Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 24
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Samweli—Yaliyomo

      • Dhambi ya Daudi ya kuwahesabu watu (1-14)

      • Ugonjwa hatari wasababisha vifo vya watu 70,000 (15-17)

      • Daudi ajenga madhabahu (18-25)

        • Hatatoa dhabihu ambazo hazimgharimu (24)

2 Samweli 24:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Daudi alipochochewa.”

Marejeo

  • +2Sa 21:1
  • +1Nya 27:23, 24
  • +1Nya 21:1-3

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    The Watchtower,

    5/15/2005, uku. 19

    7/15/1992, uku. 5

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 5/15 19

2 Samweli 24:2

Marejeo

  • +2Sa 8:16; 20:23
  • +Amu 20:1

2 Samweli 24:4

Marejeo

  • +Hes 1:2; 1Nya 21:4

2 Samweli 24:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kusini.”

Marejeo

  • +Kum 2:36; Yos 13:8, 9
  • +Hes 32:34, 35

2 Samweli 24:6

Marejeo

  • +Hes 32:40
  • +Mwa 10:15; 49:13; Yos 11:8

2 Samweli 24:7

Marejeo

  • +Yos 19:24, 29
  • +Yos 11:19
  • +Yos 15:1
  • +Mwa 21:31; Yos 15:21, 28

2 Samweli 24:9

Marejeo

  • +Hes 2:32; 26:51; 1Nya 21:5, 6; 27:23

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    7/15/1992, uku. 5

2 Samweli 24:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “dhamiri ya Daudi ikajaa.”

Marejeo

  • +1Sa 24:5; Ro 2:15
  • +2Sa 12:13
  • +Zb 130:3; Ho. 14:2; 1Yo 1:9
  • +1Nya 21:8-13

2 Samweli 24:11

Marejeo

  • +1Sa 22:5; 1Nya 29:29

2 Samweli 24:12

Marejeo

  • +Met 3:12

2 Samweli 24:13

Marejeo

  • +Law 26:18, 20; 2Sa 21:1
  • +Law 26:14, 17
  • +Law 26:16

2 Samweli 24:14

Marejeo

  • +Ebr 12:6
  • +Zb 103:8; 119:156
  • +2Nya 28:1, 5

2 Samweli 24:15

Marejeo

  • +Hes 16:46; 1Nya 27:24
  • +1Nya 21:14, 15
  • +2Sa 24:2

2 Samweli 24:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “akahuzunika.”

Marejeo

  • +Zb 78:38; Yer 26:19; Yoe 2:13
  • +2Nya 3:1
  • +Mwa 10:15, 16; Yos 15:8

2 Samweli 24:17

Marejeo

  • +Zb 95:7
  • +1Nya 21:16, 17

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    The Watchtower,

    5/15/2005, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 5/15 19

2 Samweli 24:18

Marejeo

  • +1Nya 21:18-23; 2Nya 3:1

2 Samweli 24:21

Marejeo

  • +Hes 16:46, 47; 25:8; 2Sa 24:15

2 Samweli 24:22

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kilicho chema machoni pako.”

2 Samweli 24:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Shekeli moja ilikuwa na uzito wa gramu 11.4. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +1Nya 21:24-28

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha,

    7/2022, uku. 7

2 Samweli 24:25

Marejeo

  • +Kut 20:25; 1Nya 22:1
  • +2Sa 21:14; 2Nya 33:13

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Sam. 24:12Sa 21:1
2 Sam. 24:11Nya 27:23, 24
2 Sam. 24:11Nya 21:1-3
2 Sam. 24:22Sa 8:16; 20:23
2 Sam. 24:2Amu 20:1
2 Sam. 24:4Hes 1:2; 1Nya 21:4
2 Sam. 24:5Kum 2:36; Yos 13:8, 9
2 Sam. 24:5Hes 32:34, 35
2 Sam. 24:6Hes 32:40
2 Sam. 24:6Mwa 10:15; 49:13; Yos 11:8
2 Sam. 24:7Yos 19:24, 29
2 Sam. 24:7Yos 11:19
2 Sam. 24:7Yos 15:1
2 Sam. 24:7Mwa 21:31; Yos 15:21, 28
2 Sam. 24:9Hes 2:32; 26:51; 1Nya 21:5, 6; 27:23
2 Sam. 24:101Sa 24:5; Ro 2:15
2 Sam. 24:102Sa 12:13
2 Sam. 24:10Zb 130:3; Ho. 14:2; 1Yo 1:9
2 Sam. 24:101Nya 21:8-13
2 Sam. 24:111Sa 22:5; 1Nya 29:29
2 Sam. 24:12Met 3:12
2 Sam. 24:13Law 26:18, 20; 2Sa 21:1
2 Sam. 24:13Law 26:14, 17
2 Sam. 24:13Law 26:16
2 Sam. 24:14Ebr 12:6
2 Sam. 24:14Zb 103:8; 119:156
2 Sam. 24:142Nya 28:1, 5
2 Sam. 24:15Hes 16:46; 1Nya 27:24
2 Sam. 24:151Nya 21:14, 15
2 Sam. 24:152Sa 24:2
2 Sam. 24:16Zb 78:38; Yer 26:19; Yoe 2:13
2 Sam. 24:162Nya 3:1
2 Sam. 24:16Mwa 10:15, 16; Yos 15:8
2 Sam. 24:17Zb 95:7
2 Sam. 24:171Nya 21:16, 17
2 Sam. 24:181Nya 21:18-23; 2Nya 3:1
2 Sam. 24:21Hes 16:46, 47; 25:8; 2Sa 24:15
2 Sam. 24:241Nya 21:24-28
2 Sam. 24:25Kut 20:25; 1Nya 22:1
2 Sam. 24:252Sa 21:14; 2Nya 33:13
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Samweli 24:1-25

Kitabu cha Pili cha Samweli

24 Hasira ya Yehova ikawaka tena dhidi ya Waisraeli+ mtu fulani alipomchochea Daudi* atende kinyume chao kwa kumwambia: “Nenda, ukawahesabu+ watu wa Israeli na Yuda.”+ 2 Basi mfalme akamwambia Yoabu+ mkuu wa jeshi aliyekuwa pamoja naye: “Tafadhali nenda katika makabila yote ya Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-sheba,+ uwaandikishe watu, ili nijue idadi yao.” 3 Lakini Yoabu akamwambia mfalme: “Yehova Mungu wako na azidishe idadi ya watu mara 100, na macho yako bwana wangu mfalme na yaone jambo hilo, lakini kwa nini bwana wangu mfalme unataka kufanya jambo la namna hii?”

4 Lakini neno la mfalme likawa na nguvu kuliko neno la Yoabu na wakuu wa jeshi. Basi Yoabu na wakuu wa jeshi wakaondoka mbele ya mfalme na kwenda kuwaandikisha watu wa Israeli.+ 5 Wakavuka Yordani na kupiga kambi Aroeri,+ upande wa kulia* wa jiji katikati ya bonde, kuelekea kwa Wagadi, na mpaka Yazeri.+ 6 Kisha wakaenda mpaka Gileadi+ na nchi ya Tahtim-hodshi, wakaendelea mpaka Dani-yaani nao wakazunguka mpaka Sidoni.+ 7 Kisha wakaenda kwenye ngome ya Tiro+ na katika majiji yote ya Wahivi+ na ya Wakanaani, mwishowe wakafika Negebu+ ya Yuda kule Beer-sheba.+ 8 Kwa hiyo wakapita katika nchi yote na kurudi Yerusalemu baada ya miezi tisa na siku 20. 9 Basi Yoabu akampa mfalme idadi ya watu walioandikishwa. Mashujaa wa Israeli waliojihami kwa mapanga walikuwa 800,000, na wanaume wa Yuda walikuwa 500,000.+

10 Lakini moyo wa Daudi ukajaa* majuto+ baada ya kuwahesabu watu. Basi Daudi akamwambia Yehova: “Nimetenda dhambi+ kubwa kwa kufanya jambo hili. Na sasa, Yehova, tafadhali nisamehe kosa langu mimi mtumishi wako,+ kwa maana nimetenda kwa upumbavu sana.”+ 11 Daudi alipoamka asubuhi, neno la Yehova likamjia nabii Gadi,+ mwonaji wa Daudi, likisema: 12 “Nenda ukamwambie Daudi, ‘Yehova anasema hivi: “Ninakupa mambo matatu ya kuchagua. Chagua jambo nitakalokutendea.”’”+ 13 Basi Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia: “Je, unataka njaa kali ije katika nchi yako kwa miaka saba?+ Au unataka kuwakimbia maadui wako kwa miezi mitatu huku wakikufuatia? + Au unataka nchi yako ikumbwe na ugonjwa hatari kwa siku tatu?+ Sasa fikiria kwa makini jibu ninalopaswa kumpa Yule aliyenituma.” 14 Kwa hiyo Daudi akamwambia Gadi: “Jambo hilo linanihuzunisha sana. Tafadhali, acha tuanguke mkononi mwa Yehova,+ kwa maana rehema zake ni nyingi;+ lakini usiniache nianguke mkononi mwa mwanadamu.”+

15 Ndipo Yehova akaleta ugonjwa hatari+ Israeli kuanzia asubuhi mpaka wakati uliowekwa, hivi kwamba watu 70,000 wakafa+ kuanzia Dani mpaka Beer-sheba.+ 16 Malaika alipounyoosha mkono wake kuelekea jiji la Yerusalemu ili kuliangamiza, Yehova akaghairi* kwa sababu ya msiba huo,+ akamwambia malaika aliyekuwa akiwaangamiza watu: “Imetosha! Sasa shusha mkono wako.” Malaika wa Yehova alikuwa karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna+ Myebusi.+

17 Daudi alipomwona malaika aliyekuwa akiwaangamiza watu, akamwambia Yehova: “Mimi ndiye niliyetenda dhambi, na mimi ndiye niliyekosea; lakini kondoo hawa+—wamefanya nini? Tafadhali, acha mkono wako uniadhibu mimi na nyumba ya baba yangu.”+

18 Basi Gadi akaenda kwa Daudi siku hiyo na kumwambia: “Panda ukamjengee Yehova madhabahu kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi.”+ 19 Basi Daudi akapanda kulingana na neno la Gadi, kama Yehova alivyoamuru. 20 Arauna alipotazama chini na kumwona mfalme na watumishi wake wakija kumwelekea, mara moja Arauna akatoka nje na kumwinamia mfalme kifudifudi. 21 Arauna akamuuliza: “Bwana wangu mfalme kwa nini umekuja kwangu mimi mtumishi wako?” Daudi akamjibu: “Kununua uwanja wako wa kupuria ili nimjengee Yehova madhabahu, ili ugonjwa hatari ambao umewakumba watu ukomeshwe.”+ 22 Lakini Arauna akamwambia Daudi: “Bwana wangu mfalme uchukue na kutoa unachoona ni chema.* Ndio hawa ng’ombe kwa ajili ya dhabihu ya kuteketezwa na kifaa cha kupuria nafaka na nira za ng’ombe utakazotumia kama kuni. 23 Ee mfalme, mimi Arauna nimekupa vitu hivi vyote.” Kisha Arauna akamwambia mfalme: “Yehova Mungu wako na akupe kibali.”

24 Hata hivyo, mfalme akamwambia Arauna: “Hapana, ni lazima niununue kwa bei fulani. Sitamtolea Yehova Mungu wangu dhabihu za kuteketezwa ambazo hazinigharimu chochote.” Basi Daudi akanunua uwanja huo wa kupuria nafaka na hao ng’ombe kwa shekeli 50 za fedha.*+ 25 Kisha Daudi akamjengea Yehova madhabahu+ mahali hapo na kutoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za ushirika. Ndipo Yehova akakubali maombi ya kusihi yaliyotolewa kwa ajili ya nchi,+ na ugonjwa hatari uliowakumba Waisraeli ukakomeshwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki