwa uliuziwa ndugu yako, mwanamume au mwanamke Mwebrania, naye amekutumikia kwa miaka sita, basi katika mwaka wa saba unapaswa kumwachilia huru.+ 13 Na ikiwa utamwachilia huru, usimwache aende mikono mitupu. 14 Mpe kwa ukarimu kitu fulani kutoka katika mifugo yako, uwanja wako wa kupuria, na shinikizo lako la mafuta na divai. Unapaswa kumpa kama vile ambavyo Yehova Mungu wako amekubariki. 15 Kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri na Yehova Mungu wako akakukomboa. Ndiyo sababu leo ninakuamuru ufanye hivyo.

16 “Lakini akikuambia, ‘Sitakuacha!’ kwa sababu anakupenda wewe na familia yako, kwa maana amefurahia kuwa pamoja nawe,+ 17 utachukua msumari na kutoboa sikio lake kwa msumari huo mpaka upenye mlangoni, naye atakuwa mtumwa wako daima. Utamfanyia kijakazi wako vivyo hivyo. 18 Usione vigumu kumwachilia huru, naye aondoke, kwa sababu thamani ya utumishi wake kwa miaka sita aliyokutumikia ni mara mbili ya thamani ya utumishi wa mfanyakazi aliyeajiriwa, na Yehova Mungu wako amekubariki katika kila jambo ambalo lilifanywa.

19 “Unapaswa kumtakasa kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa ng’ombe wako na kondoo wako kwa ajili ya Yehova Mungu wako.+ Usimtumie mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe dume wako kufanya kazi yoyote wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kondoo wako. 20 Wewe na familia yako mnapaswa kumla mbele za Yehova Mungu wenu mwaka baada ya mwaka mahali ambapo Yehova Mungu wenu atachagua.+ 21 Lakini ikiwa ana kasoro, yaani, ni mlemavu, ni kipofu, au ana kasoro nyingine kubwa, usimtoe dhabihu kwa Yehova Mungu wako.+ 22 Mnapaswa kumla ndani ya majiji* yenu, mtu asiye safi na aliye safi watamla, kama mnavyokula swala au paa.+ 23 Lakini hampaswi kula damu yake;+ mtaimwaga ardhini kama maji.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki