Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1994
MAAGIZO
Wakati wa 1994, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango ya kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli [uw-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi [gt-SW], na “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation [*td] au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW] vitakuwa msingi wa migawo.
Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha, kisha itaendelea hivi:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Hotuba hii yapasa ishughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma mwenye kustahili, na itategemea habari katika kitabu Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika kichapo hicho. Lengo lapasa kuwa si kufanya mwenezo wa habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, kwa kukazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa kinapasa kitumiwe. Wote wanatiwa moyo wafanye matayarisho ya kimbele kwa uangalifu ili wanufaike kikamili na habari hiyo.
Ndugu waliogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa lazima, au ikiwa msemaji ameomba shauri hilo kimbele.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Hii yapasa ishughulikiwe na mwangalizi wa shule au mzee mwingine au na mtumishi wa huduma atakayeonyesha kwa matokeo jinsi habari hiyo inavyohusu mahitaji ya mahali hapo. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Tumia sekunde 30 hadi 60 tu kutoa mwono wa ujumla. Lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Hii ni kusoma Biblia juu ya habari iliyotolewa kuwa mgawo itakayotolewa na ndugu. Itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na jinsi kanuni zinavyohusu, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo yapasa hasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi anaweza kutaja mstari mahali ambapo usomaji waendelea.
HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa akina dada. Vichwa vya hotuba hii vitategemea kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Mwanafunzi aliyegawiwa apaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hii, mwanafunzi aweza kuwa ameketi au amesimama. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi wa ziada wanaweza kutumiwa. Ni afadhali vikao vihusishe utumishi wa shambani au utoaji wa ushahidi wa vivi hivi. Anayetoa hotuba hii aweza ama kuanzisha mazungumzo ili kuweka kikao au kuacha msaidizi (wasaidizi) wake afanye hivyo. Habari wala si kikao ndiyo ya kufikiriwa kwanza. Mwanafunzi apaswa kutumia kichwa kilichoonyeshwa.
HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Itategemea Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia. Inapogawiwa ndugu, yapaswa iwe hotuba inayotolewa kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi ndugu huyo atayarishe hotuba yake akiwa anafikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Hata hivyo, endapo habari hiyo yataka kikao cha aina nyingine ya wasikilizaji chenye kutumika na kinachofaa, ndugu huyo aweza kuchagua kusitawisha hotuba yake kwa njia hiyo. Mwanafunzi apaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
Inapogawiwa kwa dada, habari hii yapasa itolewe kama ambavyo Hotuba Na. 3 imetolewa muhtasari.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, si lazima afuate mpango wa shauri lenye kufuliza kama ilivyoandikwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala yake, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri amepaswa atie duara kuzunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atafanyia kazi safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V” “M” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati, na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo mengine mafupi baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa ule utoaji wa mambo makuu ya Biblia haukuridhisha, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA HOTUBA: Kabla ya kutayarisha mgawo wa hotuba, mwanafunzi anapaswa kusoma kwa uangalifu habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulikia sifa ya usemi ipasayo kufanyiwa kazi. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya pili wapaswa kuchagua kichwa kinachofaa sehemu ya Biblia inayopasa isomwe. Hotuba nyingine zitatayarishwa kulingana na kichwa kilichoonyeshwa kwenye ratiba iliyochapishwa.
KUFUATA WAKATI: Hotuba, wala shauri na maelezo ya mshauri havipaswi kupita wakati uliowekwa. Hotuba Na. 2 hadi 4 zapasa zikatizwe kwa busara wakati unapokwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa ishara ya kuacha amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 na mambo makuu ya Biblia wanapopitisha wakati wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wapaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Programu kwa jumla: Dakika 45, bila wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi, pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari na kukamilisha ratiba ya kusoma Biblia. Biblia pekee ndiyo ya kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atapitia majibu ya maswali ya pitio pamoja na wasikilizaji na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kutumiwa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.
MAKUTANIKO MAKUBWA: Makutaniko yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasiobatizwa wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kutaniko wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa kudhamiria. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule anaweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
*td – “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation
Jan. 3 Kusoma Biblia: Nehemia 9 hadi 11
Na. 1: Namna Umoja wa Kikristo wa Kweli Unavyopatikana (uw-SW kur. 5-7 maf. 1-7)
Na. 2: Nehemia 9:4, 26-33, 36-38
Na. 3: Kufanya Mambo Yenye Ustahili wa Kweli kwa Mungu (gt-SW sura 83)
Na. 4: *td 12A au td-SW 6A Kusudi la Mungu Kuiumba Dunia
Jan. 10 Kusoma Biblia: Nehemia 12 na 13
Na. 1: Nehemia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 90-1 maf. 16-19)
Na. 2: Nehemia 13:15-18, 23-31
Na. 3: Daraka la Uanafunzi (gt-SW sura 84)
Na. 4: *td 12B au td-SW 6C Dunia Itakaliwa na Watu Sikuzote
Jan. 17 Kusoma Biblia: Esta 1 hadi 5
Na. 1: Utangulizi kwa Esta (si-SW kur. 91-2 maf. 1-6)
Na. 2: Esta 4:6-17
Na. 3: Jihadhari Kutojiona Kuwa Mwadilifu na Thamini Unyenyekevu (gt-SW sura 85)
Na. 4: *td 13A au td-SW 21A Namna ya Kuwatambua Manabii wa Uongo
Jan. 24 Kusoma Biblia: Esta 6 hadi 10
Na. 1: Esta—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 94 maf. 16-18)
Na. 2: Esta 6:1-13
Na. 3: Mwana Mpotevu na Baba Yake Mwenye Upendo (gt-SW sura 86 maf. 1-9)
Na. 4: *td 14A au td-SW 15A Sababu Kuponya kwa Kiroho Ni Muhimu
Jan. 31 Kusoma Biblia: Ayubu 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Ayubu (si-SW kur. 95-6 maf. 1-6)
Na. 2: Ayubu 2:1-13
Na. 3: Kurudi kwa Mwana Mpotevu Kwawaathiri Wengine (gt-SW sura 86 maf. 10-20)
Na. 4: *td 14B au td-SW 15B Ufalme wa Mungu Utaleta Maponyo ya Kimwili Yenye Kudumu
Feb. 7 Kusoma Biblia: Ayubu 4 hadi 6
Na. 1: Mambo Muhimu kwa Umoja wa Kikristo (uw-SW uku. 8 fu. 8 hadi 8 [3])
Na. 2: Ayubu 6:1-11, 29, 30
Na. 3: Andalia Wakati Ujao kwa Hekima Inayotumika (gt-SW sura 87)
Na. 4: *td 14C au td-SW 15C Maponyo ya Imani Leo Hayana Ushuhuda wa Kukubaliwa na Mungu
Feb. 14 Kusoma Biblia: Ayubu 7 hadi 9
Na. 1: Mambo Yanayosaidia Kuwe na Umoja wa Kikristo (uw-SW uku. 9 maf. 8 [4] hadi 9)
Na. 2: Ayubu 9:1-15
Na. 3: Tajiri na Lazaro (gt-SW sura 88 maf. 1-10)
Na. 4: *td 14D au td-SW 15D Kusema Lugha Nyingi ni Mpango wa Muda Tu
Feb. 21 Kusoma Biblia: Ayubu 10 hadi 12
Na. 1: Wakristo wa Kweli Huepuka Mavutano Yenye Kugawanya (uw-SW kur. 10-11 maf. 10-12)
Na. 2: Ayubu 12:1-16
Na. 3: Maana ya Kielezi cha Tajiri na Lazaro (gt-SW sura 88 maf. 11-21)
Na. 4: *td 15A au td-SW 25B 144,000 Peke Yao Ndio Watakwenda Mbinguni
Feb. 28 Kusoma Biblia: Ayubu 13 hadi 15
Na. 1: Mjue na Kumthamini Yehova (uw-SW kur. 12-13 maf. 1-4)
Na. 2: Ayubu 13:1-13
Na. 3: Ujumbe wa Rehema Katika Yudea (gt-SW sura 89)
Na. 4: *td 16A Hakuna Moto Halisi wa Mateso
Mac. 7 Kusoma Biblia: Ayubu 16 hadi 18
Na. 1: Iga Kielelezo cha Yehova cha Upendo (uw-SW kur. 14-15 maf. 5-7)
Na. 2: Ayubu 16:1-11, 22
Na. 3: Yesu Asema Juu ya Tumaini la Ufufuo (gt-SW sura 90)
Na. 4: *td 16B au td-SW 27A Moto ni Mfano wa Maangamizi ya Daima
Mac. 14 Kusoma Biblia: Ayubu 19 na 20
Na. 1: Saidia Watu Wajifunze Kweli Juu ya Mungu (uw-SW kur. 15-17 maf. 8 hadi 11 [2])
Na. 2: Ayubu 19:14-29
Na. 3: Yesu Amfufua Lazaro (gt-SW sura 91)
Na. 4: *td 16C au td-SW 27C Masimulizi ya Tajiri na Lazaro Hayahakikishi Kuna Mateso ya Milele
Mac. 21 Kusoma Biblia: Ayubu 21 na 22
Na. 1: Kuna Yehova Mmoja tu (uw-SW kur. 17-18 maf. 11 [3] hadi 12)
Na. 2: Ayubu 21:19-34
Na. 3: Onyesha Shukrani Kwa Ajili ya Wema wa Mungu (gt-SW sura 92)
Na. 4: *td 17A au td-SW 39B Wakristo wa Mapema Hawakuadhimisha Ukumbusho wa Siku za Kuzaliwa wala Krismasi
Mac. 28 Kusoma Biblia: Ayubu 23 hadi 26
Na. 1: Kinachomaanishwa na Kutembea Katika Jina la Mungu (uw-SW kur. 18-19 maf. 13-15)
Na. 2: Ayubu 24:1, 2, 14-25
Na. 3: Wakati Mwana wa Binadamu Anapofunuliwa (gt-SW sura 93)
Na. 4: *td 18A au td-SW 36A Kutumia Sanamu Katika Ibada Ni Kukosa Kumheshimu Mungu
Apr. 4 Kusoma Biblia: Ayubu 27 hadi 29
Na. 1: Saidia Wengine Waikubali Biblia Kuwa Neno la Mungu (uw-SW kur. 20-2 maf. 1-6)
Na. 2: Ayubu 29:2-18
Na. 3: Uhitaji wa Sala na Unyenyekevu (gt-SW sura 94)
Na. 4: *td 18B au td-SW 36B Ibada ya Sanamu Ililetea Taifa la Israeli Msiba
Apr. 11 Kusoma Biblia: Ayubu 30 na 31
Na. 1: Soma Biblia Kila Siku (uw-SW kur. 23-5 maf. 7-11)
Na. 2: Ayubu 31:23-37
Na. 3: Masomo Kuhusu Talaka na Kupenda Watoto (gt-SW sura 95)
Na. 4: *td 18C Ibada Husianifu Hairuhusiwi na Mungu
Apr. 18 Kusoma Biblia: Ayubu 32 na 33
Na. 1: Jifunze Ili Kupata Ujuzi Juu ya Yehova (uw-SW kur. 25-6 fu. 12 hadi 12 [1])
Na. 2: Ayubu 33:1-6, 23-33
Na. 3: Yesu na Mtawala Kijana Tajiri (gt-SW sura 96)
Na. 4: *td 19A au td-SW 26A Umoja wa Kweli Hauwezi Kuja Kupitia Kuchangamana na Dini Nyingine
Apr. 25 Pitio La Kuandika. Kamilisha Nehemia 9 hadi Ayubu 33
Mei 2 Kusoma Biblia: Ayubu 34 hadi 36
Na. 1: Fikiria Kichwa cha Biblia na Mistari Inayotangulia na Kufuata Andiko (uw-SW uku. 26 fu. 12 [2] na 12 [3])
Na. 2: Ayubu 34:1-15
Na. 3: Kielezi cha Yesu cha Shamba la Mizabibu (gt-SW sura 97)
Na. 4: *td 19B au td-SW 26B Si Kweli Kwamba “Dini Zote Ni Nzuri”
Mei 9 Kusoma Biblia: Ayubu 37 na 38
Na. 1: Tumia Kibinafsi Yale Unayojifunza na Kuyashiriki Pamoja na Wengine (uw-SW kur. 26-8 maf. 12 [4] hadi 13)
Na. 2: Ayubu 37:5-14, 23, 24
Na. 3: Yesu Atayarisha Wanafunzi Wake kwa Yale Yaliyo Mbele (gt-SW sura 98)
Na. 4: *td 20A au td-SW 55A Wakristo Wanapaswa Kulitumia Jina la Mungu la Kibinafsi
Mei 16 Kusoma Biblia: Ayubu 39 na 40
Na. 1: Yale Ambayo Manabii Husema Juu ya Yesu (uw-SW kur. 29-31 maf. 1-6)
Na. 2: Ayubu 40:1-14
Na. 3: Yesu Arudisha Mwana Mpotevu wa Abrahamu (gt-SW sura 99)
Na. 4. *td 20B au td-SW 55C Kweli Juu ya Kuwako kwa Mungu
Mei 23 Kusoma Biblia: Ayubu 41 na 42
Na. 1: Ayubu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 100 maf. 39-43)
Na. 2: Ayubu 42:1-10, 12-17
Na. 3: Kielezi cha Zile Mina (gt-SW sura 100)
Na. 4: *td 20C au td-SW 55D Kuzitambulisha Sifa za Mungu
Mei 30 Kusoma Biblia: Zaburi 1 hadi 6
Na. 1: Utangulizi kwa Zaburi—Sehemu 1 (si-SW uku. 101 maf. 1-5)
Na. 2: Zaburi 2:1-12
Na. 3: Yesu Amtetea Mariamu kwa Tendo Lake Jema (gt-SW sura 101)
Na. 4: *td 20D au td-SW 55F Si Wote Wanaotumikia Mungu Yule Yule
Juni 6 Kusoma Biblia: Zaburi 7 hadi 10
Na. 1: Utangulizi kwa Zaburi—Sehemu 2 (si-SW uku. 102 maf. 6-11)
Na. 2: Zaburi 8:1–9:5
Na. 3: Kristo Aingia Katika Yerusalemu kwa Shangwe ya Ushindi (gt-SW sura 102)
Na. 4: *td 21A au td-SW 22A Chanzo cha Mashahidi wa Yehova
Juni 13 Kusoma Biblia: Zaburi 11 hadi 17
Na. 1: Kaza Fikira Kwenye Mifano ya Unabii (uw-SW kur. 32-3 maf. 7 hadi 8 [2])
Na. 2: Zaburi 14:1–15:5
Na. 3: Yesu Awashutumu Wale Wanaochafua Hekalu la Mungu (gt-SW sura 103)
Na. 4: *td 22A au td-SW 56B Yesu Ni Mwana wa Mungu na Mfalme Aliyewekwa
Juni 20 Kusoma Biblia: Zaburi 18 hadi 20
Na. 1: Kuhani Wetu Mkuu Afananishwa (uw-SW uku. 33 fu. 8 [3] na 8 [4])
Na. 2: Zaburi 19:1-14
Na. 3: Sauti ya Mungu Yasikiwa Mara ya Tatu (gt-SW sura 104)
Na. 4: *td 22B au td-SW 56D Kumwamini Yesu Kristo Ni kwa Lazima ili Kupata Wokovu
Juni 27 Kusoma Biblia: Zaburi 21 hadi 24
Na. 1: Kwa Nini Toba na Imani Ni Muhimu (uw-SW kur. 33-7 maf. 9-14)
Na. 2: Zaburi 23:1–24:10
Na. 3: Kinachowakilishwa na Mtini Uliolaaniwa (gt-SW sura 105)
Na. 4: *td 22C au td-SW 56E Kumwamini Yesu Hakutoshi
Julai 4 Kusoma Biblia: Zaburi 25 hadi 29
Na. 1: Kumtii Mungu Huleta Uhuru wa Kweli (uw-SW kur. 38-40 maf. 1-5)
Na. 2: Zaburi 26:1-12
Na. 3: Namna Viongozi wa Kidini Wanavyofichuliwa (gt-SW sura 106)
Na. 4: *td 23A au td-SW 42B Mambo Ambayo Ufalme wa Mungu Utafanyia Ainabinadamu
Julai 11 Kusoma Biblia: Zaburi 30 hadi 33
Na. 1: Mahali Uhuru wa Kweli Unapoweza Kupatikana Leo (uw-SW kur. 40-2 maf. 6-9)
Na. 2: Zaburi 32:1-11
Na. 3: Kinachowakilishwa na Kielezi cha Karamu ya Ndoa (gt-SW sura 107)
Na. 4: *td 23B au td-SW 42C Utawala wa Ufalme Waanza Adui za Kristo Wakiwa Wangali Watendaji
Julai 18 Kusoma Biblia: Zaburi 34 hadi 36
Na. 1: Uhuru wa Kilimwengu Ni Utumwa Hasa (uw-SW kur. 42-3 maf. 10-12)
Na. 2: Zaburi 36:1-12
Na. 3: Washindwa Kutega Yesu (gt-SW sura 108)
Na. 4: *td 23C au td-SW 42E Ufalme wa Mungu Hausitawishwi kwa Jitahada za Wanadamu
Julai 25 Kusoma Biblia: Zaburi 37 hadi 39
Na. 1: Namna ya Kutambulisha Mashirika Mabaya (uw-SW kur. 44-5 maf. 13, 14)
Na. 2: Zaburi 37:23-38
Na. 3: Yesu Ashutumu Wapinzani Wake (gt-SW sura 109)
Na. 4: *td 24A au td-SW 40A Maana ya “Mwisho wa Ulimwengu”
Ago. 1 Kusoma Biblia: Zaburi 40 hadi 44
Na. 1: Suala Ambalo Kila Mtu Apaswa Kulikabili (uw-SW kur. 46-7 maf. 1-3)
Na. 2: Zaburi 41:1-13
Na. 3: Huduma ya Yesu Kwenye Hekalu Inakamilishwa (gt-SW sura 110)
Na. 4: *td 24B au td-SW 40B Uwe Macho Kuona Uthibitisho wa Siku za Mwisho
Ago. 8 Kusoma Biblia: Zaburi 45 hadi 49
Na. 1: Iga Imani ya Washikamanifu (uw-SW kur. 47-52 maf. 4-11
Na. 2: Zaburi 45:1-7, 10-17
Na. 3: Yesu Atoa Ishara ya Siku za Mwisho (gt-SW sura 111 maf. 1-11)
Na. 4: *td 25A au td-SW 51A Mungu Aahidi Uhai wa Milele kwa Ainabinadamu Tiifu
Ago. 15 Kusoma Biblia: Zaburi 50 hadi 52
Na. 1: Ile Kweli Humheshimu Yehova (uw-SW kur. 52-4 maf. 12-15)
Na. 2: Zaburi 51:1-17
Na. 3: Yesu Ajulisha Mengine Juu ya Siku za Mwisho (gt-SW sura 111 maf. 12-19)
Na. 4: *td 25B au td-SW 51D Washiriki wa Mwili wa Kristo Peke Yao Ndio Watakwenda Mbinguni
Ago. 22 Kusoma Biblia: Zaburi 53 hadi 57
Na. 1: Tunayojifunza Kutokana na Mungu Kuruhusu Uovu (uw-SW kur. 55-7 maf. 1-7)
Na. 2: Zaburi 55:1, 2, 12-23
Na. 3: Wale Wanawali Wenye Hekima na Wale Wapumbavu (gt-SW sura 111 maf. 20-8)
Na. 4: *td 25C au td-SW 51E Uhai wa Milele Waahidiwa kwa “Kondoo Wengine” Wasio na Hesabu
Ago. 29 Pitio La Kuandika. Kamilisha Ayubu 34 hadi Zaburi 57
Sept. 5 Kusoma Biblia: Zaburi 58 hadi 62
Na. 1: Hakuna Kamwe Ukosefu wa Haki kwa Mungu (uw-SW kur. 57-61 maf. 8-16)
Na. 2: Zaburi 62:1-12
Na. 3: Kile Kielezi cha Talanta (gt-SW sura 111 maf. 29-37)
Na. 4: *td 26A au td-SW 32B Lazima Mwungano wa Ndoa Uheshimike
Sept. 12 Kusoma Biblia: Zaburi 63 hadi 67
Na. 1: Mtegemee Yehova—Kinza Majeshi ya Roho Waovu (uw-SW kur. 62-4 maf. 1-5)
Na. 2: Zaburi 65:1-13
Na. 3: Kristo Awasilipo Katika Mamlaka ya Ufalme (gt-SW sura 111 maf. 38-46)
Na. 4: *td 26B au td-SW 32C Lazima Wakristo Waheshimu Kanuni ya Ukichwa
Sept. 19 Kusoma Biblia: Zaburi 68 na 69
Na. 1: Jihadhari na Mbinu za Ujanja za Ibilisi (uw-SW kur. 64-7 maf. 6-12)
Na. 2: Zaburi 68:1-11, 32-35
Na. 3: Sikukuu ya Kupitwa Iliyo ya Mwisho kwa Yesu Yakaribia (gt-SW sura 112)
Na. 4: *td 26C au td-SW 32D Daraka la Wazazi Wakristo Juu ya Watoto
Sept. 26 Kusoma Biblia: Zaburi 70 hadi 73
Na. 1: Vaa Suti ya Silaha Kamili Kutoka kwa Mungu (uw-SW kur. 67-9 maf. 13-15)
Na. 2: Zaburi 72:1-20
Na. 3: Yesu Atoa Somo Katika Unyenyekevu (gt-SW sura 113)
Na. 4: *td 26D au td-SW 32E Inawapasa Wakristo Waoe au Waolewe na Wakristo Tu
Okt. 3 Kusoma Biblia: Zaburi 74 hadi 77
Na. 1: Ujuzi, Imani, na Ufufuo (uw-SW kur. 70-3 maf. 1-7)
Na. 2: Zaburi 76:1-12
Na. 3: Yesu Aanzisha Ukumbusho (gt-SW sura 114)
Na. 4: *td 26E au td-SW 32F Wakristo wa Kweli Hawaoi Wake Zaidi ya Mmoja
Okt. 10 Kusoma Biblia: Zaburi 78 na 79
Na. 1: Yesu Ana Funguo za Kifo na za Hadesi (uw-SW kur. 73-7 maf. 8-15)
Na. 2: Zaburi 79:1-13
Na. 3: Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake kwa Subira Juu ya Upendo na Unyenyekevu (gt-SW sura 115)
Na. 4: *td 27A au td-SW 14A Mariamu Alikuwa Mama ya Yesu, Si “Mama ya Mungu”
Okt. 17 Kusoma Biblia: Zaburi 80 hadi 85
Na. 1: Thamini Ufalme wa Mungu Wenye Kudumu (uw-SW kur. 78-81 maf. 1-9)
Na. 2: Zaburi 83:1-18
Na. 3: Yesu Awatayarisha Mitume Kwa Ajili ya Kuondoka Kwake (gt-SW sura 116 maf. 1-14)
Na. 4: *td 27B au td-SW 14C Biblia Huonyesha Kwamba Mariamu Hakuwa “Bikira Sikuzote”
Okt. 24 Kusoma Biblia: Zaburi 86 hadi 89
Na. 1: Ufalme Utatimiza Kusudi la Mungu la Kwanza (uw-SW kur. 81-2 maf. 10-12)
Na. 2: Zaburi 86:1-17
Na. 3: Wale Walio Marafiki wa Yesu wa Kweli (gt-SW sura 116 maf. 15-25)
Na. 4: *td 28A au td-SW 45A Yale Ambayo Maandiko Husema Juu ya Ukumbusho
Okt. 31 Kusoma Biblia: Zaburi 90 hadi 94
Na. 1: Yale Ambayo Ufalme Umetimiza Tayari (uw-SW kur. 83-6 maf. 13-15)
Na. 2: Zaburi 90:1-17
Na. 3: Yesu Atangulia Kuwatahadharisha na Kuwatia Moyo Wanafunzi Wake (gt-SW sura 116 maf. 26-37)
Na. 4: *td 28B au td-SW 45B Kuadhimisha Misa Ni Kinyume cha Maandiko
Nov. 7 Kusoma Biblia: Zaburi 95 hadi 101
Na. 1: Jinsi Tunavyoutafuta Ufalme Kwanza (uw-SW kur. 87-9 maf. 1-6)
Na. 2: Zaburi 100:1–101:8
Na. 3: Sala ya Yesu ya Kumalizia Katika Chumba cha Juu (gt-SW sura 116 maf. 38-51)
Na. 4: *td 29A Ni Lazima Wakristo Wote Wawe Wahudumu
Nov. 14 Kusoma Biblia: Zaburi 102 hadi 104
Na. 1: Fuata Mfano wa Wanafunzi wa Kwanza (uw-SW kur. 90-1 maf. 7-9)
Na. 2: Zaburi 103:1-14, 21, 22
Na. 3: Uguo Kali Katika Bustani (gt-SW sura 117)
Na. 4: *td 29B Sifa za Kustahili Kwa Ajili ya Huduma
Nov. 21 Kusoma Biblia: Zaburi 105 na 106
Na. 1: Uweke Ufalme Kwanza Wewe Binafsi (uw-SW kur. 91-4 maf. 10-15)
Na. 2: Zaburi 106:1-12, 47, 48
Na. 3: Kusalitiwa na Kukamatwa kwa Yesu (gt-SW sura 118)
Na. 4: *td 30A au td-SW 47A Sababu Wakristo wa Kweli Wanachukiwa
Nov. 28 Kusoma Biblia: Zaburi 107 hadi 109
Na. 1: Yale Ambayo Maandiko Husema Juu ya Ubatizo Uliofanywa na Yohana (uw-SW 95-6 maf. 1-5)
Na. 2: Zaburi 108:1-13
Na. 3: Yesu Anatendwa Vibaya na Kuhukumiwa Isivyo Halali (gt-SW sura 119)
Na. 4: *td 30B au td-SW 47C Mke Asiruhusu Mume Amtenge na Mungu
Des. 5 Kusoma Biblia: Zaburi 110 hadi 115
Na. 1: Ubatizo Katika Kifo (uw-SW kur. 97-8 maf. 6-8)
Na. 2: Zaburi 110:1-7; 114:1-8
Na. 3: Kumhofu Binadamu Kwamsukuma Petro Amkane Kristo (gt-SW sura 120)
Na. 4: *td 30C au td-SW 47D Mume Asiruhusu Mke Amzuie Kumtumikia Mungu
Des. 12 Kusoma Biblia: Zaburi 116 hadi 119:32
Na. 1: Ubatizo “Katika Jina la Baba na la Mwana na la Roho Takatifu” (uw-SW uku. 98 fu. 9)
Na. 2: Zaburi 116:1-19
Na. 3: Yesu Asema Kweli kwa Ujasiri Mbele ya Sanhedrini na Pilato (gt-SW sura 121)
Na. 4: *td 31A au td-SW 35A Sala Ambazo Mungu Husikia
Des. 19 Kusoma Biblia: Zaburi 119:33-112
Na. 1: Ubatizo na Madaraka ya Kikristo (uw-SW kur. 99-102 maf. 10-14)
Na. 2: Zaburi 119:97-112
Na. 3: Wala Pilato Wala Herode Hawawezi Kuona Kosa kwa Yesu (gt-SW sura 122)
Na. 4: *td 31B au td-SW 35C Sababu Sala Fulani Hazifai
Des. 26 Pitio La Kuandika. Kamilisha Zaburi 58 hadi 119:112