Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/96 kur. 3-6
  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1997

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1997
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
  • Vichwa vidogo
  • Maagizo
  • RATIBA
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 10/96 kur. 3-6

Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1997

Maagizo

Wakati wa 1997, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango wakati wa kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.

VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli [uw-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW], Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele [kl-SW], na Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW] vitakuwa msingi wa migawo.

Shule yapaswa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha kisha kuendelea kama ifuatavyo:

MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea habari katika kitabu Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapishwa katika kichapo hicho. Lengo lapaswa kuwa si kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, ukikazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe. Wote wanatiwa moyo watayarishe kimbele kwa uangalifu ili wasikilizaji wanufaike kikamili na habari hii.

Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa ni lazima, au ikiwa msemaji ameomba shauri.

MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma atakayeitumia habari vya kufaa kuhusu mahitaji ya kwao. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo zimegawiwa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani hiyo habari ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi watakaporuhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.

MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa habari iliyotolewa kuwa mgawo utakaotolewa na ndugu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika shule kubwa na pia katika vikundi visaidizi vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari mahali ambapo usomaji waendelea.

MGAWO NA. 3: Dakika 5. Huu utagawiwa akina dada. Habari za utoaji huu zitategemea kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Kikao huenda kikawa ziara ya kurudia au funzo la Biblia nyumbani, na huenda washiriki wakawa ama wameketi ama wamesimama. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na njia ambayo mwanafunzi amsaidia mwenye nyumba asababu na kuelewa habari na jinsi maandiko yanavyotumiwa. Mwanafunzi anayegawiwa sehemu hii apaswa awe anajua kusoma. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Mwanafunzi aweza kuamua kama atamtumia au hatamtumia mwenye nyumba asome mafungu fulani ya kitabu. Si kikao kinachopasa kupewa uangalifu mkuu, bali ni matumizi ya habari yenye matokeo.

MGAWO NA. 4: Dakika 5. Huu utagawiwa ndugu au dada. Utategemea habari katika kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko au “Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia.” Unapogawiwa ndugu, huu wapaswa uwe hotuba kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi kwa huyo ndugu kutayarisha hotuba yake akifikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Dada anapopewa sehemu hii, habari yapasa itolewe kama vile ilivyoonyeshwa kwa Mgawo Na. 3.

SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila utoaji wa mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, bila kufuata kwa lazima programu ya shauri ya hatua kwa hatua iliyoonyeshwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala ya hivyo, apaswa kukazia fikira sehemu zile ambazo mwanafunzi ahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mwanafunzi astahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri apaswa atie duara kuzunguka kisanduku, ambamo kwa kawaida alama “V,” “M,” au “T” zingewekwa, cha sifa ya usemi ambayo mwanafunzi apaswa kufanyia kazi safari nyingine. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale watakaoshiriki katika programu wapaswa wakae kuelekea mbele ya jumba. Hilo litaokoa wakati na litamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati uruhusupo baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuarifu na yenye mafaa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Mwangalizi wa shule hapaswi kutumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo mengine yoyote mafupi baada ya kila utoaji wa mwanafunzi. Ikiwa ndugu anayeshughulikia ule mgawo wa mambo makuu ya Biblia ahitaji shauri, hilo laweza kutolewa faraghani.

KUTAYARISHA MIGAWO: Kabla ya kutayarisha sehemu iliyogawiwa, mwanafunzi apaswa kusoma kwa uangalifu habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulikia sifa ya usemi ipasayo kufanyiwa kazi. Wanafunzi waliopewa Mgawo Na. 2 waweza kuchagua kichwa kinachofaa sehemu ya Biblia inayopasa isomwe. Migawo mingine yapaswa kutayarishwa kulingana na kichwa kilichoonyeshwa kwenye ratiba iliyochapishwa.

KUFUATA WAKATI: Hakuna apaswaye kuzidi wakati uliowekwa, wala shauri na maelezo ya mshauri hayapaswi kuzidi wakati uliowekwa. Migawo Na. 2 hadi 4 yapasa ikatizwe kwa busara wakati unapokwisha. Yule anayechaguliwa kutoa ishara ya kuacha apaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 na mambo makuu ya Biblia wanapopitisha wakati wao wapaswa wapewe shauri la faragha. Programu kwa jumla: Dakika 45, bila wimbo na sala.

PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia habari iliyogawiwa na kukamilisha usomaji wa Biblia ulioratibiwa. Biblia pekee ndiyo yaweza kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atapitia majibu ya maswali ya pitio pamoja na wasikilizaji na kukazia fikira maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayaelewe majibu kwa wazi. Ikiwa hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kutolewa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.

MAKUTANIKO MAKUBWA: Makutaniko yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine sehemu zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasiobatizwa ambao maisha zao zapatana na kanuni za Kikristo waweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.

WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kutaniko waweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa kudhamiria. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mjitoleaji aweza kuchukua mgawo huo, akifanya matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule aweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.

RATIBA

*td – “Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia” kama ipatikanavyo katika New World Translation

Jan. 6 Usomaji wa Biblia: Zekaria 1 hadi 5

Wimbo Na. 85

Na. 1: Utangulizi kwa Zekaria (si-SW kur. 168-169 maf. 1-7)

Na. 2: Zekaria 2:1-13

Na. 3: Mwanadamu Hakuumbwa Ili Afe (kl-SW uku. 53 maf. 1-3)

Na. 4: Roho ya Ulimwengu Ni Nini, na Kwa Nini Ni Hatari? (rs-SW uku. 265 fu. 2-uku. 266 fu. 2)

Jan. 13 Usomaji wa Biblia: Zekaria 6 hadi 9

Wimbo Na. 215

Na. 1: Yesu Ana Funguo za Kifo na Hadesi (uw-SW kur. 73-77 maf. 8-15)

Na. 2: Zekaria 7:1-14

Na. 3: Njama Yenye Uovu (kl-SW kur. 55-56 maf. 4-7)

Na. 4: Kiburi na Uasi Ni Maonyesho ya Roho ya Ulimwengu (rs-SW uku. 266 fu. 3-267 fu. 1)

Jan. 20 Usomaji wa Biblia: Zekaria 10 hadi 14

Wimbo Na. 98

Na. 1: Zekaria—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 171-172 maf. 23-27)

Na. 2: Zekaria 12:1-14

Na. 3: Jinsi Shetani Alivyotekeleza Njama Yake (kl-SW kur. 56-58 maf. 8-12)

Na. 4: Roho ya Ulimwengu Huchochea Tamaa za Mnofu (rs-SW uku. 267 fu. 2)

Jan. 27 Usomaji wa Biblia: Malaki 1 hadi 4

Wimbo Na. 118

Na. 1: Utangulizi kwa Malaki na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 172-175 maf. 1-6, 13-17)

Na. 2: Malaki 1:6-14

Na. 3: Jinsi Dhambi na Kifo Vilivyoenea (kl-SW kur. 58-59 maf. 13-15)

Na. 4: Roho ya Ulimwengu Huchochea Mambo ya Kimwili (rs-SW uku. 267 maf. 3-4)

Feb. 3 Usomaji wa Biblia: Mathayo 1 hadi 3

Wimbo Na. 132

Na. 1: Utangulizi kwa Mathayo (si-SW kur. 175-177 maf. 1-10)

Na. 2: Mathayo 2:1-15

Na. 3: Jihadhari na Mbinu za Shetani (kl-SW kur. 59-60 maf. 16-18)

Na. 4: Piga Vita Vikali Dhidi ya Mnofu (rs-SW uku. 268 fu. 1)

Feb. 10 Usomaji wa Biblia: Mathayo 4 na 5

Wimbo Na. 36

Na. 1: Thamini Ufalme wa Mungu Wenye Kudumu (uw-SW kur. 78-81 maf. 1-9)

Na. 2: Mathayo 4:1-17

Na. 3: Uwe na Imani na Ujitayarishe kwa Upinzani (kl-SW kur. 60-61 maf. 19-21)

Na. 4: Mtumaini Yehova, Si Watawala wa Kibinadamu (rs-SW uku. 268 fu. 2-3)

Feb. 17 Usomaji wa Biblia: Mathayo 6 na 7

Wimbo Na. 222

Na. 1: Yale Ambayo Ufalme wa Mungu Utatimiza (uw-SW kur. 81-82 maf. 10-12)

Na. 2: Mathayo 7:1-14

Na. 3: Njia ya Mungu ya Kuokoa Wanadamu (kl-SW kur. 62-63 maf. 1-5)

Na. 4: Ni Nani Mwenye Lawama Kwa Ajili Ya Kuteseka kwa Binadamu? (rs-SW uku. 131 fu. 5- uku. 132 fu. 2)

Feb. 24 Usomaji wa Biblia: Mathayo 8 na 9

Wimbo Na. 162

Na. 1: Yale Ambayo Ufalme Umetimiza Tayari (uw-SW kur. 83-86 maf. 13-15)

Na. 2: Mathayo 8:1-17

Na. 3: Sababu Kwa Nini Mesiya Angekufa (kl-SW kur. 63-65 maf. 6-11)

Na. 4: Kuteseka kwa Binadamu Kulianzaje? (rs-SW uku. 132 fu. 3-uku. 133 fu. 1)

Mac. 3 Usomaji wa Biblia: Mathayo 10 na 11

Wimbo Na. 172

Na. 1: Jinsi Tunavyoutafuta Kwanza Ufalme (uw-SW kur. 87-89 maf. 1-6)

Na. 2: Mathayo 11:1-15

Na. 3: Jinsi Fidia Ilivyolipwa (kl-SW kur. 65-68 maf. 12-16)

Na. 4: Kile Ambacho Mungu Amefanya Ili Kusaidia Wanadamu Wanaoteseka (rs-SW uku. 133 maf. 2-3)

Mac. 10 Usomaji wa Biblia: Mathayo 12 na 13

Wimbo Na. 133

Na. 1: Fuata Kigezo cha Wanafunzi wa Kwanza (uw-SW kur. 90-91 maf. 7-9)

Na. 2: Mathayo 12:22-37

Na. 3: Fidia ya Kristo na Wewe (kl-SW kur. 68-69 maf. 17-20)

Na. 4: Kwa Nini Mungu Ameruhusu Kuteseka Kuendelee? (rs-SW uku. 134 fu. 1-uku. 135 fu. 2)

Mac. 17 Usomaji wa Biblia: Mathayo 14 na 15

Wimbo Na. 129

Na. 1: Uweke Ufalme Kwanza Katika Maisha Yako (uw-SW kur. 91-94 maf. 10-15)

Na. 2: Mathayo 14:1-22

Na. 3: Je, Mungu Anahusika na Kuteseka kwa Binadamu? (kl-SW kur. 70-71 maf. 1-5)

Na. 4: Tunayopaswa Kujua Kuhusu Kasoro za Kuzaliwa (rs-SW uku. 135 maf. 3-6)

Mac. 24 Usomaji wa Biblia: Mathayo 16 na 17

Wimbo Na. 151

Na. 1: Yanayosema Maandiko Kuhusu Ubatizo wa Yohana (uw-SW kur. 95-96 maf. 1-5)

Na. 2: Mathayo 17:14-27

Na. 3: Mwanzo Mkamilifu na Shtaka Lenye Nia Mbovu (kl-SW kur. 72-73 maf. 6-10)

Na. 4: Sababu Gani Mungu Anaruhusu “Misiba Asilia”? (rs-SW uku. 136 fu. 1-3)

Mac. 31 Usomaji wa Biblia: Mathayo 18 na 19

Wimbo Na. 97

Na. 1: Ubatizo Katika Kifo Ni Nini? (uw-SW kur. 97-98 maf. 6-8)

Na. 2: Mathayo 19:16-30

Na. 3: Yale Masuala Halisi na Njia ya Yehova ya Kuyasuluhisha (kl-SW kur. 74-76 maf. 11-15)

Na. 4: Je, Watu Wanaopatwa na Taabu Wanaadhibiwa na Mungu? (rs-SW uku. 137 maf. 1-4)

Apr. 7 Usomaji wa Biblia: Mathayo 20 na 21

Wimbo Na. 107

Na. 1: Inamaanisha Nini Kubatizwa kwa “Jina la Baba na la Mwana na la Roho Takatifu”? (uw-SW uku. 98 fu. 9)

Na. 2: Mathayo 20:1-16

Na. 3: Kile Ambacho Kimethibitishwa Kuhusu Sababu ya Mungu Kuruhusu Uovu (kl-SW kur. 76-77 maf. 16-19)

Na. 4: Je, Kusema Katika Ndimi Kwathibitisha Kwamba Mtu Ana Roho Takatifu? (rs-SW uku. 236 fu. 5-uku. 237 fu. 4)

Apr. 14 Usomaji wa Biblia: Mathayo 22 na 23

Wimbo Na. 56

Na. 1: Kuishi Kulingana na Maana ya Ubatizo Wetu (uw-SW kur. 99-102 maf. 10-14)

Na. 2: Mathayo 23:1-15

Na. 3: Wewe Wasimama Upande wa Nani? (kl-SW kur. 78-79 maf. 20-23)

Na. 4: Kwa Nini Baadhi ya Wakristo wa Karne ya Kwanza Walisema kwa Ndimi? (rs-SW uku. 237 fu. 5-uku. 238 fu. 3)

Apr. 21 Usomaji wa Biblia: Mathayo 24 na 25

Wimbo Na. 193

Na. 1: Kuutambulisha Umati Mkubwa (uw-SW kur. 103-104 maf. 1-4)

Na. 2: Mathayo 24:32-44

Na. 3: Inakuwaje kwa Wapendwa Wetu Waliokufa? (kl-SW kur. 80-82 maf. 1-6)

Na. 4: Twaweza Kuwatambuaje Wale Walio na Roho ya Mungu? (rs-SW uku. 238 fu. 5-uku. 239 fu. 2)

Apr. 28 Pitio la Kuandika. Kamilisha Zekaria 1 hadi Mathayo 25

Wimbo Na. 6

Mei 5 Usomaji wa Biblia: Mathayo 26

Wimbo Na. 14

Na. 1: Ni Nini Kinachohitajiwa Ili Kuokoka Dhiki Kubwa? (uw-SW uku. 105 fu. 5)

Na. 2: Mathayo 26:31-35, 69-75

Na. 3: Kinachomaanishwa Hasa na Kurudi Mavumbini (kl-SW kur. 82-83 maf. 7-10)

Na. 4: Jinsi Wakristo wa Kweli Wanavyotambuliwa Leo (rs-SW uku. 239 maf. 3-5)

Mei 12 Usomaji wa Biblia: Mathayo 27 na 28

Wimbo Na. 102

Na. 1: Mathayo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 180-181 maf. 29-33)

Na. 2: Mathayo 27:11-26

Na. 3: Hali ya Wafu Ikoje? (kl-SW kur. 83-84 maf. 11-14)

Na. 4: Je, Karama ya Ndimi Ingeendelea kwa Muda Gani? (rs-SW uku. 239 fu. 6–​uku. 239 fu. 3)

Mei 19 Usomaji wa Biblia: Marko 1 na 2

Wimbo Na. 180

Na. 1: Utangulizi kwa Marko (si-SW kur. 181-183 maf. 1-11)

Na. 2: Marko 1:12-28

Na. 3: Wote Waliomo Katika Kumbukumbu la Yehova Watafufuliwa (kl-SW kur. 85-87 maf. 15-18)

Na. 4: Fundisho la Utatu Ni Nini, na Chanzo Chalo Ni Kipi? (rs-SW uku. 373 fu. 3-uku. 374 fu. 4)

Mei 26 Usomaji wa Biblia: Marko 3 na 4

Wimbo Na. 46

Na. 1: Sababu Kwa Nini Umati Mkubwa Waokoka Dhiki Kubwa (uw-SW kur. 106-107 maf. 6-8)

Na. 2: Marko 3:1-15

Na. 3: Ufufuo Ili Kwenda Wapi? (kl-SW kur. 88-89 maf. 19-22)

Na. 4: Je, Roho Takatifu Ni Mtu? (rs-SW uku. 375 maf. 1-4)

Juni 2 Usomaji wa Biblia: Marko 5 na 6

Wimbo Na. 220

Na. 1: Sababu Inayotufanya Tuhazini Paradiso Yetu ya Kiroho (uw-SW kur. 107-109 maf. 9-13)

Na. 2: Marko 5:21-24, 35-43

Na. 3: Ufalme wa Mungu na Kusudi Lao (kl-SW kur. 90-91 maf. 1-5)

Na. 4: Je, Yesu na Yehova Ni Mtu Yuleyule? (rs-SW uku. 375 fu. 5-uku. 377 fu. 2)

Juni 9 Usomaji wa Biblia: Marko 7 na 8

Wimbo Na. 207

Na. 1: Kwa Nini Kuna Warithi wa Ufalme Wachache Sana Duniani Leo? (uw-SW kur. 110-112 maf. 1-7)

Na. 2: Marko 7:24-37

Na. 3: Ufalme wa Mungu Ni Serikali (kl-SW kur. 91-92 maf. 6-7)

Na. 4: Je, Biblia Hufundisha Kwamba Yehova, Yesu, na Roho Takatifu Wote Wanalingana? (rs-SW uku. 378 fu. 1-uku. 379 fu. 2)

Juni 16 Usomaji wa Biblia: Marko 9 na 10

Wimbo Na. 11

Na. 1: Wana wa Kiroho—Wanajuaje? (uw-SW kur. 112-114 maf. 8-10)

Na. 2: Marko 9:14-29

Na. 3: Jinsi Tunavyojua Kwamba Ufalme wa Mungu Ni Halisi (kl-SW kur. 92-93 maf. 8-11)

Na. 4: Je, Biblia Hufundisha Kwamba Kila Mmoja wa Wale Wanaosemwa Kuwa Sehemu ya Utatu Ni Mungu? (rs-SW uku. 379 fu. 3-uku. 380 fu. 2)

Juni 23 Usomaji wa Biblia: Marko 11 na 12

Wimbo Na. 87

Na. 1: Umaana wa Mwadhimisho wa Ukumbusho Ni Nini? (uw-SW kur. 114-116 maf. 11-14)

Na. 2: Marko 11:12-25

Na. 3: Sababu Kwa Nini Ufalme wa Mungu Ndio Tumaini Pekee la Wanadamu (kl-SW kur. 94-95 maf. 12-13)

Na. 4: Jinsi Wanautatu Wanavyopotoa Maandiko Fulani (rs-SW uku. 380 fu. 3-uku. 382 fu. 1)

Juni 30 Usomaji wa Biblia: Marko 13 na 14

Wimbo Na. 38

Na. 1: Kutambua Tengenezo Linaloonekana la Yehova (uw-SW kur. 117-118 maf. 1-3)

Na. 2: Marko 14:12-26

Na. 3: Sababu Kwa Nini Yesu Hakuanza Kutawala Mara Baada ya Kwenda Mbinguni (kl-SW kur. 95-96 maf. 14-15)

Na. 4: Sababu Kwa Nini Maandiko Yanayomtaja Yehova Yaweza Kutumiwa Kumhusu Kristo (rs-SW uku. 382 fu. 2-3)

Julai 7 Usomaji wa Biblia: Marko 15 na 16

Wimbo Na. 187

Na. 1: Marko—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 186 maf. 31-33)

Na. 2: Marko 15:16-32

Na. 3: Nyakati Zilizowekwa Rasmi za Mataifa Zilianza na Kwisha Lini? (kl-SW kur. 96-97 maf. 16-18)

Na. 4: Maandiko Yatumiwayo Vibaya na Wanautatu (rs-SW uku. 383 fu. 1–​uku. 384 fu. 2)

Julai 14 Usomaji wa Biblia: Luka 1

Wimbo Na. 212

Na. 1: Utangulizi kwa Luka (si-SW kur. 187-188 maf. 1-9)

Na. 2: Luka 1:5-17

Na. 3: Hizi Ndizo Siku za Mwisho (kl-SW kur. 98-99 maf. 1-4)

Na. 4: Sababu Kwa Nini Yohana 1:1 na 8:58 Hayaungi Mkono Utatu (rs-SW uku. 384 fu. 3–​uku. 386 fu. 3)

Julai 21 Usomaji wa Biblia: Luka 2 na 3

Wimbo Na. 89

Na. 1: Tengenezo la Mungu Ni la Kitheokrasi (uw-SW kur. 118-120 maf. 4-7)

Na. 2: Luka 2:1-14

Na. 3: Ni Zipi Baadhi ya Sehemu za Siku za Mwisho? (kl-SW kur. 99-103 maf. 5-7)

Na. 4: Sababu Kwa Nini Kuchunguza Maneno Yanayozunguka Maandiko Ni Muhimu (rs-SW uku. 386 fu. 5–​uku. 389 fu. 2)

Julai 28 Usomaji wa Biblia: Luka 4 na 5

Wimbo Na. 92

Na. 1: Daraka la Kimaandiko la Wale Wenye Kuongoza (uw-SW kur. 120-122 maf. 8-12)

Na. 2: Luka 4:31-44

Na. 3: Mwenendo Uliopotoka wa Binadamu Uliotabiriwa Kuwapo Siku za Mwisho (kl-SW kur. 103-104 maf. 8-12)

Na. 4: Yesu Kristo na Yehova Ni Watu Mmoja-Mmoja Walio Tofauti (rs-SW uku. 389 fu. 3–​uku. 391 fu. 2)

Ago. 4 Usomaji wa Biblia: Luka 6 na 7

Wimbo Na. 213

Na. 1: Kuchanganua Uthamini Wetu kwa Tengenezo la Mungu (uw-SW kur. 123-124 maf. 13-14)

Na. 2: Luka 6:37-49

Na. 3: Sehemu Mbili za Pekee za Siku za Mwisho (kl-SW uku. 105 maf. 13-14)

Na. 4: Yesu Hakujifufua Mwenyewe Kutoka kwa Wafu, na Hakudai Kamwe Usawa Pamoja na Mungu (rs-SW uku. 391 fu. 4-uku. 392 fu. 3)

Ago. 11 Usomaji wa Biblia: Luka 8 na 9

Wimbo Na. 67

Na. 1: Kwa Nini Usikilize Shauri? (uw-SW kur. 125-127 maf. 1-4)

Na. 2: Luka 9:23-36

Na. 3: Itikia Uthibitisho wa Kwamba Hizi Ndizo Siku za Mwisho (kl-SW kur. 106-107 maf. 15-17)

Na. 4: Sababu Kwa Nini Kushikilia Itikadi ya Utatu Ni Hatari (rs-SW uku. 392 fu. 4–​uku. 393 fu. 2)

Ago. 18 Usomaji wa Biblia: Luka 10 na 11

Wimbo Na. 34

Na. 1: Mifano Mizuri ya Wale Waliokubali Shauri (uw-SW kur. 127-128 maf. 5-6)

Na. 2: Luka 11:37-51

Na. 3: Roho Waovu Wapo! (kl-SW uku. 108 maf. 1-3)

Na. 4: Kwa Nini Kuna Uovu Mwingi Sana? (rs-SW uku. 369 maf. 1-5)

Ago. 25 Pitio la Kuandika. Kamilisha Mathayo 26 hadi Luka 11

Wimbo Na. 160

Sept. 1 Usomaji wa Biblia: Luka 12 na 13

Wimbo Na. 163

Na. 1: Sitawisha Sifa Zenye Bei Kubwa (uw-SW kur. 128-130 maf. 7-11)

Na. 2: Luka 13:1-17

Na. 3: Malaika Waovu Wajiunga na Shetani (kl-SW uku. 109 maf. 4-5)

Na. 4: Kwa Nini Mungu Anaruhusu Uovu? (rs-SW uku. 370 fu. 1–​uku. 371 fu. 1)

Sept. 8 Usomaji wa Biblia: Luka 14 hadi 16

Wimbo Na. 124

Na. 1: Usikatae Nidhamu ya Yehova (uw-SW kur. 130-131 maf. 12-14)

Na. 2: Luka 14:1-14

Na. 3: Kataa Aina Zote za Uwasiliani-Roho (kl-SW uku. 111 maf. 6-8)

Na. 4: Jinsi Ambavyo Tumenufaika Kutokana na Kuruhusu kwa Mungu Uovu (rs-SW uku. 371 fu. 2- uku. 372 fu. 1)

Sept. 15 Usomaji wa Biblia: Luka 17 na 18

Wimbo Na. 200

Na. 1: Upendo Wawatambulisha Wakristo wa Kweli (uw-SW kur. 132-133 maf. 1-5)

Na. 2: Luka 17:22-37

Na. 3: Sababu Kwa Nini Biblia Hupinga Uwasiliani-Roho (kl-SW kur. 112-113 maf. 9-11)

Na. 4: Jinsi Biblia Huona Wanawake (rs-SW uku. 401 fu. 3-uku. 402 fu. 1)

Sept. 22 Usomaji wa Biblia: Luka 19 na 20

Wimbo Na. 145

Na. 1: La Kufanya Matatizo Yanapotokea (uw-SW uku. 134-135 maf. 6-9)

Na. 2: Luka 19:11-27

Na. 3: Biblia Yafunua Jinsi Roho Waovu Hutenda (kl-SW kur. 113-114 maf. 12-13)

Na. 4: Je, Kugawia Wanaume Ukichwa Ni Kushusha Heshima ya Wanawake? (rs-SW uku. 402 fu. 2-uku. 403 fu. 1)

Sept. 29 Usomaji wa Biblia: Luka 21 na 22

Wimbo Na. 86

Na. 1: Tatua Matatizo Kimaandiko (uw-SW kur. 135-136 maf. 10-13)

Na. 2: Luka 22:24-38

Na. 3: Jinsi ya Kukinza Roho Waovu (kl-SW kur. 114-115 maf. 14-15)

Na. 4: Je, Wanawake Wawe Wahudumu? (rs-SW uku. 403 maf. 2–3)

Okt. 6 Usomaji wa Biblia: Luka 23 na 24

Wimbo Na. 88

Na. 1: Luka—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 192-193 maf. 30-35)

Na. 2: Luka 23:32-49

Na. 3: Jinsi ya Kuimarisha Imani Yako (kl-SW kur. 115-116 maf. 16-17)

Na. 4: Kwa Nini Wanawake Wakristo Huvaa Vifuniko vya Kichwa Katika Pindi Fulani-Fulani? (rs-SW uku. 404 fu. 1–​uku. 405 fu. 1)

Okt. 13 Usomaji wa Biblia: Yohana 1 hadi 3

Wimbo Na. 31

Na. 1: Utangulizi kwa Yohana (si-SW kur. 193-195 maf. 1-9)

Na. 2: Yohana 1:19-34

Na. 3: Endelea na Pigano Lako Dhidi ya Roho Waovu (kl-SW kur. 116-117 maf. 18-20)

Na. 4: Je, Inafaa kwa Wanawake Kujipaka Marashi au Kuvaa Vito? (rs-SW uku. 405 fu. 2-uku. 406 fu. 1)

Okt. 20 Usomaji wa Biblia: Yohana 4 na 5

Wimbo Na. 35

Na. 1: Tafuta Njia za ‘Kupanuka’ Katika Upendo (uw-SW kur. 137-138 maf. 14-17)

Na. 2: Yohana 4:39-54

Na. 3: Kuishi Maisha ya Kimungu Huleta Furaha (kl-SW kur. 118-119 maf. 1-4)

Na. 4: Ni Nini Ulio Wakati Ujao wa Ulimwengu Huu na Kiongozi Wao? (rs-SW uku. 359 fu. 1–​uku. 360 fu. 3)

Okt. 27 Usomaji wa Biblia: Yohana 6 na 7

Wimbo Na. 150

Na. 1: Zoea Utawa Nyumbani (uw-SW uku. 139 maf. 1-2)

Na. 2: Yohana 6:52-71

Na. 3: Ufuatiaji-Haki Hutokeza Furaha (kl-SW kur. 119-120 maf. 5-6)

Na. 4: Wakristo wa Kweli Wapaswa Kuuonaje Ulimwengu? (rs-SW uku. 360 fu. 4–​uku. 361 fu. 4)

Nov. 3 Usomaji wa Biblia: Yohana 8 na 9

Wimbo Na. 48

Na. 1: Isemayo Biblia Kuhusu Ndoa, Talaka, na Kutengana (uw-SW uku. 140 fu. 3)

Na. 2: Yohana 9:18-34

Na. 3: Ukarimu Huleta Furaha (kl-SW kur. 120-121 maf. 7-8)

Na. 4: *td 15A au td-SW 25B Ni 144,000 Pekee Waendao Mbinguni

Nov. 10 Usomaji wa Biblia: Yohana 10 na 11

Wimbo Na. 117

Na. 1: Mambo ya Maana Sana Katika Ndoa Yenye Mafanikio (uw-SW kur. 140-141 maf. 4-5)

Na. 2: Yohana 10:22-39

Na. 3: Linda Uwezo Wako wa Kufikiri na Uepuke Lililo Baya (kl-SW kur. 121-122 maf. 9-10)

Na. 4: *td 16B au td-SW 27A Moto Ni Mfano wa Maangamizi ya Daima

Nov. 17 Usomaji wa Biblia: Yohana 12 na 13

Wimbo Na. 158

Na. 1: Timiza Daraka Lako Katika Mpango wa Mungu wa Familia (uw-SW kur. 142-143 maf. 6-10)

Na. 2: Yohana 12:1-16

Na. 3: Uaminifu kwa Mwenzi Wako Huleta Furaha Katika Ndoa (kl-SW kur. 122-123 maf. 11-13)

Na. 4: *td 17A au td-SW 39B Maadhimisho ya Kila Mwaka na Watumishi wa Kweli wa Yehova

Nov. 24 Usomaji wa Biblia: Yohana 14 hadi 16

Wimbo Na. 63

Na. 1: Biblia na Iwe Chanzo Chako cha Shauri (uw-SW uku. 144 maf. 11-13)

Na. 2: Yohana 16:1-16

Na. 3: Usiwe Sehemu ya Ulimwengu (kl-SW kur. 123-125 maf. 14-15)

Na. 4: *td 18B au td-SW 36B Ibada ya Sanamu Ilikuwa Mtego kwa Waisraeli

Des. 1 Usomaji wa Biblia: Yohana 17 na 18

Wimbo Na. 114

Na. 1: Sababu Kwa Nini Sheria ya Musa Hutupendeza (uw-SW kur. 146-147 maf. 1-4)

Na. 2: Yohana 18:1-14

Na. 3: Sababu Kwa Nini Wakristo wa Kweli Hawaadhimishi Krismasi au Sikukuu za Kuzaliwa (kl-SW uku. 126 maf. 16-17)

Na. 4: *td 19A au td-SW 26A Kuna Dini Moja Tu ya Kweli

Des. 8 Usomaji wa Biblia: Yohana 19 hadi 21

Wimbo Na. 138

Na. 1: Yohana—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 198-199 maf. 30-35)

Na. 2: Yohana 19:25-37

Na. 3: Endelea Kuadhimisha Mlo wa Jioni wa Bwana (kl-SW uku. 127 fu. 18)

Na. 4: *td 20A au td-SW 55A Julisha Jina la Mungu

Des. 15 Usomaji wa Biblia: Matendo 1 hadi 3

Wimbo Na. 41

Na. 1: Utangulizi kwa Matendo (si-SW kur. 199-200 maf. 1-8)

Na. 2: Matendo 1:1-14

Na. 3: Jinsi Kanuni za Biblia Hutumika Kuhusu Kazi na Vitumbuizo (kl-SW kur. 127-128 maf. 19-20)

Na. 4: *td 20C au td-SW 55D Ni Zipi Sifa Kuu za Mungu?

Des. 22 Usomaji wa Biblia: Matendo 4 hadi 6

Wimbo Na. 113

Na. 1: Sababu za Kimaandiko Zinazotufanya Tusiwe Chini ya Sheria ya Musa (uw-SW kur. 147-148 maf. 5-6)

Na. 2: Matendo 5:27-42

Na. 3: Onyesha Staha kwa Uhai na Damu (kl-SW kur. 128-129 maf. 21-23)

Na. 4: *td 21A au td-SW 22A Ni Nini Kilicho Chanzo cha Mashahidi wa Yehova?

Des. 29 Pitio la Kuandika. Kamilisha Luka 12 hadi Matendo 6

Wimbo Na. 144

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki