Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 21
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati 21:1

Marejeo

  • +Zb 9:12; Met 28:17; Isa 26:21

Kumbukumbu la Torati 21:2

Marejeo

  • +Kum 16:18

Kumbukumbu la Torati 21:4

Marejeo

  • +Hes 35:33

Kumbukumbu la Torati 21:5

Marejeo

  • +Kut 28:1; Kum 18:5
  • +Hes 6:23; 1Nya 23:13
  • +Kum 17:9; 19:17; Mal 2:7

Kumbukumbu la Torati 21:6

Marejeo

  • +Zb 26:6; Mt 27:24

Kumbukumbu la Torati 21:7

Marejeo

  • +2Sa 3:28; Zb 7:3

Kumbukumbu la Torati 21:8

Marejeo

  • +Kum 13:5; 2Sa 7:23
  • +Hes 16:22; Yer 26:15; Yon 1:14

Kumbukumbu la Torati 21:9

Marejeo

  • +Kum 19:13
  • +Kum 13:18; Zb 11:4; Met 15:3; Ebr 4:13

Kumbukumbu la Torati 21:10

Marejeo

  • +Kum 20:13; Yos 21:44
  • +Hes 31:9; Kum 20:14

Kumbukumbu la Torati 21:11

Marejeo

  • +Mwa 29:20; 34:3; Amu 14:2

Kumbukumbu la Torati 21:12

Marejeo

  • +Isa 3:24; 1Ko 11:6

Kumbukumbu la Torati 21:13

Marejeo

  • +Hes 20:29; Kum 34:8

Kumbukumbu la Torati 21:14

Marejeo

  • +Kum 24:1
  • +Law 25:46

Kumbukumbu la Torati 21:15

Marejeo

  • +Mwa 29:30, 33; 1Sa 1:4

Kumbukumbu la Torati 21:16

Marejeo

  • +2Nya 21:3

Kumbukumbu la Torati 21:17

Marejeo

  • +1Nya 5:1
  • +Mwa 49:3; Zb 105:36
  • +Mwa 25:31; Ebr 12:16

Kumbukumbu la Torati 21:18

Marejeo

  • +Met 30:11
  • +Kut 20:12; Kum 27:16; Met 1:8; 20:20; Eze 22:7; Efe 6:1
  • +Kum 8:5; Met 13:24; 19:18; 23:13; Ebr 12:9

Kumbukumbu la Torati 21:19

Marejeo

  • +Kum 16:18

Kumbukumbu la Torati 21:20

Marejeo

  • +Met 15:5; 19:26; 30:17
  • +Met 23:20; 28:7
  • +Met 20:1; 23:21; Ro 13:13; 1Ko 6:10; Efe 5:18

Kumbukumbu la Torati 21:21

Marejeo

  • +Kum 13:11

Kumbukumbu la Torati 21:22

Marejeo

  • +Hes 25:5; 2Sa 4:12
  • +Yos 10:26; Mdo 10:39

Kumbukumbu la Torati 21:23

Marejeo

  • +Yos 8:29; Yoh 19:31
  • +2Ko 5:21; Gal 3:13
  • +Hes 35:34

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 21:1Zb 9:12; Met 28:17; Isa 26:21
Kum. 21:2Kum 16:18
Kum. 21:4Hes 35:33
Kum. 21:5Kut 28:1; Kum 18:5
Kum. 21:5Hes 6:23; 1Nya 23:13
Kum. 21:5Kum 17:9; 19:17; Mal 2:7
Kum. 21:6Zb 26:6; Mt 27:24
Kum. 21:72Sa 3:28; Zb 7:3
Kum. 21:8Kum 13:5; 2Sa 7:23
Kum. 21:8Hes 16:22; Yer 26:15; Yon 1:14
Kum. 21:9Kum 19:13
Kum. 21:9Kum 13:18; Zb 11:4; Met 15:3; Ebr 4:13
Kum. 21:10Kum 20:13; Yos 21:44
Kum. 21:10Hes 31:9; Kum 20:14
Kum. 21:11Mwa 29:20; 34:3; Amu 14:2
Kum. 21:12Isa 3:24; 1Ko 11:6
Kum. 21:13Hes 20:29; Kum 34:8
Kum. 21:14Kum 24:1
Kum. 21:14Law 25:46
Kum. 21:15Mwa 29:30, 33; 1Sa 1:4
Kum. 21:162Nya 21:3
Kum. 21:171Nya 5:1
Kum. 21:17Mwa 49:3; Zb 105:36
Kum. 21:17Mwa 25:31; Ebr 12:16
Kum. 21:18Met 30:11
Kum. 21:18Kut 20:12; Kum 27:16; Met 1:8; 20:20; Eze 22:7; Efe 6:1
Kum. 21:18Kum 8:5; Met 13:24; 19:18; 23:13; Ebr 12:9
Kum. 21:19Kum 16:18
Kum. 21:20Met 15:5; 19:26; 30:17
Kum. 21:20Met 23:20; 28:7
Kum. 21:20Met 20:1; 23:21; Ro 13:13; 1Ko 6:10; Efe 5:18
Kum. 21:21Kum 13:11
Kum. 21:22Hes 25:5; 2Sa 4:12
Kum. 21:22Yos 10:26; Mdo 10:39
Kum. 21:23Yos 8:29; Yoh 19:31
Kum. 21:232Ko 5:21; Gal 3:13
Kum. 21:23Hes 35:34
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 21:1-23

Kumbukumbu la Torati

21 “Ikiwa mtu atapatikana akiwa ameuawa katika nchi ambayo Yehova Mungu wako anakupa uimiliki, akiwa ameanguka uwanjani, na haijajulikana ni nani aliyempiga na kumuua,+ 2 wanaume wako wazee na waamuzi+ wako watatoka nje na kupima mpaka kwenye majiji yanayomzunguka mtu aliyeuawa; 3 na itakuwa ni lile jiji lililo karibu zaidi na yule aliyeuawa. Nao wanaume wazee wa jiji hilo watamchukua ng’ombe mchanga kutoka kati ya mifugo ambaye hajafanya kazi, ambaye hajavuta nira; 4 na wanaume wazee wa jiji hilo watampeleka ng’ombe huyo mpaka kwenye bonde la mto wenye maji yanayotiririka ambapo kidesturi hapakuwa na kulima wala kupanda mbegu, nao watavunja shingo ya ng’ombe huyo mchanga katika bonde hilo la mto.+

5 “Na makuhani wana wa Lawi watakaribia, kwa sababu hao ndio Yehova Mungu wako amechagua wamhudumie+ na kulisifu+ jina la Yehova na ambao kwa kinywa chao kila mzozo juu ya kila tendo lenye jeuri, wapasa kuondolewa mbali.+ 6 Kisha wanaume wote wazee wa jiji hilo walio karibu zaidi na mtu aliyeuawa wataosha mikono yao+ juu ya yule ng’ombe mchanga, ambaye shingo yake ilivunjwa katika lile bonde la mto; 7 nao watajibu na kusema, ‘Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona ikimwagwa.+ 8 Usiihesabie watu wako Israeli, ambao ulikomboa,+ Ee Yehova, wala usiweke katikati ya watu wako Israeli hatia ya damu isiyo na hatia.’+ Na wasihesabiwe hatia hiyo ya damu. 9 Na wewe—wewe utaondolea mbali hatia ya damu kutoka katikati yako,+ kwa sababu utafanya yaliyo sawa machoni pa Yehova.+

10 “Ikiwa utaenda vitani kupigana na adui zako na Yehova Mungu wako awe amewatia mkononi mwako+ nawe uwachukue mateka;+ 11 nawe uone kati ya mateka hao mwanamke mwenye umbo zuri, nawe ushikamane naye+ na kumchukua awe mke wako, 12 ndipo utakapomleta ndani ya nyumba yako. Lazima anyoe kichwa chake,+ atunze kucha zake, 13 na kuvua nguo ya kujitanda ya utekwa wake, akae katika nyumba yako, amlilie baba yake na mama yake kwa mwezi mzima;+ na baada ya jambo hilo utalala naye, nawe utamchukua awe bibi-arusi wako, naye atakuwa mke wako. 14 Na itatukia kwamba ikiwa hukupendezwa naye, basi utamwacha aende zake,+ kama inavyopenda nafsi yake mwenyewe; lakini hutamuuza kamwe kwa ajili ya pesa. Usimwonee+ baada ya kumfedhehesha.

15 “Ikiwa mwanamume atakuwa na wake wawili, mmoja anayependwa na mwingine anayechukiwa, nao, yule anayependwa na yule anayechukiwa, wamzalie wana, na iwe kwamba mwana mzaliwa wa kwanza ni wa yule anayechukiwa,+ 16 pia itatukia kwamba katika siku ambayo atawapa wanawe urithi wa vitu alivyo navyo, hataruhusiwa kumfanya mwana wa yule anayependwa awe mzaliwa wake wa kwanza kwa hasara ya mwana wa yule anayechukiwa, mzaliwa wa kwanza.+ 17 Kwa maana anapaswa kumtambua mwana wa yule anayechukiwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu mbili za kila kitu alicho nacho,+ kwa sababu huyo ndiye mwanzo wa nguvu zake za uzazi.+ Haki ya cheo cha mzaliwa wa kwanza ni yake.+

18 “Ikiwa mtu atakuwa na mwana ambaye ni mkaidi na mwasi,+ awe hasikilizi sauti ya baba yake au sauti ya mama yake,+ nao wamemrekebisha bali yeye hawasikilizi,+ 19 baba yake na mama yake watamshika na kumtoa nje mpaka kwa wanaume wazee wa jiji lake na kwenye lango la mahali pake,+ 20 nao watawaambia wanaume wazee wa jiji lake, ‘Huyu mwana wetu ni mkaidi na mwasi; hasikilizi sauti yetu,+ ni mlafi+ na mlevi.’+ 21 Ndipo watu wote wa jiji watampiga kwa mawe, naye lazima afe. Kwa hiyo mtaondolea mbali kilicho kibaya kutoka kati yenu, na Israeli wote watasikia na kuogopa kwelikweli.+

22 “Na ikiwa mtu atakuwa na dhambi inayostahili hukumu ya kifo, naye ameuawa,+ nawe umemtundika juu ya mti,+ 23 maiti yake isibaki usiku kucha juu ya mti;+ bali kwa vyovyote utamzika siku hiyo, kwa sababu mtu aliyetundikwa ni kitu kilicholaaniwa na Mungu;+ nawe usiitie unajisi nchi yako, ambayo Yehova Mungu wako anakupa iwe urithi.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki