Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 17
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Daudi amshinda Goliathi (1-58)

        • Goliathi awatukana Waisraeli (8-10)

        • Daudi akubali kupigana na Goliathi (32-37)

        • Daudi apigana kwa jina la Yehova (45-47)

1 Samweli 17:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kambi zao.”

Marejeo

  • +Amu 3:1, 3; 1Sa 9:16; 14:52
  • +2Nya 28:18
  • +Yos 15:20, 35; Yer 34:7
  • +1Nya 11:12, 13

1 Samweli 17:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Nchi Tambarare ya Chini ya.”

Marejeo

  • +1Sa 21:9

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    ‘Nchi Nzuri’, uku. 16

  • Fahirishi ya Machapisho

    gl 16

1 Samweli 17:3

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/1990, uku. 16

1 Samweli 17:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Alikuwa na urefu wa mita 2.9 hivi (futi 9 na inchi 5.75). Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +1Sa 17:23
  • +Yos 11:22; 2Sa 21:20, 21

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016 kur. 9, 10-13

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2006, uku. 9

    1/1/1989, uku. 18

    “Kila Andiko,” uku. 56

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 5/15 9

1 Samweli 17:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Karibu kilogramu 57. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +1Sa 17:38, 39; 1Fa 22:34

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2006, uku. 9

    1/1/1989, kur. 18-19

    “Kila Andiko,” uku. 56

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 5/15 9

1 Samweli 17:6

Marejeo

  • +1Sa 17:45

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 169

1 Samweli 17:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Karibu kilogramu 6.84. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +1Nya 20:5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 169

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2006, uku. 9

    1/1/1989, kur. 18-19

    “Kila Andiko,” uku. 56

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 5/15 9

1 Samweli 17:8

Marejeo

  • +Hes 33:55

1 Samweli 17:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Nataka kushindana na.”

Marejeo

  • +1Sa 17:26; 2Fa 19:22

1 Samweli 17:12

Marejeo

  • +Ru 4:22
  • +Mwa 35:16, 19; Ru 1:2
  • +1Sa 17:58; Mik 5:2; Mt 2:6
  • +1Nya 2:13-15

1 Samweli 17:13

Marejeo

  • +Hes 1:3
  • +1Sa 16:6
  • +1Sa 16:8
  • +1Sa 16:9

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    9/1/2011, uku. 29

  • Fahirishi ya Machapisho

    w11 9/1 29

1 Samweli 17:14

Marejeo

  • +1Nya 2:13, 15

1 Samweli 17:15

Marejeo

  • +1Sa 16:11, 19

1 Samweli 17:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Efa ilikuwa sawa na lita 22 au kilogramu 13 hivi. Angalia Nyongeza B14.

1 Samweli 17:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “maziwa.”

1 Samweli 17:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Nchi Tambarare ya Chini ya.”

Marejeo

  • +1Sa 17:2; 21:9
  • +1Sa 9:16, 17

1 Samweli 17:22

Marejeo

  • +1Sa 17:17, 18

1 Samweli 17:23

Marejeo

  • +1Sa 17:4
  • +1Sa 17:10

1 Samweli 17:24

Marejeo

  • +1Sa 17:11

1 Samweli 17:25

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kushindana na.”

Marejeo

  • +1Sa 17:10
  • +Yos 15:16; 1Sa 14:49; 18:17, 21

1 Samweli 17:26

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “ashindane na.”

Marejeo

  • +1Sa 17:10; Yer 10:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 10

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2006, uku. 8

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 5/15 8

1 Samweli 17:28

Marejeo

  • +1Sa 16:6, 7; 1Nya 2:13
  • +1Sa 17:20

1 Samweli 17:30

Marejeo

  • +1Sa 17:26
  • +1Sa 17:25

1 Samweli 17:32

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “asiogope.”

Marejeo

  • +1Sa 16:18

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016 kur. 10-11

1 Samweli 17:33

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mwanamume wa vita.”

Marejeo

  • +1Sa 17:42

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:34

Marejeo

  • +Isa 31:4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    9/1/2011, uku. 27

  • Fahirishi ya Machapisho

    w11 9/1 27

1 Samweli 17:35

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “utaya wake.” Tnn., “ndevu zake.”

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016 kur. 9-10

    Mnara wa Mlinzi,

    9/1/2011, uku. 27

  • Fahirishi ya Machapisho

    w11 9/1 27

1 Samweli 17:36

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “ameshindana na.”

Marejeo

  • +1Sa 17:10; Yer 10:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    7/15/1993, uku. 25

1 Samweli 17:37

Marejeo

  • +Kum 7:21; 2Fa 6:16; Ebr 11:32-34

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:38

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:39

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:40

Marejeo

  • +Amu 20:15, 16

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:41

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 12

1 Samweli 17:42

Marejeo

  • +1Sa 16:12; 17:33

1 Samweli 17:43

Marejeo

  • +1Sa 24:14; 2Sa 16:9; 2Fa 8:13

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 11

1 Samweli 17:45

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “umeshindana naye.”

Marejeo

  • +1Sa 17:4, 6
  • +2Sa 5:10; Ebr 11:32-34
  • +1Sa 17:10; 2Fa 19:22

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 21

1 Samweli 17:46

Marejeo

  • +Kum 9:1-3; Yos 10:8
  • +Kut 9:16; Kum 28:10; 1Fa 8:43; 2Fa 19:19; Da 3:29

1 Samweli 17:47

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Na kutaniko hili lote litajua.”

Marejeo

  • +Zb 44:6, 7; Zek 4:6
  • +2Nya 20:15; Met 21:31
  • +Kum 20:4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 12

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/1989, kur. 19, 28

1 Samweli 17:49

Marejeo

  • +1Sa 17:37; 2Sa 21:22

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote),

    Na. 5 2016, uku. 12

    Mnara wa Mlinzi,

    1/1/1989, kur. 19, 21

1 Samweli 17:50

Marejeo

  • +Amu 3:31; 15:15, 16; 1Sa 17:47

1 Samweli 17:51

Marejeo

  • +1Sa 21:9
  • +Kum 28:7; Yos 23:10; Ebr 11:32-34

1 Samweli 17:52

Marejeo

  • +1Sa 17:2, 19
  • +Yos 15:20, 45
  • +Yos 15:20, 36

1 Samweli 17:54

Marejeo

  • +1Sa 21:9

1 Samweli 17:55

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Kama nafsi yako inavyoishi.”

Marejeo

  • +1Sa 14:50
  • +1Sa 16:19, 21

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    The Watchtower,

    3/15/2005, kur. 23-24

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 3/15 23-24

1 Samweli 17:57

Marejeo

  • +1Sa 17:54

1 Samweli 17:58

Marejeo

  • +Ru 4:22; 1Sa 16:1; 1Nya 2:13, 15; Mt 1:6; Lu 3:23, 32; Mdo 13:22
  • +1Sa 17:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    8/15/2007, uku. 19

    8/1/2007, uku. 31

  • Fahirishi ya Machapisho

    w07 8/1 31; w07 8/15 19

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 17:1Amu 3:1, 3; 1Sa 9:16; 14:52
1 Sam. 17:12Nya 28:18
1 Sam. 17:1Yos 15:20, 35; Yer 34:7
1 Sam. 17:11Nya 11:12, 13
1 Sam. 17:21Sa 21:9
1 Sam. 17:41Sa 17:23
1 Sam. 17:4Yos 11:22; 2Sa 21:20, 21
1 Sam. 17:51Sa 17:38, 39; 1Fa 22:34
1 Sam. 17:61Sa 17:45
1 Sam. 17:71Nya 20:5
1 Sam. 17:8Hes 33:55
1 Sam. 17:101Sa 17:26; 2Fa 19:22
1 Sam. 17:12Ru 4:22
1 Sam. 17:12Mwa 35:16, 19; Ru 1:2
1 Sam. 17:121Sa 17:58; Mik 5:2; Mt 2:6
1 Sam. 17:121Nya 2:13-15
1 Sam. 17:13Hes 1:3
1 Sam. 17:131Sa 16:6
1 Sam. 17:131Sa 16:8
1 Sam. 17:131Sa 16:9
1 Sam. 17:141Nya 2:13, 15
1 Sam. 17:151Sa 16:11, 19
1 Sam. 17:191Sa 17:2; 21:9
1 Sam. 17:191Sa 9:16, 17
1 Sam. 17:221Sa 17:17, 18
1 Sam. 17:231Sa 17:4
1 Sam. 17:231Sa 17:10
1 Sam. 17:241Sa 17:11
1 Sam. 17:251Sa 17:10
1 Sam. 17:25Yos 15:16; 1Sa 14:49; 18:17, 21
1 Sam. 17:261Sa 17:10; Yer 10:10
1 Sam. 17:281Sa 16:6, 7; 1Nya 2:13
1 Sam. 17:281Sa 17:20
1 Sam. 17:301Sa 17:26
1 Sam. 17:301Sa 17:25
1 Sam. 17:321Sa 16:18
1 Sam. 17:331Sa 17:42
1 Sam. 17:34Isa 31:4
1 Sam. 17:361Sa 17:10; Yer 10:10
1 Sam. 17:37Kum 7:21; 2Fa 6:16; Ebr 11:32-34
1 Sam. 17:40Amu 20:15, 16
1 Sam. 17:421Sa 16:12; 17:33
1 Sam. 17:431Sa 24:14; 2Sa 16:9; 2Fa 8:13
1 Sam. 17:451Sa 17:4, 6
1 Sam. 17:452Sa 5:10; Ebr 11:32-34
1 Sam. 17:451Sa 17:10; 2Fa 19:22
1 Sam. 17:46Kum 9:1-3; Yos 10:8
1 Sam. 17:46Kut 9:16; Kum 28:10; 1Fa 8:43; 2Fa 19:19; Da 3:29
1 Sam. 17:47Zb 44:6, 7; Zek 4:6
1 Sam. 17:472Nya 20:15; Met 21:31
1 Sam. 17:47Kum 20:4
1 Sam. 17:491Sa 17:37; 2Sa 21:22
1 Sam. 17:50Amu 3:31; 15:15, 16; 1Sa 17:47
1 Sam. 17:511Sa 21:9
1 Sam. 17:51Kum 28:7; Yos 23:10; Ebr 11:32-34
1 Sam. 17:521Sa 17:2, 19
1 Sam. 17:52Yos 15:20, 45
1 Sam. 17:52Yos 15:20, 36
1 Sam. 17:541Sa 21:9
1 Sam. 17:551Sa 14:50
1 Sam. 17:551Sa 16:19, 21
1 Sam. 17:571Sa 17:54
1 Sam. 17:58Ru 4:22; 1Sa 16:1; 1Nya 2:13, 15; Mt 1:6; Lu 3:23, 32; Mdo 13:22
1 Sam. 17:581Sa 17:12
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
  • 31
  • 32
  • 33
  • 34
  • 35
  • 36
  • 37
  • 38
  • 39
  • 40
  • 41
  • 42
  • 43
  • 44
  • 45
  • 46
  • 47
  • 48
  • 49
  • 50
  • 51
  • 52
  • 53
  • 54
  • 55
  • 56
  • 57
  • 58
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 17:1-58

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

17 Sasa Wafilisti+ wakakusanya majeshi yao* kwa ajili ya vita. Walikusanyika huko Soko,+ jiji la Yuda, wakapiga kambi kati ya Soko na Azeka,+ kule Efes-damimu.+ 2 Sauli na wanaume wa Israeli wakakusanyika na kupiga kambi katika Bonde la* Ela,+ nao wakajipanga kivita ili kupigana na Wafilisti. 3 Wafilisti walikuwa upande mmoja wa mlima, na Waisraeli walikuwa upande ule mwingine, na bonde lilikuwa katikati yao.

4 Kisha shujaa mmoja akatoka katika kambi za Wafilisti; aliitwa Goliathi,+ kutoka Gathi,+ alikuwa na urefu wa mikono sita na shubiri moja.* 5 Alikuwa na kofia ya shaba kichwani, naye alivaa koti la vita lenye magamba yanayolaliana. Koti hilo la vita la shaba+ lilikuwa na uzito wa shekeli 5,000.* 6 Alikuwa na mabamba ya shaba yaliyokinga miguu yake na fumo+ la shaba lililoning’inia katikati ya mabega yake. 7 Mpini wa mbao wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa wafumaji wa nguo,+ na kichwa cha chuma cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa shekeli 600;* na mtu aliyembebea ngao alitembea mbele yake. 8 Basi akasimama na kuviita vikosi vya Israeli+ akisema: “Kwa nini mmekuja kujipanga kivita? Je, mimi si Mfilisti nanyi je, si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mwanamume, aje kupigana nami. 9 Akiweza kupigana nami na kuniua, tutakuwa watumishi wenu. Lakini nikimshinda na kumuua, mtakuwa watumishi wetu, nanyi mtatutumikia.” 10 Kisha Mfilisti huyo akasema: “Ninavitukana* vikosi vya Israeli+ leo. Nipeni mwanamume, nipigane naye!”

11 Sauli na Waisraeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti huyo, wakashikwa na hofu na kuogopa sana.

12 Basi Daudi alikuwa mwana wa Yese,+ Mwefrathi+ kutoka mji wa Bethlehemu+ wa Yuda, ambaye alikuwa na wana wanane+ na ambaye katika siku za Sauli alikuwa tayari amezeeka. 13 Wana watatu wakubwa wa Yese walikuwa wameenda na Sauli vitani.+ Majina ya wana hao watatu walioenda vitani ni Eliabu+ mzaliwa wake wa kwanza, Abinadabu+ mwana wake wa pili, na Shamma mwana wake wa tatu.+ 14 Daudi ndiye aliyekuwa mdogo zaidi,+ na wale watatu wakubwa walikuwa wameenda pamoja na Sauli.

15 Daudi alikuwa akienda na kurudi kutoka kwa Sauli ili kuchunga kondoo+ wa baba yake huko Bethlehemu. 16 Wakati huo, yule Mfilisti alikuwa akija na kuwadhihaki kila asubuhi na kila jioni kwa siku 40.

17 Ndipo Yese akamwambia Daudi mwana wake: “Tafadhali, chukua hii efa* ya nafaka iliyokaangwa na mikate hii kumi, uwapelekee haraka ndugu zako kambini. 18 Nawe umpelekee mkuu wa elfu mafungu haya kumi ya jibini;* pia, angalia ndugu zako wanaendeleaje na uniletee kitu fulani kutoka kwao.” 19 Walikuwa pamoja na Sauli na wanaume wengine wote wa Israeli katika Bonde la* Ela,+ wakipigana na Wafilisti.+

20 Kwa hiyo Daudi akaamka asubuhi na mapema na kuwaacha kondoo mikononi mwa mtu mwingine; kisha akapakia vitu hivyo na kwenda kama Yese alivyokuwa amemwamuru. Alipofika kambini, jeshi lilikuwa likienda kwenye uwanja wa vita huku likipiga kelele za vita. 21 Waisraeli na Wafilisti wakajipanga kivita wakikabiliana uso kwa uso. 22 Mara moja Daudi akaiacha mizigo yake mikononi mwa mtu aliyetunza mizigo, akakimbia kwenda kwenye uwanja wa vita. Alipofika, akaanza kuulizia habari za ndugu zake.+

23 Alipokuwa akizungumza nao, akaja yule Mfilisti shujaa aliyeitwa Goliathi,+ kutoka Gathi. Alitoka katika vikosi vya Wafilisti, akasema maneno yaleyale aliyozoea kusema,+ na Daudi akamsikia. 24 Wanaume wote wa Israeli walipomwona mwanamume huyo, wakaogopa sana na kumkimbia.+ 25 Wanaume wa Israeli walikuwa wakisema: “Je, mnamwona mwanamume yule anayekuja? Anakuja kuwatukana* Waisraeli.+ Mfalme atampa utajiri mwingi mtu atakayemuua mwanamume huyo, atampa pia binti yake mwenyewe,+ naye ataiondolea wajibu nyumba ya baba yake katika Israeli.”

26 Daudi akaanza kuwauliza wanaume waliokuwa wamesimama karibu naye: “Mtu atakayemuua yule Mfilisti na kuwaondolea Waisraeli aibu atafanyiwa nini? Kwani huyu Mfilisti asiyetahiriwa ni nani hata avitukane* vikosi vya Mungu aliye hai?”+ 27 Basi watu hao wakamwambia maneno yaleyale yaliyokuwa yamesemwa: “Hivi ndivyo atakavyofanyiwa mwanamume atakayemuua.” 28 Eliabu ndugu yake mkubwa+ alipomsikia Daudi akizungumza na wanaume hao, akamkasirikia Daudi na kumwambia: “Kwa nini umeshuka huku? Na wale kondoo wachache nyikani umemwachia nani?+ Najua vizuri kimbelembele chako na nia mbaya ya moyo wako; umeshuka tu ili kutazama vita.” 29 Daudi akamwambia: “Sasa nimefanya nini? Nilikuwa nikiuliza swali tu!” 30 Ndipo Daudi akamwacha, akamgeukia mtu mwingine na kumuuliza swali lilelile,+ na watu wakamjibu vilevile kama mwanzoni.+

31 Watu wakasikia maneno aliyosema Daudi, wakamwambia Sauli. Basi Sauli akaagiza aitwe. 32 Daudi akamwambia Sauli: “Mtu yeyote asife moyo* kwa sababu yake. Mimi mtumishi wako nitaenda kupigana na huyo Mfilisti.”+ 33 Lakini Sauli akamwambia Daudi: “Huwezi kwenda kupigana na huyo Mfilisti, kwa sababu wewe ni mvulana tu,+ naye amekuwa mwanajeshi* tangu alipokuwa kijana.” 34 Ndipo Daudi akamwambia Sauli: “Mimi mtumishi wako nimekuwa nikichunga kondoo wa baba yangu, na simba+ akaja, na pia dubu, na kila mmoja wao akamchukua kondoo kutoka kundini. 35 Nilimfuata, nikamuua na kumwokoa kondoo kutoka kinywani mwake. Aliporuka ili kunishambulia, nilimkamata manyoya yake,* nikampiga, na kumuua. 36 Mimi mtumishi wako nilimuua simba na dubu pia, na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amevitukana* vikosi vya Mungu aliye hai.”+ 37 Kisha Daudi akasema: “Yehova, aliyeniokoa kutoka katika makucha ya simba na ya dubu, ndiye atakayeniokoa kutoka mikononi mwa Mfilisti huyo.”+ Ndipo Sauli akamwambia Daudi: “Nenda, na Yehova awe pamoja nawe.”

38 Basi Sauli akamvisha Daudi mavazi yake. Akamvisha kofia ya shaba kichwani, halafu akamvisha koti la vita. 39 Kisha Daudi akajifunga upanga wake juu ya mavazi yake, akajaribu kutembea lakini akashindwa kwa sababu hakuwa ameyazoea. Basi Daudi akamwambia Sauli: “Siwezi kwenda nikiwa nimevaa vitu hivi, kwa maana sijavizoea.” Kwa hiyo Daudi akavivua. 40 Kisha akachukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe matano laini kutoka katika bonde la kijito, akayaweka kwenye kifuko ndani ya mfuko wake wa mchungaji, na kombeo+ lilikuwa mkononi mwake. Naye akaanza kumkaribia huyo Mfilisti.

41 Mfilisti huyo akaanza kumkaribia Daudi zaidi na zaidi, na mtu aliyembebea ngao alikuwa mbele yake. 42 Mfilisti huyo alipotazama na kumwona Daudi, akaanza kumdhihaki kwa dharau kwa sababu alikuwa tu mvulana mwekundu mwenye sura nzuri.+ 43 Basi Mfilisti huyo akamuuliza Daudi: “Je, mimi ni mbwa+ hivi kwamba unijie na vijiti?” Ndipo huyo Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. 44 Akamwambia Daudi: “Nikaribie tu, nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.”

45 Daudi akamjibu hivi huyo Mfilisti: “Unakuja kupigana nami kwa upanga, mkuki, na fumo,+ lakini mimi naja kupigana nawe kwa jina la Yehova wa majeshi,+ Mungu wa vikosi vya Israeli, ambaye umemtukana.*+ 46 Siku hii ya leo Yehova atakutia wewe mikononi mwangu,+ nami nitakuua na kukata kichwa chako; na siku ya leo nitawapa ndege wa angani na wanyama mwitu wa dunia maiti za kambi ya Wafilisti; na watu wote duniani watajua kwamba kuna Mungu katika Israeli.+ 47 Na watu wote waliokusanyika hapa watajua* kwamba Yehova haokoi kwa upanga wala kwa mkuki,+ kwa sababu vita ni vya Yehova,+ naye atawatia ninyi nyote mikononi mwetu.”+

48 Basi Mfilisti huyo akasimama, akazidi kukaribia ili akutane na Daudi, lakini Daudi akakimbia haraka kuelekea kwenye uwanja wa vita kukutana na Mfilisti huyo. 49 Daudi akautia mkono wake ndani ya mfuko wake, akachukua jiwe kutoka humo, na kulirusha kwa kombeo. Akampiga Mfilisti huyo kwenye paji la uso, na jiwe hilo likapenya katika paji la uso wake, akaanguka chini kifudifudi.+ 50 Basi Daudi akamshinda Mfilisti huyo kwa kombeo na jiwe; alimpiga Mfilisti huyo na kumuua, ingawa Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.+ 51 Daudi akaendelea kukimbia na kusimama juu yake. Kisha akaushika upanga wa Mfilisti+ huyo na kuuchomoa kutoka katika ala yake, akahakikisha kwamba amekufa kwa kumkata kichwa kwa upanga huo. Wafilisti walipoona kwamba shujaa wao amekufa, wakakimbia.+

52 Kisha wanaume wa Israeli na Yuda wakainuka na kuanza kupiga kelele na kuwafuatia Wafilisti kuanzia bondeni+ mpaka kwenye malango ya Ekroni,+ na maiti za Wafilisti waliouawa zilienea barabarani kuanzia Shaaraimu,+ mpaka Gathi na Ekroni. 53 Waisraeli waliporudi baada ya kuwafuatia vikali Wafilisti, walipora kambi zao.

54 Halafu Daudi akachukua kichwa cha yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu, lakini akaziweka silaha za Mfilisti huyo ndani ya hema lake mwenyewe.+

55 Sauli alipomwona Daudi akienda kupigana na Mfilisti huyo, alimuuliza hivi Abneri+ mkuu wa jeshi: “Abneri, mvulana huyu ni mwana wa nani?”+ Abneri akajibu: “Kwa hakika kama unavyoishi,* Ee mfalme, mimi sijui!” 56 Mfalme akasema: “Tafuta mvulana huyu ni mwana wa nani.” 57 Basi mara tu Daudi aliporudi baada ya kumuua huyo Mfilisti, Abneri akamchukua na kumpeleka mbele ya Sauli akiwa na kichwa cha huyo Mfilisti+ mkononi mwake. 58 Ndipo Sauli akamuuliza: “Mvulana, wewe ni mwana wa nani?” Daudi akamjibu: “Mimi ni mwana wa mtumishi wako Yese+ Mbethlehemu.”+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki